Arusha: Kiwanja Kilichouzwa Kifisadi na Madiwani Wa CCM Charudi Mikononi Mwa Umma Chini ya CHADEMA

katika jambo hili ni dhairi madiwani, Mbunge pamoja na Mh Rais wanapaswa kupongezwa sana kwa jitihada zao zilizopelekea kurudishwa kwa Eneo hili lililouzwa kifisadi.

Sote tunajua Adha waliopata wafanya biashara wadogo wadogo kwa kutanga tanga bila kuwa na Eneo maalum.

Sasa naamini utapangwa utaratibu mzuri wa kuwagawia wafanyabiashara wadogo wadogo Eneo hili bila kubaguana na Mh Waziri Mkuu Aliliongelea swala hili Juzi akiwa Arusha.
 
Ile stand ya daladala kilombero mna mpango gani diwani?iboresheni ina vumbi sana.isakafiwe!..
Hapa umelenga Ile stand inalishusha kabisa hadhi ya jiji nimezunguka majiji yote hakuna stand ya jiji iliyokaa kihasarahara kama Ile waiboreshe iwe kama mbezi mwisho au makumbusho kabisa sababu eneo ni kubwa.
 
Ndio mkuu,Arusha haipaswi kua na stand ina vumbi kama hii katikati ya mji.waiboreshe iwe stand ya kisasa,iwe na vituo vya kueleweka,sehemu ya abiria kupumzika,iwe na taa kwa ajili ya ucku,isakafiwe!...diplomatic city kua na stand kama hii ina vumbi hivi mjini kati haifai.
Nanyaro lifikishe sehemu husika hili!...
 
Duh! Mbona umeandika vice versa? Hii ni aibu kwa NANYARO maana kipo katika kata yake. Hiki kiwanja kilikuwa na mgogoro, na mgogoro uliisha mwaka 2014 baada ya baraza la madiwani kuridhia kuuzwa na mnunuzi kuanza kujenga ukuta pale. Taja mnunuzi tujue ni nani kama co kamanda wa CHADEMA

Je 2014 Halmashauri ilikuwa inaongozwa na nani? umesahau mapema hii kuwa waliolimaliza 2014 ni Baraza la ccm?leo 2016 Halmashauri inaongozwa na CHADEMA
 
Kiwanja namba 67 kilichopo eneo la Kilombero kata ya Levolosi,kiliuzwa kifisadi mwaka 2005 na madiwani wa ccm wakati huo.

Mwaka 2007 ccm iliwavua uanachama Madiwani watatu wakiongozwa na aliyekuwa Meya Paul Lota Laizer. kiwanja hiki kilikuwa ajenda ya CHADEMA kuanzia 2010 kwenye kampeni,na tumeendelea kupambana kuhakikisha kuwa kinarudi kwa umma.

Katika jitihada zetu hizo Halimashauri ya CHADEMA iliandika barua kwa Mh Rais ikimwomba Mh Rais atumie mamlaka yake ya sheria afute hatimiliki ya kiwanja hicho kwa kuwa kiliuzwa kifisadi.

Tunashukuru kuwa jitihada zetu zimezaa matunda na Mh Rais amefuta hatimiliki na kiwanja kimerudi mikononi mwana umma wa Arusha.

Sasa ni mali ya Halimashauri ya Jiji la Arusha chini ya CHADEMA

Ephata Nanyaro
 
Je 2014 Halmashauri ilikuwa inaongozwa na nani? umesahau mapema hii kuwa waliolimaliza 2014 ni Baraza la ccm?leo 2016 Halmashauri inaongozwa na CHADEMA
Hongereni tunatambua juhudi zenu ktk kuleta maendeleo mkuu!..achana na hao wanaopinga hawaka Arusha kwanza,sasa diwani mtuboreshee hii stand kuu ya daladala iwe ya kisasa,stand kama hii haifai kua katikati ya mji,iingizeni katika mipango yenu mkuu.
 
Tunashukuru kuona kumbe kuna wanachadema wanayaona mazuri ya Rais Magufuli.!
Katika jitihada zetu hizo Halimashauri ya CHADEMA iliandika barua kwa Mh Rais ikimwomba Mh Rais atumie mamlaka yake ya sheria afute hatimiliki ya kiwanja hicho kwa kuwa kiliuzwa kifisadi.Tunashukuru kuwa jitihada zetu zimezaa matunda na Mh Rais amefuta hatimiliki na kiwanja kimerudi mikononi mwana umma wa Arusha.
Sasa ni mali ya Halimashauri ya Jiji la Arusha
 
Duh! Mbona umeandika vice versa? Hii ni aibu kwa NANYARO maana kipo katika kata yake. Hiki kiwanja kilikuwa na mgogoro, na mgogoro uliisha mwaka 2014 baada ya baraza la madiwani kuridhia kuuzwa na mnunuzi kuanza kujenga ukuta pale. Taja mnunuzi tujue ni nani kama co kamanda wa CHADEMA
hapo ndio inaonyesha vijana wengi wa lumumba kichwani ni peupe pee
 
Hilo la kutajwa jina la aliyenunua hicho kiwanja sijui kwa nini linarukwa,mimi yangu ni hayo tu
 
Madiwani wa CCM waliuza eneo hili wakati wakiendesha Halmashauri na leo aibu kwao.Mtachelewesha haki kwa hilo mtaweza lakini haki itasimama hata baada ya miaka kupita.
 
Back
Top Bottom