Asili Halisi ya Mwenge wa Uhuru: Siri Yafichuka

Wengi wetu tumebahatika aidha kushiriki au hata kuchangia mbio za Mwenge wa uhuru wa Tanganyia (Tanzania), lakini ni wangapi kati yetu tunajuwa asili haswa ya huo Mwenge!?

Ipo siri kubwa kuhusu Mwenge wa Uhuru ambao hukimbizwa nchi nzima. Wapo wanaodhani kwamba aliyeleta mabadiliko katika nchi kwa kuanzishwa kwa mwenge huo ni Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere lakini kiukweli haswa Mwalimu Nyerere si mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru.

Mnajimu maarufu ambaye sasa ni marehemu, Sheikh Yahya Hussein aliwahi kusema na ikaandikwa kwamba mvumbuzi wa wazo la kuwa na Mwenge wa Uhuru ni Forojo Ganze ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Forojo Ganze aliyezaliwa mwaka 1902 alifuatana na wazee wengine kwenda kwenye zindiko Bagamoyo ili Mwalimu Julius Nyerere aweze kutawala vema.

Wazee hao na miaka yao ya kuzaliwa kwenye mabano ni Mzee Ramadhan (1920), Ally Tarazo (1929), Komwe wa Komwe (1918) na Sheikh Yahya Hussein (1925).

Wazee hao walipewa kazi hiyo na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote, zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo na baadaye Mwalimu Nyerere alipelekwa Bagamoyo, akachinjwa mbuzi na Nyerere akaambiwa atambuke (aruke damu) baada ya kutokula kutwa nzima (alifunga), jambo ambalo aliwahi kukiri hadharani katika moja ya hotuba zake.

Sheikh Yahya Hussein alinukuliwa akisema hata hivyo, katika mashimo yale Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia katika moja ya shimo kwa ajili ya kuuliza mizimu na aliwaacha wenzake nje wakimngoja ili kujua atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es Salaam.

Utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema, zindiko la Bagamoyo linafanya kazi.

Kilichoshangaza, alisema ni mtu huyo kuingia shimoni na kukaa siku kumi na siku ya kumi na moja alipotoka alikuwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa, na alikuwa akiongea lugha isiyojulikana.

"Tulimchukua akiwa hoi hadi Ikulu Dar es Salaam na tulimfikisha mbele ya Mwalimu Nyerere na akatamka maneno yanayotumika au yanayohusu Mwenge wa Uhuru kwa Kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho," alisema Sheikh Yahya.

Akinukuu maneno hayo Sheikh Yahya alisema Forojo alimwambia Nyerere:

"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau."

Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwalimu Nyerere, Ganze alikata roho na siku chache baadaye Mwalimu Nyerere akayafanyia kazi maneno yake na kuanzisha Mwenge wa Uhuru ambao ulipandishwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Alexander Nyirenda aliyekuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)," alisema Sheikh Yahya.

Hata hivyo, mtaalam huyo wa unajimu alisema kilichowashangaza wengi ni maneno yaliyoongozwa yasemayo "UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI" akahoji ina maana ndani ya nchi tubaki gizani? Sheikh Yahya Hussein alisema anashangazwa kwa nini Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru kwani baada ya mazishi ya Forojo, mwenge ulianzishwa ambao ulikimbizwa nchi nzima mara tu baada ya uhuru mwaka 1961 na unaendelea kukimbizwa hadi sasa.

Nyerere alimuagiza Sheikh Yahya Hussein atafsiri maana ya ile namba 115 aliyokuwa ameiandika mkononi Forojo akamwambia:

"Namba 115 maana yake utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na Taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38," na ndivyo ilivyokuwa.
Mwaka 1999 Mwalimu Nyerere alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru na 77+38 =115, namba aliyoiandika Forojo Ganze mkononi.
Nikiwa mdogo niliwahi kukaa karibu na wale jamaa wanabeba mwenge. Kuna kipindi wanauchukua, wanauzingira na kuutamkia maneno yasiyoeleweka!
Kuanzia siku hiyo sikutaka kabisa kujihusisha na mwenge!
Kifupi kabisa! Mwenge ni tambiko!
 
Kwahiyo walitufanya mazezeta?...Mzee Yahya Hussein alikuwa ni mtu aliyejua vitu vingi kuhusu hii nchi, Kati ya wazee wa Kiswahili waliokuwa wa mwanzo kuwa na exposure basi na yeye yumo, ishu za numerology ambapo alibobea ni kama Inakuja halafu inakataa.
 
"Tulimchukua akiwa hoi hadi Ikulu Dar es Salaam na tulimfikisha mbele ya Mwalimu Nyerere na akatamka maneno yanayotumika au yanayohusu Mwenge wa Uhuru kwa Kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho,"
 
Hayo uliyofanya kwenye mikesha ya Mwenge ni maagano ya ulimwengu wa kiroho na mpaka Sasa bado umeyabeba..

Omba toba...ungama
Duh...!.
Hivi Adam na Eva, waliungama kula lile tunda?
hivi Caine aliungama ?
Yakobo aliungama kuiba urithi wa Essau?
Yuda alipompachika mimba Tamari aliungama?
Wale mabinti B' wa Lutu, waliungama walichomfanya baba yao akawatundika ujau...?
King David aliungama alichomfanya Uria na kumtwaa mke wake Bersheeba na kumfanya mkewe?
Kuna vitu vinatokea, Mungu hajali sana, anakubariki. Mimi ni baraka!, nina watoto 9 wajukuu 7!.

P
 
Habari hii siyo ya kweli. Yamepachikwa maneno mengi ya uwongo kwenye maneno ya ukweli.

Mwenge ulianzishwa na Nyerere kwa kushauriana na wakuu wa Kanisa ili kuomba baraka za Mungu kwa taifa jipya.

Ikumbukwe kuwa waingereza walitaka kuipa uhuru Tanganyika mwezi wa September, lakini Mwalimu Nyerere alikataa, akitaka uhuru wa Tanganyika uendane na tukio la kiimani. Tukio lililokuwa karibu ni sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili.Mwalimu aliridhia Tanganyika ipate uhuru siku hiyo, huku akiomba Mama Bikira Maria awe mwombezi wa Taifa hili:

Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili inaadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 8 Desemba, lakini nchini Tanzania huadhimishwa rasmi kitaifa tarehe 9 Desemba.

Kwa kuzingatia maneno ya Kristo kuwa YEYE ni mwanga wa Ulimwengu, na moto hasa mshumaa hutumika kama alama ya mwanga wa Kristo, mwalimu Nyerere alitaka mwenge utumike kama alama ya mwanga wa Kristo, na katika adhimisho hilo la kuzindua mwenge, Nyerere alinukuu sala ya Mtakatifu Fransisco wa Aziz:

Palipo na chuki nilete mapendo
Palipo na makosa nilete msamaha
Palipo na shaka nilete imani
Pasipo na matumaini nilete tumaini
Palipo na giza nilete mwanga
Palipo na huzuni nilete furaha.

Ni kweli kuwa wazee wa Dar, walifanya tambiko. Lakini Nyerere hakufurahishwa nalo, ndiyo maana mara baada ya tambiko, yeye aliibuka na sala ya Mtakatifu Fransisco wa Aziz.

Icahamike kuwa Nyerere alipoachishwa kazi ya uwalimu kwa sababu ya kujishughulidha na siasa, familia yakeilipelekwa Tosamaganga, Itinga, ambako ilitunzwa na masisita wa shirika la Wakosolata.

Na wimbo wa Taifa, wa MUNGU IBARIKI Tanzania, ulitungwa na padre wa shirika la wakonsolata, Tosamaganga.
 
King David aliungama alichomfanya Uria na kumtwaa mke wake Bersheeba na kumfanya mkewe?
Ndio aliungama ila bado Mungu alimuadhibu na yule mtoto aliyezaa na Bathsheba aliugua na kufa.
Hivi Adam na Eva, waliungama kula lile tunda?
Hawakutubu ndio maana walifukuzwa bustanini.

Yakobo aliungama kuiba urithi wa Essau?
Hakutubu ndio maana hata yeye alidhulumiwa na mjomba wake Labani kwa kupewa mke asiyekuwa chaguo lake baada ya kuchunga mifugo ya mjomba kwa miaka 7, hivyo ikabidi achunge miaka mingine 7 ndio ampate aliyempenda.....na mwishowe aliondoka kwa mjomba wake kwa kukimbia.
hivi Caine aliungama ?
Ndio maana na yeye pia alipewa adhabu.
Yuda alipompachika mimba Tamari aliungama?
Alijutia hilo na yeye ndiye sababu maana hakutimiza ahadi kwa mkwewe ya kumuoza kwa mwanae.

Kuna vitu vinatokea, Mungu hajali sana, anakubariki. Mimi ni baraka!, nina watoto 9 wajukuu 7!
Ungama na utubu Ili wanao, wajukuu na vitukuu wasibebe hizo roho za maagano
 
Habari hii siyo ya kweli. Yamepachikwa maneno mengi ya uwongo kwenye maneno ya ukweli.

Mwenge ulianzishwa na Nyerere kwa kushauriana na wakuu wa Kanisa ili kuomba baraka za Mungu kwa taifa jipya.

Ikumbukwe kuwa waingereza walitaka kuipa uhuru Tanganyika mwezi wa September, lakini Mwalimu Nyerere alikataa, akitaka uhuru wa Tanganyika uendane na tukio la kiimani. Tukio lililokuwa karibu ni sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili.Mwalimu aliridhia Tanganyika ipate uhuru siku hiyo, huku akiomba Mama Bikira Maria awe mwombezi wa Taifa hili:

Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili inaadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 8 Desemba, lakini nchini Tanzania huadhimishwa rasmi kitaifa tarehe 9 Desemba.

Kwa kuzingatia maneno ya Kristo kuwa YEYE ni mwanga wa Ulimwengu, na moto hasa mshumaa hutumika kama alama ya mwanga wa Kristo, mwalimu Nyerere alitaka mwenge utumike kama alama ya mwanga wa Kristo, na katika adhimisho hilo la kuzindua mwenge, Nyerere alinukuu sala ya Mtakatifu Fransisco wa Aziz:

Palipo na chuki nilete mapendo
Palipo na makosa nilete msamaha
Palipo na shaka nilete imani
Pasipo na matumaini nilete tumaini
Palipo na giza nilete mwanga
Palipo na huzuni nilete furaha.

Ni kweli kuwa wazee wa Dar, walifanya tambiko. Lakini Nyerere hakufurahishwa nalo, ndiyo maana mara baada ya tambiko, yeye aliibuka na sala ya Mtakatifu Fransisco wa Aziz.

Icahamike kuwa Nyerere alipoachishwa kazi ya uwalimu kwa sababu ya kujishughulidha na siasa, familia yakeilipelekwa Tosamaganga, Itinga, ambako ilitunzwa na masisita wa shirika la Wakosolata.

Na wimbo wa Taifa, wa MUNGU IBARIKI Tanzania, ulitungwa na padre wa shirika la wakonsolata, Tosamaganga.
Hapo kwenye wimbo wa taifa umetuuza kapasome vizuri.
Wimbo wa taifa asili yake ni south afrika
 
Wengi wetu tumebahatika aidha kushiriki au hata kuchangia mbio za Mwenge wa uhuru wa Tanganyia (Tanzania), lakini ni wangapi kati yetu tunajuwa asili haswa ya huo Mwenge!?

Ipo siri kubwa kuhusu Mwenge wa Uhuru ambao hukimbizwa nchi nzima. Wapo wanaodhani kwamba aliyeleta mabadiliko katika nchi kwa kuanzishwa kwa mwenge huo ni Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere lakini kiukweli haswa Mwalimu Nyerere si mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru.

Mnajimu maarufu ambaye sasa ni marehemu, Sheikh Yahya Hussein aliwahi kusema na ikaandikwa kwamba mvumbuzi wa wazo la kuwa na Mwenge wa Uhuru ni Forojo Ganze ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Forojo Ganze aliyezaliwa mwaka 1902 alifuatana na wazee wengine kwenda kwenye zindiko Bagamoyo ili Mwalimu Julius Nyerere aweze kutawala vema.

Wazee hao na miaka yao ya kuzaliwa kwenye mabano ni Mzee Ramadhan (1920), Ally Tarazo (1929), Komwe wa Komwe (1918) na Sheikh Yahya Hussein (1925).

Wazee hao walipewa kazi hiyo na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote, zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo na baadaye Mwalimu Nyerere alipelekwa Bagamoyo, akachinjwa mbuzi na Nyerere akaambiwa atambuke (aruke damu) baada ya kutokula kutwa nzima (alifunga), jambo ambalo aliwahi kukiri hadharani katika moja ya hotuba zake.

Sheikh Yahya Hussein alinukuliwa akisema hata hivyo, katika mashimo yale Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia katika moja ya shimo kwa ajili ya kuuliza mizimu na aliwaacha wenzake nje wakimngoja ili kujua atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es Salaam.

Utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema, zindiko la Bagamoyo linafanya kazi.

Kilichoshangaza, alisema ni mtu huyo kuingia shimoni na kukaa siku kumi na siku ya kumi na moja alipotoka alikuwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa, na alikuwa akiongea lugha isiyojulikana.

