Asha Migiro in Tanzania

Heshima mbele mkuu,

Hapa tunajadili siasa ya Tanzania na hasa viongozi wetu mimi sina tatizo na hoja nziro dhidi ya viongozi waadilifu ndani ya CCM, kwa sababu ni the only way wananchi watawafahamu vizuri, kwa hiyo kwa wale wanaofikiri kuwa kwa kuwarushia matusi ya nguoni kuwa huenda wanawaharibia, ninawaambia kuwa ni kinyume, ni kwamba wanatupa nafsi za kuwaonyesha uwezo wao, ndio maana hatuchoki hata siku moja,

Mama Kilango, ninamchukulia kidogo almost kama Mrema, unajua Mrema hakuwa na elimu kubwa sana ya siasa, angekuwa nayo by now angekuwa rais wa bongo tayari kwa sababu everything was lined up tayari, lakini ni tamaa zake za fisi ndio zilizomponza mpaka leo ameshindwa kuwa hata waziri mkuu, unajua alishakuwa Deputy Waziri Mkuu, unajua sababu? Ni kwa sababu alikuwa very popular na wananchi, kwa hiyo kiongozi yoyote aliyetaka kukubalika na wananchi ilikuwa ni lazima am-include Mrema kwenye safu yake ya uongozi tena nafasi ya juu, kwa hiyo ni clear next poosition angekuwa angalau waziri mkuu, lakini ni wasi wasi wake na haraka ya madaraka ndiyo ikamfanya aondoke kabla, na mpaka leo hajui jinsi viongozi wengi wa CCM walivyofurahi alipoenda upinzani, maana walijua akiwa huko hawezi kuwaumbua sana kama angekuwa ndani, ingawa pia tunaheshimu sana kitendo chake cha kwenda kule maana kilitusaidia sana taifa kuwaamsha CCM,

Mama Kilango, is doing just fine tena real fine, mkuu wangu waulize wanasiasa wote wa bongo, nini maana ya kiongozi wa level ya ubunge kuweza kuchangisha Sillingi Millioni 10 kwa siku moja, maana kumbuka kuwa siasa ya sasa ni pesa sio maneno mengi tena, sasa kiongozi wa siasa ukifikia level hii ya kuweza kuchangisha hela zote hizi kwa notice ya siku mbili tatu tu, unakuwa umefika mbalia sana as far as influence na kukubalika, sasa kwenye siasa za taifa she is great, na za local ndio hivi majuzi amekuwa akitembelea jimbo lake zima na kufungua misingi 30 ya visima vya maji, ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi zake kwa wananchi wakati wa kampeni za ubunge, pia kuacha zilizotolewa na muungwana, kwenye huo mradi sasa in two months hivi visima vitakuwa vimekwiwsha na wananchi watakunywa maji safi sana, na bado yupo shuleni akiendelea kumalizia Degree yake ya uchumi maana yeye hii ya economics anaijua kwa kuzaliwa nayo, huwezi kuwa na maduka yote aliyonayo bila kuwa mchumi uliyebobea,

Ni kiongozi ambaye hajawahi kuiba wala kuharibu akiwa kwenye uongozi wa siasa, na wala sio fisadi, sasa pole pole ana-make a lot of political gains locally ingawa ukiangalia kwa wasi wasi unaweza kumdharau, maana wanaume waafrika tumezoea hilo against wanawake, lakini ndugu yangu mdharau mwiba si unajua huota nini sasa usije shangaa siku moja wananchi watakapoamua kumpa heshima yake anayostaili, maana kwenye siasa cha muhimu ni kujali small deatils kwanza kabla hujarukia details kubwa, na ndio tatizo kubwa la wanasiasa wetu, kwa wale tunaomfuatilia wka karibu sana tunaridhika sana na hatua alziokwisha piga so far tena yuko far ahead of the game, kuacha hizi kelel za mlango hapa na pale,

Tunasema toa constructive criticism, kwa sababu zinaeza hata kumsaidia mama katika kuongoza wananchi hasa katika hii vacuuum ya political will among viongozi wetu wa juu, sasa mwenye kuonyesha kuwa nayo ni lazima tumsaidie, mapungufu wote kama bina-adam tunayo, lakini kama unajua mapungufu ya kiongozi yoyote kiuongozi ni vema uyasema kama yalivyo, lakini usizushe uongo maana sasa utasaidia kumuongezea umaarufu tu yule kiongozi, sasa toa constructive criticism utamsiadia sana yle kiongozi badala ya matusi ya nguoni na mitaaani, huu uwanja wa JF ni too big na hizo criticism ziszokuwa na macho wala miguu, ninajua kuwa kuna wanaoathirika sana na ushambulizi wake dhidi ya mafisadi, lakini kwenye kumkoma nyani giladi huwa hatuangalii uso wa mtu!

Halafu when the times come, yaani ya uchaguzi tutakuwa na viongozi wengi sana wa kuchagua, wananchi kama Dr. Slaaa, Zitto, Mwakyembe, Sendeka, Mama Kilango, Asha Migiro, Masha, Mwandosya, na wengineo wengi tu, this is good for our country mkuu, kuwa na choices mbali mbali, kwa hiyo si kweli kuwa sioni chongo, hapana nina tabia ya kuheshimu vipaji vya wananchi bila kujali kama ni wanaume au wanawake, wamesoma au hawakusoma, ninawafahamu au siwafahamu, ndio maana pia ninamfagilia sana Mama Migiro, maana huyu naye ni super super!

Hapendwi mtu hapa ila ni matendo na hoja tu!

