Arusha: Wananchi waandamana kumuunga Mkono Rais!

Arusha: Wananchi waandamana kumuunga Mkono Rais!

Mie nimeona tai ya kijani au utasema ni Waziri Mwigulu? Bwana Ngushi naona nyie mmeshaamua liwalo na liwe, hadi binti wa Sokoine mkamkataa alipokataa ujinga wa kwenda chadema.
Wekeni picha kulikuwa Ipad iliyokuwa ikiwapiga.Ni full vichekesho.
 
Kuna maandamano makubwa yamemalizika muda si mrefu katika jiji la kitalii na kiharakati...yamepokelewa na DC wa Arusha.

lengo la maandamano hayo ni kuunga mkono hatua za Rais Magufuli kusimamia Rasilimali za nchi.
View attachment 527071
Baadhi ya Wananchi wa Arusha wakifanya Maandamano yakumuunga mkono Rais Magufuli

My Take:
Tuwapongeze wananchi kwa uelewa na kuwa wamoja kama Taifa.
Duh!! Umati unatisha!!!!
 
Waandamane upuuzi kama Tanzanite imeshawahi kuwanufaisha
 
Naona mikokoteni ya kuwabeba viongozi au matunda kwenda soko la kilombero ?
 
Kumbe maandamano yanayozuiwa ni ya kupinga. Ya kusifia yanaruhusiwa! Demokrasia imekua sana katika nchi yetu.
 
Nilipishana nao mchana.ni kakikundi ka vijana waliotayarishwa na uongozi wa mkoa kwa ajili ya kutengeneza hii sinema.
Watu walikuwa wanawashangaa wengine wakiwatukana.
 
Nilipishana nao mchana.ni kakikundi ka vijana waliotayarishwa na uongozi wa mkoa kwa ajili ya kutengeneza hii sinema.
Watu walikuwa wanawashangaa wengine wakiwatukana.
Mbona hukuleta hiyo taarifa?
 
hahahahahahahaha Jingalao kweli umeamua, unajisikiaje kwa taabu yote unayopata kujaribu kuubadili mchana kuwa usiku.
Unajisikiaje usiku unavyobadilika kuwa mchana?
 
Back
Top Bottom