Arusha: Kiwanja Kilichouzwa Kifisadi na Madiwani Wa CCM Charudi Mikononi Mwa Umma Chini ya CHADEMA

Ile stand ya daladala kilombero mna mpango gani diwani?iboresheni ina vumbi sana.isakafiwe!..
Unateremka stendi iliyo katikati ya mji lakini utadhani Mtu umetokea Enaboishu kwa miguu.
 
Duh! Mbona umeandika vice versa? Hii ni aibu kwa NANYARO maana kipo katika kata yake. Hiki kiwanja kilikuwa na mgogoro, na mgogoro uliisha mwaka 2014 baada ya baraza la madiwani kuridhia kuuzwa na mnunuzi kuanza kujenga ukuta pale. Taja mnunuzi tujue ni nani kama co kamanda wa CHADEMA
Madiwani wa CCM waliuza eneo hili wakati wakiendesha Halmashauri na leo aibu kwao.Mtachelewesha haki kwa hilo mtaweza lakini haki itasimama hata baada ya miaka kupita.
 
Kiwanja namba 67 kilichopo eneo la Kilombero kata ya Levolosi,kiliuzwa kifisadi mwaka 2005 na madiwani wa ccm wakati huo.Mwaka 2007 ccm iliwavua uanachama Madiwani watatu wakiongozwa na aliyekuwa Meya Paul Lota Laizer.

Kiwanja hiki kilikuwa ajenda ya CHADEMA kuanzia 2010 kwenye kampeni,na tumeendelea kupambana kuhakikisha kuwa kinarudi kwa umma.Katika jitihada zetu hizo Halimashauri ya CHADEMA iliandika barua kwa Mh Rais ikimwomba Mh Rais atumie mamlaka yake ya sheria afute hatimiliki ya kiwanja hicho kwa kuwa kiliuzwa kifisadi.

Tunashukuru kuwa jitihada zetu zimezaa matunda na Mh Rais amefuta hatimiliki na kiwanja kimerudi mikononi mwana umma wa Arusha.
Sasa ni mali ya Halimashauri ya Jiji la Arusha chini ya CHADEMA

EPHATA NANYARO
Diwani-Levolosi
Mikononi mwa umma chini ya Chadema!!! Haiko sahihi maana hata chadema bado ni chama cha kisiasa tu. Nadhani hapakuwa na haja ya kusema mikononi mwa umma chini ya chadema kuonyeshA jidihada zao bali ungesema 'mikononi mwa umma'.
 
Rais amekifuta baada ya chadema kumuandikia barua kuwa kiwanja kiliuzwa kwa ufisadi, hata vile vya kina Sumaye vilikuwa na walakini ndio maana rais alivifuta.Tusiingize siasa kwenye sheria ila tumsifu rais linapokuja swala la ufisadi haangali limefanywa na chama gani.
 
Mikononi mwa umma chini ya Chadema!!! Haiko sahihi maana hata chadema bado ni chama cha kisiasa tu. Nadhani hapakuwa na haja ya kusema mikononi mwa umma chini ya chadema kuonyeshA jidihada zao bali ungesema 'mikononi mwa umma'.
yote yapo sahihi tafuta Kamusi Kijana
 
MEYA WA JIJI LA ARUSHA ACHOCHEA VURUGU ZA MADIWANI NA KUSABABISHA KUVUNJIKA KWA BARAZA MAALUM LA MADIWANI LA TAREHE 18 NOVEMBER 2016


Katika Kikao maalum kujadili vibanda vya maduka zaidi ya 1000 mali ya jiji la Arusha vilivyokodishwa kinyume cha sheria ya manunuzi ya Umma na 7 ya mwaka 2011 ambapo wapangaji wamekuwa wakitoa Shilingi milioni 1 mpaka 3 kwa madiwani hao kama hongo ili wapewe nafasi Na wengine waendelee kufanya biashara katika vibanda hivyo . Kupitia kikao hicho mkurugenzi wa jiji la Arusha bw. Athumani Kihamia aliwaelimisha madiwani hao kutoa maamuzi yanayo zingatia sheria badala ya kutanguliza maslahi yao binafsi hali inayosababisha jiji hilo kutokaukiwa na Migogoro

Kihamia aliweka bayana kuwa sheria ya manunuzi ya Umma inataka ukodishwaji wa mali za serikali ufanywe kwa njia ya ushindani na siyo madiwani kuleta watu na kuwapangisha kinyemela hali inayoshiria harufu ya rushwa .

Kikao hicho kilikuwa mahususi kujadili taarifa ya uchunguzi uliofanywa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha ambaye sasa ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya umiliki na upangishwaji wa vibanda hivyo. Wakati waki endelea na kikao hicho madiwani zaidi ya 25 kati ya 30 waliohudhuria walisimama bila utaratibu na kuanza kupiga makelele ya kupinga ushauri wa kitaalam waliokuwa wakielekezwa na mkurugenzi huyo pamoja na timu yake ya wataalam 18 wanaomsaidia kuendesha jiji hilo akiwemo mwanasheria wa jiji ambaye ni wakili msomi, afisa Manunuzi aliyebobea katika taaluma hiyo na wengineo wa fani mbalimbali .

Mapema julai mwaka huu mkurugenzi huyo alifyeka posho za madiwani walizokuwa wanajilipa kinyume na sheria ikiwemo nauli ya shs 60,000 kwa umbali usiozidi kilometa 5 kwa walio wengi na hatimaye kuzielekeza ktk maeneo yenye kero za wananchi ikiwemo kulipa yaliyokuwa madeni sugu ya walimu.

Kwa sasa madiwani hao wanahaha kila pembe kuhakikisha mkurugenzi huyo anaondolewa katika jiji hilo kisa kikubwa kikiwa ni maslahi yao binafsi hasa posho zisizofuata utaratibu ambapo wameapa kuitisha baraza maalum ili wamjadili na kumkataa mkurugenzi huyo kwa kisingizio cha kwamba amelipa madai yaliyokuwa Kero Kwa walimu. Hao ndiyo madiwani wa jiji la Arusha

Ufike madiwani hawa wajitambue kuwa wapo kwa ajili ya wananchi na siyo kutanguliza matumbo yao mbele na kuwazuga wananchi wakijifanya watetezi wao kumbe walikuwa wanalifanya jiji ni shamba la bibi.


No More Drama Kama mlitegemea mtatokea Jiji sio katika Awamu hii.

Sheria Ya Manunuzi Vs Maslahi Binafsi

Kawaida ya Kinyonga
 
Safi SANA ukawa najua Habari hii watu wa nini saba hawata ifurahia kabisa

OVA
 
Pongezi zinakwenda kwa magufuli aliefuta hati miliki na kuirudisha ardhi manispaa.
Ni kama alivyofuta ardhi ya mabwe pande tu,chadema hapo ni kama matarishi
 
"Kubalansisha story", Waziri mkuu Majaliwa Kassim wakati akiwa ziarani Arusha juzi ametamka kuanza rasmi mchakato wa kuirudisha ardhi hiyo baada ya kuombwa na wananchi wakiongozwa na mbunge wa viti maalumu CCM Ms Magige. Huo ndo uhalisia.
 
Back
Top Bottom