Ahsante Mkuu
 
Heshima mbele mkuu,

Hapa tunajadili siasa ya Tanzania na hasa viongozi wetu mimi sina tatizo na hoja nziro dhidi ya viongozi waadilifu ndani ya CCM, kwa sababu ni the only way wananchi watawafahamu vizuri, kwa hiyo kwa wale wanaofikiri kuwa kwa kuwarushia matusi ya nguoni kuwa huenda wanawaharibia, ninawaambia kuwa ni kinyume, ni kwamba wanatupa nafsi za kuwaonyesha uwezo wao, ndio maana hatuchoki hata siku moja,

Mama Kilango, ninamchukulia kidogo almost kama Mrema, unajua Mrema kutok hakuwa na elimu kubwa sana ya siasa, angekuwa nayo by now angekuwa rais wa bongo tayari kwa sababu everything was lined up tayari, lakini ni tamaa zake za fisi ndio zilizomponza mpaka leo ameshindwa kuwa hata waziri mkuu, unajua alishakuwa Deputy Waziri Mkuu, unajua sababu? Ni kwa sababu alikuwa very popular na wananchi, kwa hiyo kiongozi yoyote aliyetaka kukubalika na wananchi ilikuwa ni lazima am-include Mrema kwenye safu yake ya uongozi tena nafasi ya juu, kwa hiyo ni clear next poosition angekuwa angalau waziri mkuu, lakini ni wasi wasi wake na haraka ya madaraka ndiyo ikamfanya aondoke kabla, na mpaka leo hajui jinsi viongozi wengi wa CCM walivyofurahi alipoenda upinzani, maana walijua akiwa huko hawezi kuwaumbua sana kama angekuwa ndani, ingawa pia tunaheshimu sana kitendo chake cha kwenda kule maana kilitusaidia sana taifa kuwaamsha CCM,

Mama Kilango, is doing just fine tena real fine, mkuu wangu waulize wanasiasa wote wa bongo, nini maana ya kiongozi wa level ya ubunge kuweza kuchangisha Sillingi Millioni 10 kwa siku moja, maana kumbuka kuwa siasa ya sasa ni pesa sio maneno mengi tena, sasa kiongozi wa siasa ukifikia level hii ya kuweza kuchangisha hela zote hizi kwa notice ya siku mbili tatu tu, unakuwa umefika mbalia sana as far as influence na kukubalika, sasa kwenye siasa za taifa she is great, na za local ndio hivi majuzi amekuwa akitembelea jimbo lake zima na kufungua misingi 30 ya visima vya maji, ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi zake kwa wananchi wakati wa kampeni za ubunge, pia kuacha zilizotolewa na muungwana, kwenye huo mradi sasa in two months hivi visima vitakuwa vimekwiwsha na wananchi watakunywa maji safi sana, na bado yupo shuleni akiendelea kumalizia Degree yake ya uchumi maana yeye hii ya economics anaijua kwa kuzaliwa nayo, huwezi kuwa na maduka yote aliyonayo bila kuwa mchumi uliyebobea,

Ni kiongozi ambaye hajawahi kuiba wala kuharibu akiwa kwenye uongozi wa siasa, na wala sio fisadi, sasa pole pole ana-make a lot of political gains locally ingawa ukiangalia kwa wasi wasi unaweza kumdharau, maana wanaume waafrika tumezoea hilo against wanawake, lakini ndugu yangu mdharau mwiba si unajua huota nini sasa usije shangaa siku moja wananchi watakapoamua kumpa heshima yake anayostaili, maana kwenye siasa cha muhimu ni kujali small deatils kwanza kabla hujarukia details kubwa, na ndio tatizo kubwa la wanasiasa wetu, kwa wale tunaomfuatilia wka karibu sana tunaridhika sana na hatua alziokwisha piga so far tena yuko far ahead of the game, kuacha hizi kelel za mlango hapa na pale,

Tunasema toa constructive criticism, kwa sababu zinaeza hata kumsaidia mama katika kuongoza wananchi hasa katika hii vacuuum ya political will among viongozi wetu wa juu, sasa mwenye kuonyesha kuwa nayo ni lazima tumsaidie, mapungufu wote kama bina-adam tunayo, lakini kama unajua mapungufu ya kiongozi yoyote kiuongozi ni vema uyasema kama yalivyo, lakini usizushe uongo maana sasa utasaidia kumuongezea umaarufu tu yule kiongozi, sasa toa constructive criticism utamsiadia sana yle kiongozi badala ya matusi ya nguoni na mitaaani, huu uwanja wa JF ni too big na hizo criticism ziszokuwa na macho wala miguu, ninajua kuwa kuna wanaoathirika sana na ushambulizi wake dhidi ya mafisadi, lakini kwenye kumkoma nyani giladi huwa hatuangalii uso wa mtu!

Ahsante Mkuu

Na hivi ndio vinamfanya awe Presidential material......ama tuone ni sawa kwa mtu kama yeye na wengineo wengi waliojaa NAKISI za Kiuongozi kutumia ONGWA LA UONGOZI na Janga la Ufisadi nchini kujijenga kisiasa wakati tukijua wazi kuwa nao ni wahusika muhimu katika mchakato wa kupelekea hali hiyo kutokana na nafasi yao katika kulinda na kutetea mfumo fisadi tulionao?...

Siamini kama tumeishiwa kiasi cha kumchukulia kila muongea kwa jazba na kujiamini kuwa ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa kumkomboa mtanzania kutoka kwenye janga kuu ambalo ni mfumo fisadi tulionao. Mfumo ambao unakandamiza hata nafasi na haki ya watanzania kupata upeo mkubwa wa kuweza kuchagua VIONGOZI BORA na kuondokana na changuzi za BORA UONGOZI.....

