Arusha- Mji wa kitalii - mji uliojaa kinyesi

Arusha tatizo ni wakazi wanaoishi hapa. Kila mahali ni pachafu hata majumbani kwa watu ni wachafu. Niliwahi kumwona dada fulani kaotesha majani (Garden) pembezoni mwa barabara uongozi ukwamuamuru ayang`oe, kisa ni aneo la barabara.Pita Kimandolu Stendi pembeni kabisa ya barabara ya Arusha- Moshi kuna dampo limewekwa hapo na hii ndio Kata anayotoka Meya Msaidizi aliyejichakachua mwenyewe. Tatizo ni USTAARABU hatuna watu wa A-Town.

ni kweli kabisa,..ila tatizo hili la uchafu sio arusha pekee_nenda dar(anakoishi presidaa wako kunanuka shombo)utatamani ujinyonge mkuu,...issue hapa ni tubadili tabia ikiwa ni pamoja na kuacha kutema mate ovyo
 
Tumia neno "VINYESI"............... Wewe ni Muarusha nini?

suala sio kabila hapa, ukiona mtu ameshindwa kutumia tafsida jua hicho kitu kilikua kinamkera ila hakua na pakusemea, vibarabara vyenyewe vidogo na vingi vumbi tupu, sasa ukijumlisha na hayo mavi ndo usipime, tembelea wakati wa masika ndo utanielewa vizuri.....wale wamama wa sokoni wanavaa zile boots na kupanga mboga za majani chini yani ni aibu tupu.....huwezi amini ile kitu inaitwa geniva of africa ndo imetapakaa mavi kiasi kile tena pale mjini kabisa....shame on who ever concerned!!
 
Sasa mnalalamika nini huku mnalilia si mwambieni Lema sindio Mbunge wenu wa Arusha
 
ni kweli kabisa,..ila tatizo hili la uchafu sio arusha pekee_nenda dar(anakoishi presidaa wako kunanuka shombo)utatamani ujinyonge mkuu,...issue hapa ni tubadili tabia ikiwa ni pamoja na kuacha kutema mate ovyo
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa kuwa lazima wakazi wa maeneo husika wabadilike lakini uongozi unaweza kulisimamia hili kuweka sheria nikupe mfano mdogo...miaka miwili iliyopita chini ya standi ndogo watu waligeuza choo palikuwa hapafai nennda sasa hivi ukapaone, huku polisi tarafic karibu na ile njia ya kuibukia AA Computers kulikuwa hakufai watu waligeuza choo ilikuwa ni mavi tu lakini leo hii subutu hata kukojoa inakula kwako na pamekuwa pasafi huwizi amini kwahiyo swala ni sheria binadamu ndivyo tulivyo bila kuweka sheria na kusimamiwa hakuna linaweza kufanyika, lakini la mabomba kuziba je ni la wanachi kutema mate hovyo au ni la kiuongozi...
 
Sasa mnalalamika nini huku mnalilia si mwambieni Lema sindio Mbunge wenu wa Arusha
kuna watu wanawajibika ndiyo tunao walalamikia hata Lema kama mbunge baada ya kesi kusikilizwa tutaenda kufungua ile barabara aliyo iziba mke wa mkuu wa mkoa kisa magari yana timua vumbi nyumbani kwake kama atakuwa hajatoa maelezo ya kutosha maana alishaandikiwa barua....harafu tutakuja kwa hawa wanaohusika na mavi...
 
