Asante sana Mungu kwa kutuvusha nusu mwaka

Asante sana Mungu kwa kutuvusha nusu mwaka

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Ee Mungu nakushukuru umetuvusha nusu mwaka salama.

1. Maadui walikuja ili watuangamize, ukawatawanya! Asante sana Mungu.
2. Magonjwa yalitupata, ukatuponya nayo yote. Nakushukuru Mungu wetu.
3. Umebariki kazi za mikono yetu, tumepata pesa ya kununua mahitaji muhimu. Asante Mungu mkuu.
4. Tumesafiri huku na kule, na kukutana na ajali, hukutuacha tuangamie. Asante Mungu mwenye nguvu.
5. Ibilisi alituletea vishawishi na majaribu ya uzinzi, umetusaidia kumpinga na kumshinda. Asante Muumba mbingu na nchi.
6. Tumepita katikati ya mambo ambayo yangetufanya tutoe machozi sana, lakini Mungu umetuepusha nayo yote. Asante Mungu mwenye rehema.
7. Tumekutana na hali ngumu za kuvunja moyo. Kwa neema yako tumefarijiwa. Asante Mungu Mfariji
8. Umetupa mvua na chakula cha kutosha. Asante Mungu mwaminifu.
9. Katika ndoto zetu usiku, ulizungumza nasi na kutuonya. Asante Mungu Mtakatifu.
10. Katika nusu hii ya mwaka, tumesikia habari za vita na machafuko, zilizotufanya tusikitike. Umetukumbusha kuwa mwisho umekaribia, karibu Yesu atakuja kutufuta machozi. Asante Mungu mwenye pendo kuu.

Nakushukuru kwa Jina la Yesu Kristo. Amen
 
Mungu amekufanyia nini katika miezi sita iliyopita? Mshukuru hata kwa maneno machache, utaona baraka zaidi.

"Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu." (1 Wathesalonike 5:18)

"Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele." (Zaburi 107:1)
 
Mungu Baba umetufanyia mengi sana. Naendelea kukushukuru...

11. Tuliposikia udhaifu, ulinyoosha mkono wako na kututia nguvu mpya. Asante Bwana wa majeshi.

12. Ulipoona tumekengeuka, uliturudi kwa upole na kuturekebisha. Asante kwa upendo wako usio na kifani.

13. Wadudu na wanyama wabaya walisogea karibu na sisi. Hukuwaacha watushambulie. Ulitufunika, Ee Mungu, tukawa salama. Asante sana kwa ulinzi wako.

14. Tulipita katika vipindi vya kuishiwa, lakini tukaona miujiza yako mingi: Ulifanya njia pasipo na njia na kutulisha 'mana' jangwani. Asante Mungu umetupatia kicheko.

15. Tulikumbwa na huzuni ya kuwapoteza wapendwa wetu, lakini ukatufariji na kututuliza roho. Asante Ee Mfariji wa kweli.
 
Mungu Baba pokea tena shukrani hizi...

16. Waliotufanyia hila kazini na kututakia mabaya, mipango yao haikufanikiwa, badala yake ulitupatia kibali machoni pa wakuu. Asante Ee Mungu mwenye haki.

17. Umetupa nafasi ya kusikia Neno lako tena na tena, na kulifanya chakula cha roho zetu. Asante Mungu wa uzima.

18. Ulitufundisha kuwa watulivu hata kwenye mawimbi makali ya maisha. Asante Mungu, Mtetezi wetu.

19. Ulitujalia nguvu ya kusamehe, hata wakati tulipojeruhiwa. Asante Ee Mungu wetu.

20. Ulitufungulia milango ya riziki kwa njia ambazo hatukutegemea. Asante Ee Mungu Muweza wa yote.
 
Ee Mungu, mambo uliyotutendea nusu ya mwaka huu ni mengi. Naendelea kukushukuru...

21. Ulitusaidia kuendelea mbele, hata tulipohisi tumefika mwisho wa safari. Ee Mungu pokea shukrani.

22. Umetuwezesha kuwasaidia wengine hata katika hali zetu ngumu. Asante Mungu wa milele.

23. Tulipoambiwa "haiwezekani", wewe ulisema "Inawezekana!" Asante Mungu wa miujiza.

24. Umetusaidia tusichukuliwe na mafundisho ya mashetani. Asante Ee Mungu mwenye kweli.

25. Umetuwezesha kuimba nyimbo za matumaini hata wakati wa kilio. Asante Mungu kwa kutuwezesha.
 
Back
Top Bottom