  • Hivi sio huyu aliyesema wazi kuwa anaongea yeye ili kina Zitto wasiongee.....
  • hivi sio huyu ambaye kila aongeapo anahakikisha "anapledege" uaminifu wake kwa CCM(Ngome kuu na kongwa ya mfumo fisadi)......
  • hivi sio huyu anayeamini kuwa ni CCM tu ndio inapaswa kuendelea kutawala Tanzania na wengine sio wazalendo wa kutosha.....
  • Hivi sio huyu aliyetekwa na wahuni wa ROSTAM na kuporwa zaidi ya milioni 300 alizokuwa akienda kuhonga wana CCM kumchagua mume wake....
  • Hivi sio huyu aliyetumia mamilioni na ubabe wa kila aina kushindana na BABU KEENJA kupata nafasi ya kuwalaghai watanzania wa jimbo la UBUNGO.....
  • Hivi sio huyu aliye.......mengine niyaache....

FMES, najua mahusiano yako ya karibu na Mama Kilango...na pia umuhimu wake kwako kimikakati lakini ni lazima tutambue kuwa kuacha hali mbaya ya na ndoto binafsi za kisiasa kutuingiza katika mitego ya kuamini na kukasimu hatma ya nchi yetu kwa viongozi wa aina hii ni hatari kubwa ambayo tunapaswa kuiepuka.....ni hatari inayozidi hali iliyopo sasa.......

Tanzanianjema
 
1.
Na hivi ndio vinamfanya awe Presidential material......ama tuone ni sawa kwa mtu kama yeye na wengineo wengi waliojaa NAKISI za Kiuongozi kutumia ONGWA LA UONGOZI na Janga la Ufisadi nchini kujijenga kisiasa

Nimesema hivi, ubunge wake sasa hivi unampa nafasi kubwa sana kuwa presidential material, kwa sababu nimekuomba mara nyingi sana wewe na wenzio wawili kuwa mniwekee majina yana-fit hiyo presidential material yenu mpaka sasa mmeshindwa, nimeawaambinei hivi marais wote tuliowahi kuwa nao baada ya Mwalimu, kwanza walianza na ubunge wa kuchaguliwa kazi ambayo sasa hivi Mama Kilango anaifanya,

Hoja yako ya kutafuta umaarufu na janga la ufisadi, haina hata nguvu licha ya mvuto kwa sababu huonekani kuelewa vizuri siasa na time zake, sasa hivi USA umaarufu unapatikana kutokana na msimamo wa mgombea on vita vya Iraq, Jaluo anaheshimika zaidi kuliko Mama Clinton, among the lefties kwa sababu hakupiga kura akiwa Senate, ku-authorize US kuivamia Iraq, ndio maana amemshinda Mama Clinton, it does not matter kama Jaluo hana experience, lakini aliweza kuliona hili na ku-capitalize on it, ndio siasa za kisasa mkuu,

Tanzania sasa hivi tatizo letu kubwa kisiasa na kiuongozi ni ufisadi, kwa hiyo kwa anayetaka umaarufu wa kisiasa sasa hivi ni kuka-pitalize on it, zitto na Dr. Slaa sio maarufu kwa sababu wamelima mashamba makubwa kuliko wananchi wote wa Tanzania, ila ni kwa sababu wamelivalia njuga sana suala ufisadi na mikataba mibovu, mkuu hata siasa ndogo ndogo namna ni lazima tuje tuelimishane hapa JF?

2.
wakati tukijua wazi kuwa nao ni wahusika muhimu katika mchakato wa kupelekea hali hiyo kutokana na nafasi yao katika kulinda na kutetea mfumo fisadi tulionao?...

Sawa sawa, sasa uweke ushaidi wa jinsi Mama Kilango alivyohusika na hayo unayoyasema ya ufisadi, mkuu wewe una elimu kubwa sana kuliko wengine wengi humu, sasa unaposhindwa kujenga hoja nzito na kujaribu kulazimisha ishu isiyokuwepo inasikitisha, kuwa mwanachama wa CCM au mbunge wa CCM haina maana kulinda mfumo wa the nonesense, mimi ni mwanachama wa CCM tena hai, lakini I have nothing to na hayo ya ufisadi, lakini ninajua kuwa ndani ya chama changu kuna baadhi ya viongozi ambao ni mafisadi,

Otherwise, wa-Tanzania wote tunahusika na kuilinda hiyo system ya ufisadi kama unavyosema kwa sababu wote tunahusika kwa njia moja au nyingine kuwaruhusu CCM kututawala kwa miaka 45 iliyopita, hivi wewe huko nyuma kabla ya kupewa huu uhuru wa kuandika hapa JF, uliwahi kufanya nini cha maana kwa taifa kuonyesha kuwa hukubaliani na system iliyokuwepo huko nyuma na hii ya sasa? Hapa unajaribu kukimbia kivuli chako mwenyewe na hoja njiwa mkuu, kama point yako ninaielewa ni kwamba unamlazimisha Mama kilango, kwenye ufisadi kwa sababu alipokuwa mbunge wa kuteuliwa na rais Mkapa, hakuwa na kelele kama alizonazo sasa, kwa hiyo wale wote tuliokuwa kimyaa enzi za zamani tunahusika na kuifagilia system ya ufisadi, wewe ukiwemo is that so?
 
3.
Siamini kama tumeishiwa kiasi cha kumchukulia kila muongea kwa jazba na kujiamini kuwa ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa kumkomboa mtanzania kutoka kwenye janga kuu ambalo ni mfumo fisadi tulionao. Mfumo ambao unakandamiza hata nafasi na haki ya watanzania kupata upeo mkubwa wa kuweza kuchagua VIONGOZI BORA na kuondokana na changuzi za BORA UONGOZI.....