Mamlaka yenye dhamana ya kukussanya kodi na kuweka mji katika hali inayostahil kwa maisha ya binadamu ni manispaa/halmashauri ya jiji la arusha.
Hawa ndio wanaotakiwa kuratibu mambo yote yahusuyo miundombinu. Kama mitaro na chambers zinavuja hovyo, kamkamateni mkurugenzi, mumuulize fedha za kodi anapeleka wapi? Na idara zake zinafanya nini?
Unalilia nini wewe si umwambie Lema akitoe hivyo vinyesi vyenu! Kwani kazi ya Lema nini au Maandamano tu ndio mnayojua.
Acheni uchafu nyie watu wa Arusha, mnajisaidia hovyo hovyo halafu mnalalamika
 
Sasa mnalalamika nini huku mnalilia si mwambieni Lema sindio Mbunge wenu wa Arusha

yaani mpaka sasa haujui bado tunacholalamikia_kweli wewe kichwa ngumu,anyway..tunalalamika miji/majiji yetu ni machafu sana(hii ikiwa ni pamoja na dar)na wakubwa wanaonekana kutojali kabisa,.umelewa sasa nafikir
 
Unalilia nini wewe si umwambie Lema akitoe hivyo vinyesi vyenu! Kwani kazi ya Lema nini au Maandamano tu ndio mnayojua.
Acheni uchafu nyie watu wa Arusha, mnajisaidia hovyo hovyo halafu mnalalamika
Tatizo lako mkuu Ritz unakurupuka sana....Lema siyo mbunge wa kuzibua mabomba ya mavi kuna wanaohusika na tunawalipa kwa kazi hiyo kama wewe unavyo lipwa na Nepi...
 
Unalilia nini wewe si umwambie Lema akitoe hivyo vinyesi vyenu! Kwani kazi ya Lema nini au Maandamano tu ndio mnayojua.
Acheni uchafu nyie watu wa Arusha, mnajisaidia hovyo hovyo halafu mnalalamika

Hebu niambie unaishi wapi tz hii ambako hii kero haipo,....acha mashauzi yasiyo na mshiko
 
wakuu hii yote inachangiwa pia na siasa....

Safi naona omeona mbali ha CCM wata hakikisha nyie hapo arusha hamfurukuti, CCM hilo hawajui kama ndipo wanapo haribu zaidi wakipenda hapo arusha pawe shwari wamalize haraka mgogoro wa Madiwana na Mayor wafanye uchaguzi upya then ndipo patatulia kwani kwa takwimu zangu nilizo pata Mwanza,Musoma,Arusha,Moshi,Iringa,Mbeya, na Dar CCM haina nguvu tena kabisa kwani wapiga kura wengi ni vijana na wengi wao wako CDM na hata vijana wanao support CCM huwaunga mkono vijana wenzao wa CDM hilo CCM wanajifanya kupotezea na ndipo hapo wanapo kosa ushiriokiano na raia, katika hili CCM waache kuwavuruga wananchi la sivyo ndio itakuwa inajiharibia zaidi,
Serikali ya CCM kufikisha huduma tu huku mijini ni taaaabu kweli nastahajabika ati wanapanua mikoa na kuongeza huku matatizo yaliyopo ni taabu kweli kutatua, kukuza mikoa mingine mipya kwa kisingizio cha kufikisha huduma haraka kwa wananchi si kisingizio hata tu ya maji taka mijini serikali imeshindwa sasa kufikisha huduma huko mikoa mipya itaweza??

Hizi siasa chafu ndio chanzo cha miji mingi kuwa michafu hizi Malimashauri hazi kai na kuweka mikakati mathubuti ya kukuza miji wao ni kuchonga madeal tuu basi sasa kama hili la maji taka kufumuka mjini lina leta picha gani??
 
Tatizo lako mkuu Ritz unakurupuka sana....Lema siyo mbunge wa kuzibua mabomba ya mavi kuna wanaohusika na tunawalipa kwa kazi hiyo kama wewe unavyo lipwa na Nepi...

Ana ukuu gani huyu,...anapenda kujenga hoja hasi kwa kila jambo
 
Unalilia nini wewe si umwambie Lema akitoe hivyo vinyesi vyenu! Kwani kazi ya Lema nini au Maandamano tu ndio mnayojua.
Acheni uchafu nyie watu wa Arusha, mnajisaidia hovyo hovyo halafu mnalalamika

Hapo mbunge inamuhusu nini?? Hebu jibu hoja kama mtu mzima ni swala la usafi hapo twahitaji mtu atupe data za nani muwajibikaji wa maji taka. Kama ni idara ya maji hapo arusha ndi inayo wajibika then we need tio point fingers directly to them period na sio wabunge kuwataja at least ungemtaja diwani wa eneo hilo na isitoshe kwa kumbu kumbu ni Diwani kupitia kiti cha CCM ndio muhusika wa eneo hilo maana palipo tajwa ni Palison kwa yule atiji aliye mwagaga mapesa gorofani navyo kumbuka.

