MAMBO 7 MUHIMU MECHI YA SIMBA 2 Vs 0 GOR MAHIA
Na John Pambalu.
1. Simba imekuwa na kiwango bora zaidi kuliko Gor Mahia. Kwa mahitaji ya Simba ya kujiandaa kwa mechi za kimataifa na ile ya mtani wa jadi sidhani kama walifanya uchaguzi sahihi wa timu bora ya kukutana nayo.
2. Timu zote zimecheza mpira katikati ya uwanja. Licha ya Simba kuwa na kiwango kizuri lakini hauuoni mfumo wanaotumia kupanga mashambulizi. Gor Mahia wao staili yao ilikuwa inaonekana kupiga mipira mirefu kwa mawinga Long ball attack na switch off zilionekana licha ya kushindwa kumalizia kwa umakini.
3. Huyu Naby Kamara ni complete package. Usajiri huu utaipa Simba matokeo maana kwa dakika chache ameonyesha ana kitu cha ku offer kwenye club.
4. Jese Mukwala ameonyesha namna ambavyo mshambuliaji wa kimataifa anapaswa kuwa. Mshambuliaji mzuri hasubiri nafasi zaidi ili ajitambulishe.
5. Kipindi cha Pili Simba imekuwa na uhai kuliko kipindi cha kwanza. Kutambulishwa mchezoni kwa Yusuph Kagoma kumeimarisha sana nafasi ya kiungo ya Simba.
6. Baada ya Gor Mahia kufungwa gori la pili walipunguza kujilinda wakaanza kushambulia. Wametengeneza mashambulizi mengi kipindi cha Pili bila umakini, wameshindwa kujua wafanye nini kwenye robo ya tatu ya uwanja.
7. Tundu Lissu anaonekana kuwa ni kiungo wa ajabu kuwahi kutokea katika siasa za Tanzania. Walimshindwa kwenye jukwaa la siasa wakamtupa gerezani sasa anaitumia mahakama kuionyesha dunia kuwa yeye ni asset ya taifa hili. Amekuwa akiwatoka mawakili wa Jamuhuri kwa kasi sana akionyesha namna mfumo wa haki wa Tanzania ulivyo na makosa makubwa huku akiendelea kusisitiza kuwa No Reforms No Election ni Real.
Wasalaam
John Pambalu
Mchambuzi wa Mchongo.