Huamini what? Tizama hivi unataka itokee nini tena Tanzania ili uamini kuwa unachoona ndio tulichonacho hakuna muujiza utakuja toka Mbinguni bro, yaani tumetawaliwa na viongozi magoi goi wasiokuwa hata na muelekeo halafu unasema eti huamini kuwa tumeishiwa? Huo mfumo mbovu ndio huo Mama Kilango, anaupigia kelee at least, wewe mkuu umefanya nini na kutoamini kwako?

Sasa hapa mkuu unataka nimuheshimu nani wewe unayemtukana Mama anayepigia kelele na kuwakosesha usingizi mafisadi, au Mama mwenyewe? Mtikila tulikuwa tunamheshimu kwa sababu aliweza kuongea kwa jazba against ufisadi, mpaka juzi tulipodungua kuwa na yeye ni fisadi, it ikaisha hapo hapo, sasa labda useme ufisadi wa Mama Kilango, kama huwezi ninakuona kufanana sana na Mama Anna Abdallah, maana maneno yenu yanafanana sana, tofauti tu ni kwamba mimi ninjaribu kukuelimisha zaidi lakini Mama Anna Abdallah ametukanwa na wananchi mpaka kesho yake akaomba kujitoa kwenye uchaguzi wa UWT, again huna hoja hapa kwa sababu unadai huamini wakati unajua kuwa tulichonacho ndio hicho hicho hakuna malaika watakaotoka mbinguni kuja kutuongoza wa-Tanzania!

Halafu haya ya kwako ni maneno ya kizamani sana, siku hizi mkuu umeona serikalini kulivyojaa vijana wadogo?
 
Simwamini mtu yoyote atakayepita katika mchujo wa kundi la watu wachache wanaokihodhi chama cha mapinduzi kwa kuwatumia watanzania wengi wanaodanganywa wakati wa uchaguzi. Yeyote anayepita katika mchujo huo ni mwenzao na dont expect any difference.
 
1.
Hivi sio huyu aliyesema wazi kuwa anaongea yeye ili kina Zitto wasiongee.....

Okay, haya ni maneno ya siasa, ambayo kiongozi yoyote anaweza kuyasema, hayahusiani na anything to do na presidential material, kama antaka chama chake kichukue agenda ya kina Zitto kuwa ubaya gani kisiasa? Mbona Bill Clinton aliiba agenda ya Republicans on Welfare na akaigeuza kuwa yake na Democrat, na akaweza kuitumia kushinda urais term ya pili? Mkuu hivi kweli unaelewa vizuri siasa na vyama au? Naona unahitaji elimu nzito sana hapa!

4.
hivi sio huyu ambaye kila aongeapo anahakikisha "anapledege" uaminifu wake kwa CCM(Ngome kuu na kongwa ya mfumo fisadi)......
hivi sio huyu anayeamini kuwa ni CCM tu ndio inapaswa kuendelea kutawala Tanzania na wengine sio wazalendo wa kutosha.....

Off course hata mimi kama Mwanachama wa CCM hai, ninakubaliana na haya, viongozi wachache wahuni ndani ya CCM hawaifanyi CCM yote kama chama cha siasa kuwa kibovu na wananchi wengi wa Tanzania wanajua hilo, ndio maana wakati wa uchaguzi huamua kutoa kura kwa CCM, na what this has to do na hiyo presidential material yenu? Kwani Kikwete alikuwa na msimamo gani wakati anachaguliwa kuhusu CCM?

5.
Hivi sio huyu aliyetekwa na wahuni wa ROSTAM na kuporwa zaidi ya milioni 300alizokuwa akienda kuhonga wanansa CCM kumchagua mume wake....

Again hii haina anything to do na hiyo presidential material yenu, naomba nikusahihishe kama ifuatavyo kwa sababu hapa umeleta maneno ya vijiweni na mtaani ambayo kwanza ni aibu kwa mtu mzima kama wewe tena mwenye elimu kubwa sana kama yako kuyasema tena mbele ya uwanja mkubwa kama huu,

(a). Mama Kilango, hakuporwa na watu wa Rostam, huo ni uongo tena ni ujinga, walompora wote wako jela, wangekuwa wametumwa na Rostam, wasingefungwa jela, tizama jambazi Nyari yuko wapi sasa hivi ni kwa sababu ya kushirkiana na kina Rostam na Lowassa, binafsi nimewahi kushuhudia mjumbe wa Nyari alipokuwa jela, akimuomba kiongozi mmoja mzito kumsaidia huku yule mjumbe akiwataja hawa kina Rostam kuwa yuko nao, mkuu acha majungu tena ya kijinga kama haya!

(b). Mama Kilango, aliporwa shillingi laki tatu tu, na haukuwa wakati wa uchaguzi, pia alikuwa akitokea USA kuchukua bidhaa za maduka yake, between Dar, Dodoma, na Kihurio, gari alilokuwemo lilikuwa limekwenda Dar kutoka Dodoma likiendeshwa na Dreva wa mumewe, ambaye alikuwa bungeni kwani kulikuwa na kikao cha bunge kikiendelea, na mama alikuwa anajaribu kuwahi bungeni kwani aliambiwa kuwa saaa aliyoodoka Dar haikuwa nzuri ansubiri mpaka kukuche zaidi, lakini akagoma akitaka kuwahi bungeni, ndipo yakamkuta hayo ya ujambazi, ambayo kesho yake pia yalimkuta Makongoro Nyerere, je naye alikuwa amebeba hela za kuhinga uchaguzi? Au nao walikuwa majambazi wa Rostam?

