Asante Mungu leo nimewahama Rasmi NBC

Asante Mungu leo nimewahama Rasmi NBC

Dah, hawa jamaa NBC kumbe bado wapo!! Nilipiga nao sana kazi 2005-2012 so mishahara yangu kama 84 hivi ilipitia huko na niliachana nao kimyakimya baada ya mambo kunishinda sijawahi hata kuingia ndani ya hii benki au kuchungulia ATM zao since 2012. Likadi lao la MasterCard nimeliweka kwenye archive
 
Mpango wa hundi niliwakatalia maana inaweza kuleta usumbufu, niliamua kuchukua madafu yenyewe na kuyabeba kupeleka CRDB.
Kufungua Account CRDB mradi una kitambulisho kinachotambulika kitaifa si zaidi ya saa moja mambo yameshakuwa poa. Ila account number watakutumia kwenye simu au email, ukitaka unaweza kwenda kuchukua, Inachukua siku moja au mbili to process account na kupata account #. Lakini pesa utaziweka kwenye bank wanakupa account ya muda ambayo kesho yake wanahamishia kwenye account yako mpya. Hayo nilifanyiwa miaka miwili iliyopita, inawezekana kwa sasa ni haraka zaidi.

Saivi nilitumia dakika 20 tu
Na ATM kadi unapewa hapohapo...
Nbc nimetupa kule wasumbufu sn
 
aisee mkuu hii crdb wanajitahidi sana kila uchao wanaleta huduma mpya na kuboresha...

Hii internet banking...sim banking ni mkombozi mkubwa kwetu tulio busy na kazi...

Crdb....exim....kcb..boa bank ni chaguo sahihi

vp kuhusu akiba commercial bank? Kwa sie kina yakhe?
 
Nilianza kuwa mteja wa NBC 2006 then nikafungua CRDB 2007,ila 2008 nikaamua kuachana na NBC mpaka leo,wao kadi iki-expire wana usumbufu sana,kero niloipata CRDB mwaka naofungua ni kuncheleweshea ATM yangu while boom lilikua linapitia huko,sikuwah kukutana na upuuz huo mpaka sasa,
 
.... halafu wateja wa laki laki kwa mwezi wakorofi sana, mbona ulipo enda huko NBC haukuja humu kwa masham sham kama unavy ondoka kwa nyodo hivo .... #NYOKO
 
Ila umatumbini kwetu nuksi sana mkuu...

By then wakati ndio ATM zinaanza kuwa installed, na watu kuanza kuzitumia basi kulizuka ujambazi wa kubomoa vibanda vya ATM....imebidi ziwe zinalindwa sasa.

Halafu pia nashangaa Bongo nzima sijawahi kuona Deposit Friendly ATM's, sijui kama kuna benki ina hii kitu aisee...

DTB wana hiyo service.
 
watu8

Masuala ya kuwa na wadhamini watatu wenye account hapo CRDB yamebaki kule NBC tu. CRDB ni kitambulisho chako kinachotambuliwa na serikali na kama huna basi barua ya mwenyekiti wa serikali za kitongoji unachoishi mambo yatakuwa poa.

Msongamano CRDB si mkubwa kama NBC. Jengo la pale PPF mkabala na Posta mpya pamoja na kuwa na wateja wengi kuna matawi mawili ili kupunguza msongamano yameuatana hapo hapo na ATM nyingi.

Kwa vile mteja ni kama mfalme wameweka viti wakati unasubiria kwenda counter unakaa kwenye viti na kusogea mbele kutoka kiti kimoja hadi kingine hadi unafika kwa counter unatokea kwenye seat. Mambo hayo NBC huwezi kupata kamwe.

Mlimani city kuna wateja wengi yes, mimi huwa napendelea pale mjini wana matawi mengi na hakuna usumbufu kabisa kama ni kusubiri basi ni dakika chache.

Barabara ya Nyerere (Pugu road) toka mjini kabla ya Tazara kuna matawi mawili pale Shope and Relax, wanakasi sana katika huduma zao.

