Arusha: Mgomo wa daladala na pikipiki

Arusha: Mgomo wa daladala na pikipiki

Kila nikitafakari maneno mazito ya mh. Lema, napata hisia kali ya ukombozi, hata vinyweleo vya ngozi yangu hunisimama, machozi hunilenga, nauona mlango wa ukombozi, naiona nuru ya ukombozi ikiangaza kutoka kaskazini. Viva TZ.
 
Hao wanaogoma wanamgomea nani? Halafu wewe Crashwise, acha kuwasemea watu wa Arusha kama kugoma goma peke yako na Toyo yako
Acha atuhabarishe kama vipi hutaki kusikia kajisaidie ulale, hizi si enzi za RTD huwezi zuia nguvu ya internet.
 
Sinto shangaa watu hawa kugoma, kwani siku zote watu wa arusha wamekuwa wanashikwa masikio na fikra zao ni changa

Sema ungekuwa mkoa mwingine ningewaasa kuchukua precautionary measures. Lakini kwa Arusha! sio lazima, maana madereva wa dala dala na boda boda wa kule ni wasomi wengi wao wana degree mbili i.e masters wachache tu wana ka-degree kamoja, kwa hiyo wanajua wanachofanya, kwa maslahi yao.
 
kwanini wanachadema tusitafute njia nzuri ya kupata suluhisho la hili jambo? tunataka kupoteza tena wenzetu? Tusipende kumwaga damu kwa jambo lisilokuwa na Msingi. kama Mh Lema kaamua kwenda gerezani, tumwache apumzike huko, sisi huku tuendelee kukijenga chama!

We Nimtanzania kweli? Au mtu wa kuzimu?
 
Haya ni maneno tu. Lema anajitafutie cheap popularity kwa hili. Tayari tumeshaona uwezo wake wa kufanya kazi. Chadema bado ni changa, tuache ushabiki.. kwa sasa watu tunashabikia anachokifanya Lema, but kina bad impact kwa chama.
Waliozoea kudhalilishwa huwa hawaoni hata wakivuliwa nguo mbele ya watoto,kuimarisha chama ni jambo endelevu haimaanishi tukae tunyamaze na kuinamisha vichwa chini eti kwasababu ni kichanga,hata mtoto ili atembee lazima apitie changamoto mbali mbali ,hivyo kutudhalilisha siyo sababu ya kutunyamazisha,anachotendewa Lema hata sisi kinatugusa.
 
Sema ungekuwa mkoa mwingine ningewaasa kuchukua precautionary measures. Lakini kwa Arusha! sio lazima, maana madereva wa dala dala na boda boda wa kule ni wasomi wengi wao wana degree mbili i.e masters wachache tu wana ka-degree kamoja, kwa hiyo wanajua wanachofanya, kwa maslahi yao.
hahahahahahaahahahahahaahahahah
 
Asante sana.....leo kila mitaani nimeshangaa sana watu wako vikundi wana fatilia JF na kuusoma walaka wa Lema nikaona kuna haja ya kuuprint angalau kiasi na radio station za hapa Arusha wameusoma kuanzia jana jioni na leo Asubuhi naamini mpaka sasa mwana- Arusha(Mjini) ambae atakuwa hajui kinachoendelea basi ni wachache sana........
Nafarijika kusikia redio zinausoma maana kuna mtu jana alisema ni watanzania wachache sana walio na habari ya waraka wa Lema eti hawafiki hata 1/40 nikamuuliza anajua 1/40 ya watanzania ni ngapi hajanijibu hadi sasa.
 
Inawezekana kabisa mtu ukishakuwa Madarakani uwezo wa kufikiri unapungua, just thinking wide, maana dalili zoote zinaonekana lakini wapi!!, macho yao hayaoni, masikio yao hayasikii, something like Gadaffi type.
 
Mkuu kwa hiyo mtasaidiwa na Nato?
Kwani mzee mmeshamchagulia kalavati? maana Gaddafi alikimbilia kwao Sirte akaona sehemu ya kujificha ni kwenye mtaro, sasa ninawasiwasi na makalavati ya Bwagamoyo.
 
Duh hatari kubwa kwahiyo kesho nitoke na kile kiNoah changu kazi kweli kweli.

Watakaopata adha ya usafiri ni walalahoi wakubwa watapeta na miVX yao kama kawaida nadhani hili zoezi la kuandaa migomo lingeangalia nani mwathirika mkuu.

Hongereni ujumbe umefika.

Mawazo ya woga hayo.... mlalapuuuuuuuuuu anaathirika zaidi...... wa ma-vx waache watese kwa muda... mwisho wao uko karibu .. inaonekana hawasomi nyakati....!!!!! Masikini akichoka ...........!!!!! anakuwa zaidi ya viper snake.........!!!
 
Back
Top Bottom