Halafu naomba unitajie ni Wapare wangapi unaowajua duniani wanaoweza kusafiri na hela zote hizo shillingi millioni 30 kwenye gari? Hivi huwa hamuoni aibu mnapozusha ujinga wa namna hii? Unajua, hizi chuki na hasira bin-adam mnazitoa wapi against bin-adam mwingine bila hata ya kuwajua vizuri? Bin-adam unakuwaje na chuki na bin-adam mwingine hata unafikia kufurahia kuporwa kwake na majambazi?

Again kwa hiyo unasema haya ndio yanamfanya kiongozi awe au asiwe presidential material? Yaani ukiporwa tu na majambazi ya Rostam, basi wewe huwezi tena kuwa presidential material wa Tanzania?
 
Mama Kilango, is doing just fine tena real fine, mkuu wangu waulize wanasiasa wote wa bongo, nini maana ya kiongozi wa level ya ubunge kuweza kuchangisha Sillingi Millioni 10 kwa siku moja, maana kumbuka kuwa siasa ya sasa ni pesa sio maneno mengi tena, sasa kiongozi wa siasa ukifikia level hii ya kuweza kuchangisha hela zote hizi kwa notice ya siku mbili tatu tu, unakuwa umefika mbalia sana as far as influence na kukubalika, sasa kwenye siasa za taifa she is great

So this is what makes a great politician now? The ability to fundraise?

Then we need some more Tanzanians of Asian descent in the parlieament, wouldn't you agree that they are good at this thing? Some more Rostams and their likes, no?
 
Simwamini mtu yoyote atakayepita katika mchujo wa kundi la watu wachache wanaokihodhi chama cha mapinduzi kwa kuwatumia watanzania wengi wanaodanganywa wakati wa uchaguzi. Yeyote anayepita katika mchujo huo ni mwenzao na dont expect any difference.

Kutokuamini kwako hakubadili wala kuongeza anything kwenye uchaguzi, labda ukienda kupiga kura unaweza, lakini kutokuamini tu inaweza kubadili nini?
Sasa hivi huiamini CCM, je kuna kilichobadilika? So what?
 
So this is what makes a great politician now? The ability to fundraise?
Then we need some more Tanzanians of Asian descent in the parlieament, wouldn't you agree that they are good at this thing? Some more Rostams and their likes, no?

Hivi kweli jamani hata haya mambo madogo namna inabidi tuje tufundishane humu JF? Wewe mkuu unafikiri kwa nini Democrats hawamtaki Clinton na mkewe tena, lakini wanamtaka Jaluo?

Hivi unajua kuwa kila Asian aliyegombea ubunge last uchaguzi alishinda, lakini kamati kuu ya CCM ikaamua kuwaondoa wengine kwa makusudi na kuwachomeka kina Rita Mlaki?

Wewe utakuwa kiongozi gani wa kisasa ambaye huna mvuto wa kuwashawishi wananchi wenye uwezo na wasioukuwa nao kukuchangia hela nyingi za kampeni na maendeleo ya wananchi? Hivi mkuu unajua Jaluo anatoa wapi hela zake za kmapeni kule US? Anachangiwa na wananchi wenye uwezo mkubwa na mdogo, tena kutoka kila kona ya dunia!
 
Hivi sio huyu aliyetumia mamilioni na ubabe wa kila aina kushindana na BABU KEENJA kupata nafasi ya kuwalaghai watanzania wa jimbo la UBUNGO.....
Hivi sio huyu aliye.......mengine niyaache....

Alitumia ubabe dhidi ya Keenja, aliyekuwa akisaidiwa na the Sitting Waziri Mkuu Sumaye, RC Makamba, Mayor Sykes, Mwenyekiti Londa na Mkali, unasema huyu mama ambaye by then hata hakuwa mke wa Malecela, angeweza kuleta ubabe mbele ya hii team? Hivi hawa kwenye hii team unawajua vizuri au unawasikia? Yaani mkuu ni aibu sana una maneno mengi ya mtaaani matupu, ambayo hayana uhusiano wowote na u-presidential material, unless haya maneno ndio hasa material yako ya kiongozi kuwa presidential material, mimi nilifikiri kuwa una hoja nzito kwa sababu najua kuwa umesoma sana, lakini nashangaa sana na hizi hoja njiwa kama sio kunguru, mkuu tafuta hoja nzito against mama Kilango, chuki tu na maneno ya mtaani kama haya huwezi kumzibia riziki mkuu!

Taifa limebadilika, sasa kina mama tunawapa nafasi pia ya kuonyesha ujasiri wao kiuongozi na kisiasa, zile ezni za wao kipika jikoni zimeisha mkuu, amka sasa!

FMES, najua mahusiano yako ya karibu na Mama Kilango...na pia umuhimu wake kwako kimikakati

Hapana mkuu, hujui lolote ila una maneno ya chuki ya mtaani na vijiweni, lakini huna hoja, Mama Kilango ni rafiki yangu kama walivyo wengine wengi sana walioko kwenye uongozi na wanachi wa kawaida, hayo ya mkakati labda ya kwako mimi sina mkakati wowote na anybody, ila ninajihusisha sana na siasa za taifa, ndio maana nilitegema labda nitachota hoja nzito hapa, ili angalau nim-forwardie aweze kujifunza something, lakini hakuna kitu ila majungu tu kama kawaida yetu wabongo chuki tu na uzandiki, ukweli huwa hatuna hata siku moja manenom mengi ya mtaani ya wananchi waliokata tamaa, halafu mut kama wewe unaenda na kuyabeba tu bila hata kufikiri hata kidogo, no mkuu huji anything kuhusu mahusiano yangu na Mama kilango, yeye ni rafiki yangu kama wengine wote na wengi!

lakini ni lazima tutambue kuwa kuacha hali mbaya ya na ndoto binafsi za kisiasa kutuingiza katika mitego ya kuamini na kukasimu hatma ya nchi yetu kwa viongozi wa aina hii ni hatari kubwa ambayo tunapaswa kuiepuka.....ni hatari inayozidi hali iliyopo sasa.......

