1. Jamani UN tunalikizo nyingi sana kutegemea na aina ya kazi yako. Kwa mfano mimi binafsi napata likizo kila baada ya wiki 6 na kwa maana hiyo nikiamua kuja nyumbani nitakuja si chini ya mara 7 kwa mwaka. Sasa huenda mama yeye kutokana na majukumu yake mazito akawa na likizo nyingi zaidi. Un inaamini mapumziko mzfupi ya kila baada ya muda fulani ili mtu aweze kuwa more effective kwa kupunguza msongo wa maisha na zaidi likizo za UN huruhusiwi kuchukua likizo na kukaa kwenye nchi unayofanyia kazi.
2. Chondechonde naona watu huko nyumbani mnaendekeza sana suala la UDINI, why? Tuulizeni sisi tunaofanyakazi hizi na UN na kupata bahati ya kuzunguka Dunia hii. Dini na Ukabila ni vya kuviogopa kabisa kama UKOMA, mataifa mengi yameingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya Dini na Ukabila. Naomba ndugu zangu tujaribu kuepuka hili. Sidhani kama kuna tatizo lolote kama viongozi watatoka kabila moja au dini moja kama watukuwa na sifa hizo. Nyerere alisemz "tuchague au tusichague mtu kwa ajili ya kabila au dini yake".