Asante Mungu kwa hii zawadi ya Valentine

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,131
8,655
Mambo vipi,

Nisienda mbali jana nashukuru mungu ilikuwa ni siku ya valentine ambayo ni siku ya kuonyeshana mapenzi lakini huenda upande wangu mungu alinipa furaha nyingine kubwa kushinda hayo tunayoyajua.

Mida kama ya saa tano asubuhi jana tarehe 14/2 nikiwa maeneo ya mbezi beach kwenye kijimgahawa nikinywa zangu chai,huku nikisubiria biashara yangu ambayo nilikuwa nataka kuifanya maeneo hayo na mteja wangu.

Akatokea mdada mmoja mzuri tu akiwa amembeba mtoto wa kama miezi 8 na kukaa jirani yangu huku na yeye akiagiza chai na maandazi mawili, baada ya salamu alikuwa anaongea sana na simu mwishoni akaniomba nimshkie mtoto wake ili aende kutoa hela.

Basi mie nikamshka mtoto huku nikishushia zangu maji yangu taratiibu huku nikimsubiria mhusika arudi amchukue mtoto wake lakini nusu saa ilikatika, likaenda lisaa mpaka masaa 3 yakakatika bila mtu kuonekana wala dalili.

To be honest ndo akili ikanifunguka kuwa hapa tayari nimeshatelekezewa mtoto, lakini jambo la ajabu mtoto muda wote alikuwa anatabasamu na kuongea tu huku akicheka cheka muda wote hali iliyokuwa inanifanya nijihisi na amani japokuwa akili nyingine ilikuwa inanambia kuwa hapa mama mtu harudi tena.

Basi nilijikuta nimekaa mgahawani mpaka mida ya saa 10 pasipo mama mtu kujitokeza mie nilichokifanya ni kuongea na wife na kumuelezea situation nzima ya tukio, then nikamchukua mtoto na kuondoka nae mpaka polisi nikiwa na mwenye mgahawa.

Tulivyofika polisi nikakamilisha taratibu zote na yule mmiliki wa ule mgahawa akaondoka zake mie nilikubali kukaa na yule mtoto kwa kumlea kama mwanangu na baada ya kuandikisha maelezo yote polisi, wife akaja kituoni na hati za ndoa kuthibitisha kuwa kweli ninaishi na mke na kuondoka na askari mmoja wa kike mpaka kwangu

Askari baada ya kufika kwangu akajiridhisha na kuondoka na kutakiwa leo niripoti tena polisi kwa ajili ya taratibu nyingine za kuishi na mtoto huyo kama wangu na mengineyo.

Leo asubuhi nimeamkia polisi nikiwa na Mwanasheria na kukutana na mkuu wa kituo na yeye akanibariki juu ya hilo na nikatoka nae mpaka ustawi wa jamii ambako nilikamilisha taratibu zote za kuishi na mtoto huyo kisheria na kuondoka zangu mpaka Kariakoo ambako hela niliyoipata jana yote nmenunua mahitaji ya mtoto kama maziwa, nguo, n.k then nikarudi zangu home.

Home furaha imezidi maana nna mtoto wa kike plus huyu wa kiume familia imeongezeka na nyumba nzima wamemkubali na kumpenda mno hope next week tukijaliwa uhai nitaanza taratibu za kufatilia vyeti vya kuzaliwa na kwa jina nimempa jina la Prince na soon nahamia kwangu hope kataenjoi mazingira tulivu.

Asante Mungu kwa hii zawadi ya valentine uliyonipatia mie na familia yangu
 
Mtoto akikua mwanamke atarudi akuambie nipe mtoto nikupe papuchi(joking)

All the best mzee wa kazi

Ila nina swali, endapo ingekuwa wewe haupo tayari kulea huyo mtoto kwa sababu yeyote ile jeshi la polisi na taasisi yeyote inayohusika na hayo masuala huwa wanachukua hatua gani?
 
Hongera sana mkuu, huyo dada atajutia maamuzi yake ila itakua rahisi kukupata akirudi pale mgahawani. Ipo siku atamtafuta huyo mtoto.
mwezi wa 3 nahama hapa mkuu nahamia kwangu na ntakapohama sijui kama kuna atakayepajua kwa hapa mtaani

pia watu wanaojua hii issue ni watu nnao ishi nao tu nachoshukuru mungu ni kwamba toka jana dogo sjamskia akilia mda ote anaongea na kucheka tu inshort anafurahisha kukaa nae mzuri kwa sura,rangi,mwili ukimuona wangu wakike na huyu wa kiume nikikwambia ni wangu ote wawili hukatai
 
Naombea tu huyo mwanamke asiwe kaiba mtoto wa mwenzie na kuja kutelekeza hapo. Kuna wengine wana roho mbaya wanaiba mtoto na kwenda kutelekeza mitaani mtu anadhani mtoto katelekezwa na mzazi kumbe sio
 
Back
Top Bottom