ARUSHA: Meya, wamiliki wa shule, paroko na Waandishi, wakamatwa na Polisi Shuleni, wanyimwa dhamana

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,205

Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .

Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .

Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?
pic+shule.png


======

UPDATES: 1

Waandishi waliokamatwa na jeshi la polisi Arusha kwa madai tulihudhuria kikao ambacho hakikua na kibali katika shule ya Luck vincent ambapo shirikisho la wamiliki wa shule binafsi walikuwa wanaendwa kutoa rambirambi. Sisi tulipata taarifa tukaenda kufanya kazi.

1 .Godfrey Thomas -ayo tv

2.King Alphonce Saul Kusaga

3.Filbert Emmanuel -mwananchi

4.Husein Tuta ITV

5.Joseph Ngilisho -Sunrise radio

6.Geofrey Stephen -Radio 5

7.Janeth Mushi -Mtanzania

8.Zephania Ubwani -The Citizen

9.Elihuruma Yohani -mwakilishi wa Tanzania Daima

10.Idd Uwesu - Azam Tv

UPDATES; 2

Waandishi wa habari waliokamatwa Arusha leo katika utoaji wa rambirambi shule ya Lucky Vincent wameachiwa, polisi waliwaambia waliwapa lift tu.

UPDATES: 3

Kaimu RPC wa Arusha Yusuph Ilembo amesema watu wote waliokamatwa leo shuleni Lucky Vincent ni utekelezajiwa wa agizo la RC wa Arusha Mrisho Gambo

UPDATES: 4

Meya wa Arusha, Kalist Lazaro na madiwani wawili wamenyimwa dhamana.

Hapo awali waliambiwa dhamana ipo wazi na kuanza taratibu za kuwadhamini. Huenda kesho wakafikishwa mahakamani wakikabiliwa na kosa la kufanya mkusanyiko bila kibali .

Wanaoshikiliwa wengine ni Inocent Kisanyage ambaye ni Katibu wa Mbunge Lema,diwani wa kata ya Olasiti mh. Alex Martin na diwani wa kata ya Muriet mh. Credo Kifukwe.

tmp_5880-img_20170518_16254278453930-jpg.511134

Waandishi wa habari tukiwa pamoja kutafakari tukio la leo la kukamatwa na kuambiwa tulipewa lift tuu!


WALIOKAMATWA WAKITOA RAMBIRAMBI WAELEZA WALIVYONYANYASWA

UPDATES;
Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.

Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.


Chanzo: Mwananchi
 
Waandishi wa habari jijini Arusha wamekamatwa na Polisi muda huu wakiwa shule ya Lucky Vincent, waandishi hao walikuwa na Meya pamoja na viongozi mbalimbali wa dini shuleni hapo.Waandishi hao wamepelekwa kituo cha polisi.

Habari zaidi zitafuata
Hadi sasa haijajulikana chanzo cha kukamatwa kwao kwani walikuwa kwenye majukumu yao ya kazi pamoja na Meya wa jiji na viongozi wa dini.
 
Back
Top Bottom