Hii ni bank inawafaa na kuwajali sana wafanyakazi, wafanya biashara na wasomi wanaojali muda na uwazi, na ndio maana wanazidi kutanua matawi nchini.

Morogoro kuna matawi mawili, moja kubwa sana pale karibu na kituo cha mabasi cha daladala Masika kabla hujafika kituo kikuu cha daladala mjini. na pale kona ya kwenda uwanja wa mpira au polisi kuna tawi lao pia. Hawa jamaa wanazidi kukata mbuga kiulaini.

:msela:KILA MWEZI WATAKUTUMIA BANK STATEMENT KWENYE EMAIL YAKO




Pamoja na hilo mkuu, kuna matawi mengine kama huku kwetu wameweka mashine ya kutolea namba kwa foleni mlangoni. Ukiingia tu unachukua namba yako unakaa kwenye kiti shwari kabisa unasubiria sauti ya kukuelekeza uende teller namba fulani. Hakuna foleni ya kusimama wala nini.
Safi sana Kimei.
 
NMB kitambo sema foleni yake ni shida
 
.... halafu wateja wa laki laki kwa mwezi wakorofi sana, mbona ulipo enda huko NBC haukuja humu kwa masham sham kama unavy ondoka kwa nyodo hivo .... #NYOKO

Laki laki? Uliza mtu wa mwisho ku withdraw pesa nyingi acc ikabaki empty katika hzo acc zenu famba manake niliacha kama elfu 40 na k2 tu na mkiniuzi zaidi naja kuchukua na hyo kudadadeki zenu
 
Nbc ndo baba lao benki zote ni watoto we mshamba umechemka sana kuihama benki kubwa kuliko zote na wote mnaohama mabenki ni washamba

Peleka laana zako huko hamna bank hapo na vzee vyenu visivyotaka kwenda kuea vjukuu vinang'ang'ana na mateller vimerihiwa tangia kabla haija spirit to nmb bado wamo tu hata noti hawajui wanapapasa tu
 
Baada ya kuwavumilia kwa takriban miaka minane na manyanyaso, Huduma mbovu ndani ya benk kadhalika na Atm machine zao, LEO nimeamua kuachana kabisa na benki hii kwa kufanya mambo yafuatayo
1; nimehamisha salio langu lote
2; nimevunja kadi zao zote kuanzia utambulisho mpaka atm kadi zao
3;nimehamisha mshahara kupitia kwao kudadadeki zao
4;nimezinguana na costomer service manager wao
wa tawi moja hapa town
5;nimekuja kuwapa taarifa humu wana jf wenzangu wanaofikiria kujiunga na benk hii wasithubutu itakula kwao.
Benk hawataki kubadirika, kazi kuajiri midioker tu na watu wasiojiweza, mtu dirishani kwa teller anatumia zaidi ya nusu saa bila sababu ya msingi, na siyo dar tu nimeenda matawi yao kibao kama Tabora, morogoro, dar ndo balaa, mtwARA ndo shida kabisa kudadadeki zao, nimejiendea CRDB yan burudani kumbe nilikuwa nachelewa tu siku zote hz, hongereni CRDB hasa holland branch kwa kazi nzuri.


Mie niliwahama miaka miwili iliyopita.
 
NBC ni wafu watarajiwa kibiashara... yaani mimi nilihama zamani sana... pesa ikipelekwa kwao itawekwa kwnye akaunti after three weeks tena kwa kufuatilia sana ... pia wanawahi sana kufunga eti saa tisa sharp ndo wanafunga ... phiuuuuu
 
Halafu inakuwaje mtu ukihitaji baadhi ya huduma ni lazima uende kwenye tawi ulilofungulia akaunti?

Hawana integrated system?

Mtu uko mjini na unahitaji huduma fulani....unaenda pale makao makuu unaambiwa urudi Mbezi Beach ulipofungulia akaunti yako!

Huu ni usumbufu wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom