Arusha yarindima kwa risasi! Jambazi laua polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha yarindima kwa risasi! Jambazi laua polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mkirua vunjo, Jan 3, 2012.

 1. m

  mkirua vunjo Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Arusha imetikiswa na mrindimo ya Risasi eneo la Bara bara mpya kuelekea Tangeru baada ya daraja la nduruma, baada ya polisi kuvamia nyumba moja ili kulishikilia jambazi sugu, inasemekana kuwa baada ya kuzunguka nyumba yake jambazi huyo alitoka na kupiga risasi hewani na kumuuwa polisi moja na mwingine kujeruhiwa vibaya... habari kamili tutawaletea baadae

  Nawasilisha

  UPDATE:

  [​IMG]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA BW THOBIAS ANDENGENYE AKIZIPANGA RISASI
  AMBAZO ZILITUMIKA KATIKA TUKIO LA KUUA ASKARI KATIKA ENEO LA SHANGARAI


  KATIKA hali isioyokuwa ya kawaida askari polisi F 228 Constebo Kijanda Mwandru amefariki dunia, pamoja na mkuu wa upelezi wilaya Faustine Mwafele kujeruliwa vibaya na jambazi sugu mkoani hapa ambaye amejulikana kwa jina la Hendry Samson Kaunda. Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Andengenye Thobias alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saakumi za alfajiri.

  Kamanda Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo lilitokea mara baada ya askari hao kwe nda kwa ajili ya upekuzi katika nyumba ya Bi Agness Silas ambayo ilikuwa ikitumika kwa ajili ya makazui ya majambazi mjini hapa. Alibainisha kuwa mara baada ya askari hao kufika katika eneo la tukio kwa bahati mbaya jambazi hendry aliwavamia askari hao na kisha kuwapiga kwa risasi mfulululizo hali ambayo ilimsabbishia kifo askari huyo pamoja na kumjerui Mrakibu huyo wa wilaya ya Arusha vijijini.

  Pia alisema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo polisi waliendelea na msako mkali katika nyumba hiyo ya Bi Agness ambayo ilikuwa inasadikiwa kuwaficha na kuwatunza majambazi na kisha kukuta vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vinatumika kwa ajili ya shuguli za ujambazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

  Alitaja Vifaa hivyo kuwa ni pamoja na risasi 36,risasi 12 aina ya Short gun ,kitako kimoja cha bunduki aina ya Shortgun,pamoja na soksi za kuvaa usoni ambazo walikuwa wakizitumia majambazi hayo katika shuguli mbalimbali za uhalifu.

  Bw Andengenye alieleza kuwa katika tukio hilo watoto wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi ambapo watoto hao ni DainessMsawe(9) pamoja na Alex Paramina (13) ambaye ndiye aliyefumfungulia mlango Jambazi aliyeuwa na kujerui askari polisi. Aidha mrakibu wa jeshi la polisi bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Selian wakati polisi ikiendelea na msako dhidi ya majmbazi hayo yaliyokimbia.

   
 2. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Aksante kwa habari more updates please.
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Duh!poleni.walienda kichwa kichwa!
   
 4. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hata picha unaweza ukatuwekea pia
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa mkuu!
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Asante....ila hii sio siasa ndugu....angalizo tu
   
 7. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa polisi sijui kwanini hawajifunzi kuwa makini wanapoenda kufanya 'raid'. Mimi nakumbuka nilishawahi kumtishia polisi mmoja na bastola ya toy, yaani alitoka nduki huyo utasema mwanamke anakimbia wabakaji.
   
 8. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ina ka-uhusiano fulani na siasa. Jaribu kuchunguza kwa makini utagundua.
   
 9. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  Huyo Jambzi siyo MWIZI WA MAGARI???
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Utamwingiza LEMA sasa hivi!!!
   
 11. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tatizo la Polisi wetu badala ya kufundishwa mbinu za ku-arrest wahalifu, wanafundishwa siasa na jinsi ya kuwamwagia maji ya upupu wapinzani wa CCM. Matokeo yake ndio hayo, wanakwenda kumkamata Jambazi sugu kana kwamba wanakwenda kumkamata Mbowe au Lipumba.
   
 12. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  alipiga risasi hewani akamuua polisi mmoja, je hao polisi wakua wanashuka kwa mwamvuli au walikua wanachoppa? lakini inawezekana allizingira juu ya paa. Nasubili habari kamili. Mia
   
 13. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  mia le....a
   
 14. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mia - Walikuwa ni para-troops hao - Mia
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 16. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hapa ndo nashindwa kuelewa, alipiga risasi hewani, akaua askari mmoja a kujerhi wingine vibaya. Hawa askari walikuwa juu ya mti, paa ama wapi?

  Lete taarifa kamili ndugu
   
 17. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wapiga kura wa LEMA hao!
   
 18. V

  VAMPA Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwita ondoa skendo hapa, kwa hiyo wewe bado unachezea matoi? una umri gani?
   
 19. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Huyo Jambazi walifanikiwa kumkamata?
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  polisi wenyewe waoga ka nini wataweza wapi mambo hayo ya raid
   
Loading...