happiness win
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 2,461
- 1,394
Si uongo NBC Kimeo, naanza mkakati..... new bank account, nahamisha mshahara, nitawabwaga bwaaaaaaaaaaaaaa
Ila umatumbini kwetu nuksi sana mkuu...
By then wakati ndio ATM zinaanza kuwa installed, na watu kuanza kuzitumia basi kulizuka ujambazi wa kubomoa vibanda vya ATM....imebidi ziwe zinalindwa sasa.
Halafu pia nashangaa Bongo nzima sijawahi kuona Deposit Friendly ATM's, sijui kama kuna benki ina hii kitu aisee...
Sasa mnatutisha bana!
Manake nikifikiria hela niliyonayo huko nakosa raha kabisa.
Kama ni mgonjwa NBC yuko ICU
Wewe utakuwa Marketing Manager wa CRDB, lakini unajaribu kujificha kwenye koti la aliyekuwa mteja wa benki ya NBC!Baada ya kuwavumilia kwa takriban miaka minane na manyanyaso, Huduma mbovu ndani ya benk kadhalika na Atm machine zao, LEO nimeamua kuachana kabisa na benki hii kwa kufanya mambo yafuatayo
1; nimehamisha salio langu lote
2; nimevunja kadi zao zote kuanzia utambulisho mpaka atm kadi zao
3;nimehamisha mshahara kupitia kwao kudadadeki zao
4;nimezinguana na costomer service manager wao
wa tawi moja hapa town
5;nimekuja kuwapa taarifa humu wana jf wenzangu wanaofikiria kujiunga na benk hii wasithubutu itakula kwao.
Benk hawataki kubadirika, kazi kuajiri midioker tu na watu wasiojiweza, mtu dirishani kwa teller anatumia zaidi ya nusu saa bila sababu ya msingi, na siyo dar tu nimeenda matawi yao kibao kama Tabora, morogoro, dar ndo balaa, mtwARA ndo shida kabisa kudadadeki zao, nimejiendea CRDB yan burudani kumbe nilikuwa nachelewa tu siku zote hz, hongereni CRDB hasa holland branch kwa kazi nzuri.
Wewe utakuwa Marketing Manager wa CRDB, lakini unajaribu kujificha kwenye koti la aliyekuwa mteja wa benki ya NBC!
Crdb wenyewe wanajisahau sana, foleni za kijinga. Wananichosha sana. Wateja wanakuwa kwa kasi ila hawatanui matawi yao hasa zile sehemu zenye mizunguko mikubwa kama dar. Ukienda mcity kama mtu usiependa foleni utaishia kukasirika tu
Mkuu juzi nilienda ya pale Chuo Mlimani walai kwa saa moja walihudumia watu 3....hiyo bank haifai kabisa
Just ignore, (he is wasting time with NBC). Tunahangaika na dhana kubwa haya mambo ya spelling ni madogo na wanaofikiri kidogo ndio they mind.Mkuu hapo kwenye west ulitaka maanisha nini? Au ulitaka sema waste??
Sijui kwa siku za karibuni lakini hao CRDB zamani walikuwa wananikera sana na kile kipengele chao cha kuwa na mdhamini ambaye ni mteja wa CRDB pindi unapotaka kufungua akaunti CRDB.
Pia kwenye matawi yao hususani hapo Dar es Salaam, huwa yanajaza sana wateja kiasi kwamba inakubidi usubiri sana kupata huduma. Kuna matawi sugu kwa kuwa na watu wengi haswa yale ya mjini kati kama Holland, Azikiwe na pia pale PPF Tower...Mlimani City ndio usikaribie kabisa maana hadi kwa ATM mshine kuna msururu utadhani enzi za kununua Yanga yanga....
Hata hivyo kwa sasa mji kama wa Dar es Salaam una mabenki mengi tu yenye huduma zisizo na usumbufu zenye kujali muda pia. Pengine alternative hiyo ya CRDB ni muafaka kwa wale watumiaji wa huduma za mabenki walio nje ya Dar...
Halafu huwezi kutoa zaidi ya Tshs. 200,000/- kwenye ATM zao kwa mkupuo. Imagine unataka kutoa 1M!
Kuna siku nilienda hapo nikiwa na haraka nikatamani kupasuka kwa hasira
Akaribie ila uvumilivu muhimu