My Take;
Ndg Ritz angalia hoja ya kuhusisha wabunge na sio kukurupuka tu na kutaja mbuge wa eneo husika ndio kazi yake na hizo manispal zinafanya kazi gani??
NB;
Ni aibu na kwa Tatizo la umeme kutokuwaka Jmosi Dar AirPort nayo tusema Mbunge wa CCM nae anahusika itakuwa ni point hiyo kweli?????
 

Masaki mbona hovyo tuu,....hata magogoni kwa mkuu wenu wa kaya kuna nuka shombo,....acha ushabiki usio na maana,...hata kama unaishi masaki mbona una mdogo yako anayeishi temeke,...tandika,keko......
 
Kazi ya kuzibua na kutengeneza mifumo ya maji taka ilishaondolewa manispaa siku nyingi labda miaka kumi na tano iliyopita ieleweke si Arusha peke yake bali majiji na manispaa zote Tanganyika.Kazi zote zilihamishiwa AUWSA Arusha Urban water & sewarage Authority [Mamlaka ya maji safi na maji taka Arusha.

AUWSA imeshindwa kazi kabisa hakuna maji safi kwenye mabomba badala yake wameamua maksudi kuachilia maji taka kwa kwenda mbele.AUWSA ni hodari wa kununua magari mazuri eg Nissan na Land Cruiser,ni hodari wa kullipana mishahara mizuri na mayuniform ya rangi ya bahari.

Nenda AUWSA na tatizo dogo ambalo fundi mmoja angeweza kulishughulikia utakumbana na mlolongo wa maafisa kibao sijui nenda kwa Technical Manager ukitoka nenda kwa Busness Manager hajakaa vizuri nenda kwa Meter Supervisor ukigeuza shingo unaambiwa ili ni suala litamalizwa na Human Resource Manager !.Kwa ujumla hizi mamlaka zimeshindwa kazi malengo na madhumuni ya uanzishwaji wake yamewekwa pembeni kabisa.
Utashagaa tatizo la maji safi Arusha limekuwa sugu uku mji ukizungukwa na mito mingi na vyanzo kibao vya maji badala ya kujikita na uchimbaji wa mabwawa kwaajili ya kuhifadhi maji wakati wa kiangazi bodi imebuni mradi wa kujenga jengo refu kwaajili ya kuwasitiri waafisa kibao wasiokuwa na kazi za kufanya.

Idara ya maji taka ndiyo imesahauliwa kabisa tangu aliyekuwa meneja wa sewerage alipoukwaa uDirector wa mamalaka ya Maji Tanga.Wapo wafanyakazi waliohamishwa toka Halmashauri ya manispaa ya Arusha wamejikatia tamaa kwa manyanayaso na ubaguzi usiokwisha [Wageni].
 
Unajua vitu vingine ni majukumu ya mbunge wa eneo husika ndio anatakiwa kushughulikia.
Tawapeni mfano mmoja mimi binafsi mbunge wangu ni Halima Mdee, imepita miezi kama miwili alifanya mkutano na wapiga kura wake maeneo ya Kawe, nilikuepo kwenye mkutano huo Mbunge wetu Halima Mdee, alisema wenye kero yoyote naowamba mniambie ili nizishughulikie.
Wapiga kura wakaeleza kero zao mbunge hakazichukuwa na baadhi kazifanyia kazi kama mbunge na katatua baadhi ya kero ikiwemo usafi. Sasa nyie mjaribu kumpelekea Lema haya matatizo au yeye sio muhusika
 
Back
Top Bottom