ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

HABARI

Wamiliki wa shule, meya, waandishi wawekwa chini ya ulinzi shuleni Lucky Vincent


By Mwandishi Wetu, Mwananchi
ADVERTISEMENT

ADVERTISEMENT
Arusha. Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.

Source

http://mobile.mwananchi.co.tz/Habar...597580-3932034-format-xhtml-lkt8ww/index.html
 
Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa . Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?

Kama hii habari ni kweli basi tulikofika ni pabaya sana tena sana! Pole kwa wote waliofikwa na masaibu haya, ila yana mwisho, na mwisho wake hauko mbali!!!
 
Kama ni mkutano wa uchochezi ni sawa tu. Meya kaumbuka kwa kudai serikali imekula pesa, sasa wanataka kutumia siasa kufanya maajabu juu ya ajali iliyogusa wengi.

Mlianza mitandaoni kutishia kutumi nguvu kuichafua serikali, hiyo haikubaliki kabisaaaa.

Ni bora muweke sera zenu mbele zijulikane tho hamna, kuliko kudandia majambo kutafutia kiki.

Mengine tuheshimu dola itupe maelezo zaidi.
 
Kipindi ambacho watoto wetu wanahitaji wataalam wa tiba za saikolojia ili kuwapa nasaha baada ya kupoteza marafiki zao, wanasiasa wapumbavu wanatafuta umaarufu!
Wale watoto akili zao hazijakaa vizuri, ugeni wa watu ambao sio wale waliozoeleka hapo shuleni vinaamsha majonzi upya! Wanasiasa acheni uharamia na tamaa!
Nimetafuta tusi zito limekosa,........Mungu nipe moyo wa uvumilivu!

Uko sawa kweli humo kichwani? Angekuwepo Lema ungerukwa akil zaidininavyona!
Hivi kwa akili ya kawaida na taratibu zetu, kufariji haimanishi kuwatembelea, kukaa nao, kuwaonyesha kujali? Hao wataalam wa tiba za saikolojia (? umesema tiba???) wangefanya nini? Wako wapi? Watafika hapo lini? Imagine uko kwenye limbu la majonzi unaletewa mtu usiyemfahamu aanze kukuhubiria eti ni saikologia! Bure kabisa! au ndizo siasa zenyewe!?
 
Polisi Arusha inawashikilia takribani Watu 24 wakiwemo wanahabari waliokuwa wakishuhudia shirikisho la wamiliki wa shule binafsi Tamongsco wakitoa rambirambi ya sh,million 18 kama pole katika shule ya Lucky Vincent Leo,

Wengine waliokamatwa yumo Meya wa Arusha Kalist Lazaro,mashekh wachungaji ,padri na madiwani Wawili ,mkuu wa shule ya Lucky Vincent na viongozi wa Tamongsco kanda ya kaskazini.

Polisi wanadai ni mkusanyiko usio halali.ni maelekezo ya RC Mrisho Gambo.
Hadi kutoa rambirambi siku hizi mpaka uwe na kibali kweli kazi ipo.!!!
 
Lema wewe tulia kunywa chai ...chukua mshahara ukawasomeshe wanao

Watanzania hawa ni wazito sana kuelewa na wepesi kusahau

Ukijifanya kuwatetea utajiumiza mwenyewe na familia yako

Acha wanyanyasikeeeee...siku wao wakipata akili watajua cha kufanya
 
Kama ni mkutano wa uchochezi ni sawa tu. Meya kaumbuka kwa kudai serikali imekula pesa, sasa wanataka kutumia siasa kufanya maajabu juu ya ajali iliyogusa wengi.

Mlianza mitandaoni kutishia kutumi nguvu kuichafua serikali, hiyo haikubaliki kabisaaaa.

Ni bora muweke sera zenu mbele zijulikane tho hamna, kuliko kudandia majambo kutafutia kiki.

Mengine tuheshimu dola itupe maelezo zaidi.
Huyu ni binadamu?!
 
Back
Top Bottom