Asante Mungu leo nimewahama Rasmi NBC

Asante Mungu leo nimewahama Rasmi NBC

Pamoja na hilo mkuu, kuna matawi mengine kama huku kwetu wameweka mashine ya kutolea namba kwa foleni mlangoni. Ukiingia tu unachukua namba yako unakaa kwenye kiti shwari kabisa unasubiria sauti ya kukuelekeza uende teller namba fulani. Hakuna foleni ya kusimama wala nini.
Safi sana Kimei.

Uko sahihi kabisa nimeona hivyo Morogoro na baadhi ya matawi ya Dar.
 
mkuu umenihamasisha nihame NBC maana kwa kweli ni kero, yaani kwanza huduma mbovu pia wafanyakazi ni slow mno mpaka kero. Wengi ni wazee mno. Mameneja wengi wa matawi ni toka dini pendwa.
 
NBC ni janga la Karne kwa kweli tena wajiangalie maana kuna benki inaitwa EQUITY na KCB & DTB wapo fasta ajabu sasa hao EQUITY baadhi ya branch ndo wanafunga saa 11 nyingine kama QUALITY CENTRE wanafunga saa 1 usiku (masaa 4 baada ya NBC kufunga) ha ha
 
Halafu huwezi kutoa zaidi ya Tshs. 200,000/- kwenye ATM zao kwa mkupuo. Imagine unataka kutoa 1M!
Zipo ATM za NBC zinazotoa mpaka 400000 at time inategemea na ukubwa wake mimi kitakachonifanya nihame hii bank ni kusuasua kwa huduma na kuahidi kutoa mikopo alafu wakakwepa
 
mkuu umenihamasisha nihame NBC maana kwa kweli ni kero, yaani kwanza huduma mbovu pia wafanyakazi ni slow mno mpaka kero. Wengi ni wazee mno. Mameneja wengi wa matawi ni toka dini pendwa.

Dini pendwa ndo ipi?
 
Zipo ATM za NBC zinazotoa mpaka 400000 at time inategemea na ukubwa wake mimi kitakachonifanya nihame hii bank ni kusuasua kwa huduma na kuahidi kutoa mikopo alafu wakakwepa


ATM za Mwanza option ya juu kabisa ni 200,000/-!
 
Nami wameblock akaunti yangu eti sijui nipeleke taarifa gani sijui! Eti kila mwaka nitakuwa napeleka taarifa! Ngoja nipeleke hizo taarifa, waifungue, nikombe kila kilichomo na kuachana nao! Nyamaf!
 
NBC ni wafu watarajiwa kibiashara... yaani mimi nilihama zamani sana... pesa ikipelekwa kwao itawekwa kwnye akaunti after three weeks tena kwa kufuatilia sana ... pia wanawahi sana kufunga eti saa tisa sharp ndo wanafunga ... phiuuuuu

Duu hiyo kali ya kubembeleza deposit....
 
Crdb wenyewe wanajisahau sana, foleni za kijinga. Wananichosha sana. Wateja wanakuwa kwa kasi ila hawatanui matawi yao hasa zile sehemu zenye mizunguko mikubwa kama dar. Ukienda mcity kama mtu usiependa foleni utaishia kukasirika tu

Huwa najiuliza kama hawana wafanyakazi wa kutosha au nini? Manake ukifika counter ndio unagundua kuwa tellers wako wawili (labda) na counter nyingine ziko tupu!
 
Mimi pia nipo mbioni kuondoka huko kwa sababu waliweka matangazo yao ya mobile banking, nikajaza From na wakaniambia kuwa baada ya siku tatu (3) nitapata sms ikinieleza jinsi ya ku-activate hiyo Mobile Banking. Baada ya wiki mbili sikupata sms yoyote ikabidi niende tena kwenye tawi nililojaza form. Baada ya kuangalia kwenye data zao wakadai kuwa hawazioni wakanishauri nijaze tena na nikafanya hivyo. Wakasema tena nisubiri siku 3 nitapata sms. Ikapita mwezi sikupata sms yoyote, nikaenda tena wakanipa form nyingine tena ambayo ilikuwa na tofauti kidogo na zile 2 za mwanzo wakaniambia nisubiri nitapata sms. Leo hii ninavyoandika hapa nadhani ni miezi 6 kama siyo 8 tangu nijaze form ya mwisho na sijapata sms wala simu wala ujumbe wowote!!!!Wakati CRDB nilijaza form siku 1 na baada ya saa 24 nilipata sms na hadi leo nina-enjoy huduma za Simbanking.


Daah...hii rekodi ya fomu kiboko...
 
Nipo CRDB ila nampango wa kuwa na Account ya Exim. Wako vizuri sana na baadhi ya branch zao hufungwa saa tatu usiku
 
Nimeisusa account yangu ya NBC,sasa hivi nipo na Exim na Dtb. Hawa Dtb Monday to Friday wanafungua SAA mbili kamili asubuhi mpaka SAA mbili kamili usiku! Jumamosi na jumapili wanafungua nusu siku.
 
Nazidi kuhamasika kuachana nao kabisa.

Mi niliamua na management nzima tukafunga akaunti zote za wafanyakazi, tukawafungulia CRDB kwa gharama za organisation na tangu hapo hata hawakutuuliza sababu.
 
Hahaa....NBC sina hamu nao, kinachouzi ni mtu kukaa dirishani kwa teller nusu saa, huduma mbovu sana.

Hamia TWB haha
 
Baada ya kuwavumilia kwa takriban miaka minane na manyanyaso, Huduma mbovu ndani ya benk kadhalika na Atm machine zao, LEO nimeamua kuachana kabisa na benki hii kwa kufanya mambo yafuatayo
1; nimehamisha salio langu lote
2; nimevunja kadi zao zote kuanzia utambulisho mpaka atm kadi zao
3;nimehamisha mshahara kupitia kwao kudadadeki zao
4;nimezinguana na costomer service manager wao
wa tawi moja hapa town
5;nimekuja kuwapa taarifa humu wana jf wenzangu wanaofikiria kujiunga na benk hii wasithubutu itakula kwao.
Benk hawataki kubadirika, kazi kuajiri midioker tu na watu wasiojiweza, mtu dirishani kwa teller anatumia zaidi ya nusu saa bila sababu ya msingi, na siyo dar tu nimeenda matawi yao kibao kama Tabora, morogoro, dar ndo balaa, mtwARA ndo shida kabisa kudadadeki zao, nimejiendea CRDB yan burudani kumbe nilikuwa nachelewa tu siku zote hz, hongereni CRDB hasa holland branch kwa kazi nzuri.

Hilo nalo ni la kumshukuru Mungu!?
 
Back
Top Bottom