Tanzanianjema

Mimi nafikiri tunatakiwa kuwaogopa wananchi waongo kama wewe, maana maneno mengi lakini uongo mtupu, sasa ni wananchi kama ndio hatari sana kwa taifa, sio viongozi waadilifu kama Mama Kilango, maana maneno yako yote against Mama ni ndoto tupu ambazo hazipo wala hazijawahi kutokea,

Pole sana mkuu, Mama Kilango, is doing just fine ndio kwanza amerudi toka jimboni ambako aliweka misingi 30 ya visima vya maji safi kwa wananchi ambavyo aliwaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi bunge zilizopita, huo ndio tunaita ni uongozi unaotakiwa, maana ahadi ni deni!

Ila mkuu umenisikitisha sana maana nilitegemea utatoa elimu ambayo inaweza kumsaidia Mama Kilango, na uongozi wake lakini ni yale yale ya mtaani, sasa nina-assume siku moja na wewe utakuwa kiongozi wetu, hivi kweli wananchi tutegemee nini zaidi ya hizi porojo za mitaaani? Aibu kweli!

Ahsante Mkuu.
 
Huyu mama si chochote.
Hafaiiiiiiiiiiiiiiii.

Sawa sawa ni wewe unayefaaa pole sana yaliyokukuta hivi karibuni nimeyasikia sana vipi umesha-recover tayari! Again pole sana ndio dunia hiyo mkuu, labda next time utajifunza!

Yaani misimamo ya makombo, tulipokuwa tunapewa makombo na mama Kilango, alikuwa anafaa sasa tumekatiwa makombo hafai wallahi the makombo motivation theory, ndio maana tumemwabia asiruhusu watu wa namna hii tena karibu yake, yaani matapeli!
 
FMES,

..hivi jimboni kwa Mzee Malecela kuna hali gani ya maendeleo?

..nakumbuka Mzee Cygwiyemwisi Malecela alipigwa vita kwamba anashindana na kina Nsekela kupeleka maendeleo Mbeya. matokeo yake akashindwa uchaguzi.

..Mtera wamechimba visima vingapi, wamejenga shule ngapi za kati, na kusambaza makontena mangapi ya vitabu?
 
1. Malecela, aliwahi kuwa DC wa kwanza wa wilaya ya Tukuyu baada ya uhuru, kwa hiyo ana mizizi mizito sana kule kama aliyonayo Mwanza, ambako pia aliwahi kuwa RC in the 60s, na Iringa pia, ambako huku kote ana nyumba na mashamba yake binafsi, kwa hiyo ndio maana alikuwa akienda sana sehemu hizi na hasa Tukuyu, ambako pia na mke wake ambaye ni marehemu sasa, alitokea kule hayo maneno ya Nsekela ni nonesense zilizoanzishwa na maadui zake ili kuhallaisha uovu wao waliomfanyia kwenye huo uchaguzi, na

2. Waliohusika na uovu huo ni Waziri mkuu Kawawa, aliyekuwa akishi Dodoma, ambaye alikasirishwa sana na sherehe za kumuaga ndugu wa Malecela Balozi Lusinde, alipokuwa akelekea China kuwa balozi wetu mpya kule, yeye Kawawa alipohamia pale Dodoma kama Waziri Mkuu mpya hakupewa mapokezi makubwa kama ile sherehe, aliapa kuwa atawamaliza wote wawili, akam-recruit Mama Anna Abdallah aliyekuwa RC, na hawara yake, halafu akam-recruit Mzee Ndejembi, aliyekuwa DC Moshi na uwt pia, kwa kushirikina na hawa na pia na mkono mmoja mzito zaidi toka Dar, aliweza kuugeuza uchaguzi wa jimbo Dodoma Vijijini na kumfanya Mazengo, a former construction worker kumshinda Malecela,

3. Ushahidi wote wa uhuni uliofanyika ulipatikana baada ya kutafutwa sana na manager wa kampeni wa uchaguzi ule wa Malecela, ambaye sasa ni rais wa Rotary Club Bwana misano, lakini alipompelekea Malecela, ili aende mahakamani Malecela alikataa kata kata na kusema kuwa kuna kazi nyingi sana anaweza kuzifanya duniani sio lazima iwe ubunge na uwaziri tu, Huu ndio ukweli wa hiyo hadithi uliyonayo ambayo ni clear kuwa masikini ya Mungu huna ukweli, na wewe umepewa maneno ya mitaaani na ukayakubali bila kuuliza.

4. Kuhusu jimbo la Malecela, labda uwaulize wabunge wengine maana tunao hapa watakwambia kuwa ni jimbo lake tu katika Tanzania, ndio lina shule na zahanati katika kila kata, na zimejengwa katika kipindi cha ubunge wake, yaaani yeye ubunge huko ni mpaka atakaposema basi yeye mwenyewe, amepeleka makontena mawili ya vitabu so far toka UK, maisha bado ni magumu so far, lakini angalau kuna unafuu kwenye shule an zahanati, bara bara na hata maji, sasa hivi unaweza kwenda Mvumi kwa saa moja tu na nusu kwa sababu ya uzuri wa bara bara,

Mara ya mwisho nilikuwa kijijini Chamwino, hivi karibuni kupima maji ya kugombea ubunge, kwa kweli sikuamini jinsi maisha yalivyo chini yaani kwa dola $ 50 tu nilifunga vilabu vyote vya pombe za kienyeji pale na kuwpaa wananchi bure kwa siku nzima, si unajua kwenye kujijenga, lakini the point hapa ni kwamba kwa maisha ya kule kuwa na shule na zahanati kwenye kila kata ni hatua kubwa sana kwa wananchi wanaoishi huko.

