Sana angetoboa hapo siyo mwenzetu ndio maana utajiri una siri nzito sana hao wapo 20 kila kichwa minimum usd 2000 maana yake alikuwa anapiga 100m kama amesimama
Kichwa chenye uwezo wa kutoa USD 2000 hakisafirishwi hivyo.
Akili ya kawaida na uzoefu wa kutafsiri haukubaliani.
 
Hata mimi huwa nikisafiri na ninajua nitavunnja sheria za usalama barabarani huwa naweka bendera ya CCM mbele na kofia juu ya dashboard na wimbo wa Capt. John Komba. Napitaga tu tena trafiki huniombaga hela ya chai nawarushiaga 3000/= wanagawana.
 
Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji”


Chanzo: Ayo TV
Wamerushana wakachomana itakuwa. Sio rahisi vx lenye bendera ya ccm kusimamishwa na askari barabarani.
 
Back
Top Bottom