"Tulimchukua akiwa hoi hadi Ikulu Dar es Salaam na tulimfikisha mbele ya Mwalimu Nyerere na akatamka maneno yanayotumika au yanayohusu Mwenge wa Uhuru kwa Kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho," alisema Sheikh Yahya.

Akinukuu maneno hayo Sheikh Yahya alisema Forojo alimwambia Nyerere:

"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau."

Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwalimu Nyerere, Ganze alikata roho na siku chache baadaye Mwalimu Nyerere akayafanyia kazi maneno yake na kuanzisha Mwenge wa Uhuru ambao ulipandishwa Mlima Kilimanjaro na Kapteni Alexander Nyirenda aliyekuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)," alisema Sheikh Yahya.

Hata hivyo, mtaalam huyo wa unajimu alisema kilichowashangaza wengi ni maneno yaliyoongozwa yasemayo "UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU ULETE TUMAINI" akahoji ina maana ndani ya nchi tubaki gizani? Sheikh Yahya Hussein alisema anashangazwa kwa nini Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge wa Uhuru kwani baada ya mazishi ya Forojo, mwenge ulianzishwa ambao ulikimbizwa nchi nzima mara tu baada ya uhuru mwaka 1961 na unaendelea kukimbizwa hadi sasa.

Nyerere alimuagiza Sheikh Yahya Hussein atafsiri maana ya ile namba 115 aliyokuwa ameiandika mkononi Forojo akamwambia:

"Namba 115 maana yake utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na Taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38," na ndivyo ilivyokuwa.
Mwaka 1999 Mwalimu Nyerere alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru na 77+38 =115, namba aliyoiandika Forojo Ganze mkononi.
Nikishika simu yangu nakutana sana na 11:11 ngoja nifuatilie
 
This is utopia. Kwamba mleta post anajua miaka ya kuzaliwa hao Wazee hadi akaiandika lakini hatwambii ni mwaka gani yule Mzee aliingia Shimoni na kutoka. Ahahahahaha!

Ila tunachojua ni kwamba usiku wa kuamkia tarehe 9/12/1961 siku tunapata Uhuru wa Tanganyika, Luteni Nyirenda alikuwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro anaupachika Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanganyika.
 
Habari hii siyo ya kweli. Yamepachikwa maneno mengi ya uwongo kwenye maneno ya ukweli.

Mwenge ulianzishwa na Nyerere kwa kushauriana na wakuu wa Kanisa ili kuomba baraka za Mungu kwa taifa jipya.

Ikumbukwe kuwa waingereza walitaka kuipa uhuru Tanganyika mwezi wa September, lakini Mwalimu Nyerere alikataa, akitaka uhuru wa Tanganyika uendane na tukio la kiimani. Tukio lililokuwa karibu ni sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili.Mwalimu aliridhia Tanganyika ipate uhuru siku hiyo, huku akiomba Mama Bikira Maria awe mwombezi wa Taifa hili:

Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili inaadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 8 Desemba, lakini nchini Tanzania huadhimishwa rasmi kitaifa tarehe 9 Desemba.

Kwa kuzingatia maneno ya Kristo kuwa YEYE ni mwanga wa Ulimwengu, na moto hasa mshumaa hutumika kama alama ya mwanga wa Kristo, mwalimu Nyerere alitaka mwenge utumike kama alama ya mwanga wa Kristo, na katika adhimisho hilo la kuzindua mwenge, Nyerere alinukuu sala ya Mtakatifu Fransisco wa Aziz:

Palipo na chuki nilete mapendo
Palipo na makosa nilete msamaha
Palipo na shaka nilete imani
Pasipo na matumaini nilete tumaini
Palipo na giza nilete mwanga
Palipo na huzuni nilete furaha.

Ni kweli kuwa wazee wa Dar, walifanya tambiko. Lakini Nyerere hakufurahishwa nalo, ndiyo maana mara baada ya tambiko, yeye aliibuka na sala ya Mtakatifu Fransisco wa Aziz.

Icahamike kuwa Nyerere alipoachishwa kazi ya uwalimu kwa sababu ya kujishughulidha na siasa, familia yakeilipelekwa Tosamaganga, Itinga, ambako ilitunzwa na masisita wa shirika la Wakosolata.

Na wimbo wa Taifa, wa MUNGU IBARIKI Tanzania, ulitungwa na padre wa shirika la wakonsolata, Tosamaganga.
Porojo
 
Back
Top Bottom