Niaamini kuwa nimekujbu maswali yako mkuu, ingawa sielewi ianhusiana vipi na kinachoendelea hapa!

Ahsante Mkuu!
 
huyu mzee wako malecela tatizo hajtulia! alipokuwa waziri mkuu alituaibisha sana pale uingereza alipokuja kuongea na watz, jioni kwenye ile part akaanza kupapasa kila demu akidhani ni...

isitoshe hotuba zake ni copy and paste za mwalimu nyerere na zinapopitwa na muda hajui hilo. aliwahi kuhutubia chuo kikuu huko namibia after 1990, wakati nchi zote za afrika zimeshapata uhuru, akaanza kurudia speech ya kwame nkrumah ya 1960, kuwa tanzania haiwezi kuwa huru hadi nchi zote za afrika ziwe huru! aliboa sana wasikilizaji wenzake

la mwish ni kuwa ameshachoka mwili na akili, ni vema wagogo kule jimboni mwake wakafahamu hilo

andaeni vijana mapema
 
1. huyu mzee wako malecela tatizo hajtulia!

Labda kama ni mzee wa kwako wewe, nafikiri sheria za JF unazijua juu ya ku-speculate ID za member wengine usiowajua, kwa hiyo naomba hapa ukome kabisa kama huna hoja kaa pembeni. Sikujui lakini nikitaka ninaweza kukujua in in some few hours, nilijua tu kuwa yatakushinda halafu utaleta viroja kama kawaida, here you are!.

alipokuwa waziri mkuu alituaibisha sana pale uingereza alipokuja kuongea na watz, jioni kwenye ile part akaanza kupapasa kila demu akidhani ni...
isitoshe hotuba zake ni copy and paste za mwalimu nyerere na zinapopitwa na muda hajui hilo. aliwahi kuhutubia chuo kikuu huko namibia after 1990, wakati nchi zote za afrika zimeshapata uhuru, akaanza kurudia speech ya kwame nkrumah ya 1960, kuwa tanzania haiwezi kuwa huru hadi nchi zote za afrika ziwe huru! aliboa sana wasikilizaji wenzake

Hapa sielewi your point labda urudie tena maana I have nothing to do na this, wala sijui unachosema hapa!

la mwish ni kuwa ameshachoka mwili na akili, ni vema wagogo kule jimboni mwake wakafahamu hilo

andaeni vijana mapema

Haya yako ni matusi ya bila sababu, sisi waa-Afrika huwa tunaheshimu wazee tena sana, kuzeeeka kwa mtu hakumfanyi kuwa amechoka unless wewe ni mkewe, au?

by the way, Mama Kilango na Mama Anna Makinda, wataondoka hivi karibuni in the next to weeks kuelekea DC Washington kwa ajili ya kuhudhuria semina ya mafunzo kuhusu utawala bora, ambayo itachukua muda wa mwezi mmoja.
 
...wazee mama anna kilango binafsi nimemfuatilia tangu akiwa UWT mkoa wa dar es salaam ...mama yupo smart....na zaidi namchukulia kati ya wanawake wachache wanaoweza kupambana na wanaume ..zaidi she is strategist...pia nafasi aliyonayo ameipata kwa uwezo binafsi wala si kwa sababu ya malecela.......

..wakati wa kampeni za uchaguzi ubungo mwaka 2000 ni wazi alimshinda keenja ..tunajua..lakini mkapa alikusudia keenja ashinde ili ampe uwaziri kama zawadi kutokana na keenja kufanikiwa kazi aliyomtuma la kuunda mfumo mpya wa jiji....akiamini akimpa uwaziri angefanya makubwa zaidi...zilikuwa ni juhudi binafsi za mkapa za anna kilango kuombwa amuachie keenja kwa ahadi ya ubunge wa kuteuliwa..

katika kuonesha hapendi mteremko huyu mama miaka 5 tu ya kuteuliwa ilimtosha ..akaamua kupandisha jimboni kupambana na akamngoa YONA.......hapo mfahamu kuwa huyu hata angeamua kuwa mbunge wa kuteuliwa kwa miaka 20 ijayo kama zakia au anna abdalh...hakuna ambaye angemzuia..kwani hata dada asha rose naye hakuwa mbunge wa jimbo......so kimsingi sipingani na uwezo wake binafsi..namuunga mkono kisiasa..

...LAKINI NAHISI ....KUWEZA HATA KUDHANI AU KUFIKIRIA KUWA ANNA KILANGO ANAWEZA KUWA AU HATA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA NAHISI WE HAVE GONE TOOO FAR.......SIMPLY ZAIDI YA UBUNGE NA UWAZIRI WA KAWAIDA ....UWAZIRI MKUU AU URAIS HAUWEZI ........

ILA NAMSHAURI AGOMBEE UWENYEKITI WA UWT TAIFA.......KITENDO CHA KUMUACHIA HUYU SOPHIA SIMBA UWENYEKITI WA UWT.............NI AS IF MUUNGWANA NDIO MWENYEKITI WA UWT.....TUTAKUWA TUNAENDELEZA SERIKALI NA CHAMA CHA KISHKAJI.......KWA KUWA UWEZO WA MWENYEKITI KUDHIBITI NCHI NA CHAMA UNATIA SHAKA...TUSIMRUHUSU ATEKE HIZI JUMUIA ....UDHAIFU UTAONGEZEKA.....!!
 
....anna kilango achukue jumuia ya wanawake.....imelala sana ..kama ya wazazi....hasa baada ya jk nayo kutaka kuiteka.........nafikiri mkono anaitaka sasa...
 
1. Malecela, aliwahi kuwa DC wa kwanza wa wilaya ya Tukuyu baada ya uhuru, kwa hiyo ana mizizi mizito sana kule kama aliyonayo Mwanza, ambako pia aliwahi kuwa RC in the 60s, na Iringa pia, ambako huku kote ana nyumba na mashamba yake binafsi, kwa hiyo ndio maana alikuwa akienda sana sehemu hizi na hasa Tukuyu, ambako pia na mke wake ambaye ni marehemu sasa, alitokea kule hayo maneno ya Nsekela ni nonesense zilizoanzishwa na maadui zake ili kuhallaisha uovu wao waliomfanyia kwenye huo uchaguzi, na

2. Waliohusika na uovu huo ni Waziri mkuu Kawawa, aliyekuwa akishi Dodoma, ambaye alikasirishwa sana na sherehe za kumuaga ndugu wa Malecela Balozi Lusinde, alipokuwa akelekea China kuwa balozi wetu mpya kule, yeye Kawawa alipohamia pale Dodoma kama Waziri Mkuu mpya hakupewa mapokezi makubwa kama ile sherehe, aliapa kuwa atawamaliza wote wawili, akam-recruit Mama Anna Abdallah aliyekuwa RC, na hawara yake, halafu akam-recruit Mzee Ndejembi, aliyekuwa DC Moshi na uwt pia, kwa kushirikina na hawa na pia na mkono mmoja mzito zaidi toka Dar, aliweza kuugeuza uchaguzi wa jimbo Dodoma Vijijini na kumfanya Mazengo, a former construction worker kumshinda Malecela,

3. Ushahidi wote wa uhuni uliofanyika ulipatikana baada ya kutafutwa sana na manager wa kampeni wa uchaguzi ule wa Malecela, ambaye sasa ni rais wa Rotary Club Bwana misano, lakini alipompelekea Malecela, ili aende mahakamani Malecela alikataa kata kata na kusema kuwa kuna kazi nyingi sana anaweza kuzifanya duniani sio lazima iwe ubunge na uwaziri tu, Huu ndio ukweli wa hiyo hadithi uliyonayo ambayo ni clear kuwa masikini ya Mungu huna ukweli, na wewe umepewa maneno ya mitaaani na ukayakubali bila kuuliza.

4. Kuhusu jimbo la Malecela, labda uwaulize wabunge wengine maana tunao hapa watakwambia kuwa ni jimbo lake tu katika Tanzania, ndio lina shule na zahanati katika kila kata, na zimejengwa katika kipindi cha ubunge wake, yaaani yeye ubunge huko ni mpaka atakaposema basi yeye mwenyewe, amepeleka makontena mawili ya vitabu so far toka UK, maisha bado ni magumu so far, lakini angalau kuna unafuu kwenye shule an zahanati, bara bara na hata maji, sasa hivi unaweza kwenda Mvumi kwa saa moja tu na nusu kwa sababu ya uzuri wa bara bara,

Mara ya mwisho nilikuwa kijijini Chamwino, hivi karibuni kupima maji ya kugombea ubunge, kwa kweli sikuamini jinsi maisha yalivyo chini yaani kwa dola $ 50 tu nilifunga vilabu vyote vya pombe za kienyeji pale na kuwpaa wananchi bure kwa siku nzima, si unajua kwenye kujijenga, lakini the point hapa ni kwamba kwa maisha ya kule kuwa na shule na zahanati kwenye kila kata ni hatua kubwa sana kwa wananchi wanaoishi huko.

Niaamini kuwa nimekujbu maswali yako mkuu, ingawa sielewi ianhusiana vipi na kinachoendelea hapa!

Ahsante Mkuu!

Kaka asante sana kwa habari unazotupa humu lakini ningependa kuweka masuala kadhaa wazi...

Hili la nyumba na mashamba kadhaa ezni zile ambazo viongozi hawakutakiwa kuwa na mali nyingi na nyumba zaidi ya moja haukuwa ufisadi kwa mantiki ya enzi zile?

Na hili la kumuita Mama ANNA ABDALA kuwa alikuwa hawara wa Kawawa ndio umakini-ustaarabu na sio matusi ya nguoni. Sasa iweje wewe uwe wa mwanzo kulalama kuwa wengine wahuni na wanatoa matusi ya nguoni pale wanapowasema watu nasaba zako?

Na hili la kusema kuwa MVUMI ni jimbo lake Mzee Malecela na kutoa mfano wa kupeleka vitabu makontena mawili ni mafanikio ni sawa kweli. Hivi vitabu ni jitihada za Mzee Malecela ama yule Mzee wetu pale New York?

Naamini MVUMI ni jimbo la wana mvumi wote akiwemo yule msema maneno mengi (LUSINDE) aliyekuwa UDP akaenda CHADEMA na baadaye kuingia CCM kwa makubaliano ya kurithishana na Mzee Malecela na about 5 milion za hongo....i mean takrima ya kukubali kujitoa......

Na hili la kwenda MVUMI kupima maji ya kugombea ubunge mhhh...nilidhani hii mambo ya kurithishana ni dhambi kwa wote kumbe ni kwa kina KIKWETE tu.

Vilevile ina maana Mzee MAlecela alimhadaa lusinde mdogo kumuachia apite kiulani si kwa nia ya kumuachia 2010 kwani tayari anamwandalia MTOTO wake nafasi hiyo?

Kaka, mimi na wewe nothing personal kama wasemavyo "wanyamwezi" ila ni muhimu kuwekana sawa......

Tanzanianjema
 
Back
Top Bottom