Arusha: Madiwani watatu wa CHADEMA wajiuzulu na kujiunga na CCM

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
16,635
Points
2,000

figganigga

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
16,635 2,000
Madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha watangaza kujiuzulu na kuhamia Chama Chama cha Mapinduzi (CCM). Madiwani hao ni Zacharia Mollel wa kata ya Oloirieni, diwani wa kata ya Themi Melance Kinabo na diwani wa Kata ya Unga Limited James Lyatuu.

====
Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jiji la Arusha wamejiuzulu na kuhamia katika Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa maelezo kuwa wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jiji la Arusha wamejiuzulu na kuhamia katika Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa maelezo kuwa wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Madiwani hao ni pamoja na Welance Kinabo (Themi), Zakaria Mollel (Oloirien), na James Lyatuu (Unga Limited). Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dk. Maulid Madeni amethibitisha kupokea barua za madiwani hao kujiuzulu.

“Nimepokea barua zao nitatoa taarifa baaadaye,” amesema Madeni.

Hivi karibuni aliyekuwa Meya wa jiji hilo, Kalist Lazaro alijiuzulu na kujiunga na CCM. Katika uchaguzi mkuu wa 2015, Chadema kilikuwa na madiwani 25 na CCM mmoja, lakini kutokana na baadhi ya madiwani kuhamia chama hicho tawala kimekuwa na madiwani nane hadi sasa na Chadema kubakia 15.
 

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
11,188
Points
2,000

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
11,188 2,000
... duh! Hatari sana; Chadema Arusha si itakuwa imesambaratika rasmi? Ni diwani gani wa upinzani aliyebaki Arusha?
 

Benny Haraba

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Messages
5,104
Points
2,000

Benny Haraba

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2012
5,104 2,000
Madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha watangaza kujiuzulu na kuhamia Chama Chama cha Mapinduzi (CCM). Madiwani hao ni Zacharia Mollel wa kata ya Oloirieni, diwani wa kata ya Themi Melance Kinabo na diwani wa Kata ya Unga Limited James Lyatuu.
Asante kwa taarifa
 

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
82,688
Points
2,000

Mmawia

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
82,688 2,000
Tuwapongeze sana kwa kusoma alama za nyakati na kuamua kupambania matumbo yao badala ya kuwapigania wananchi walio wachagua.
Madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha watangaza kujiuzulu na kuhamia Chama Chama cha Mapinduzi (CCM). Madiwani hao ni Zacharia Mollel wa kata ya Oloirieni, diwani wa kata ya Themi Melance Kinabo na diwani wa Kata ya Unga Limited James Lyatuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
7,309
Points
2,000

Crimea

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2014
7,309 2,000
Kipindi cha JK tulikuwa tunaambiwa na machadema kwamba Kaskazini ikiwemo Arusha hakuna wachumia tumbo na kwamba kule watu wana msimamo!

Wakawa wanajigamba kwamba hata Kikwete akienda wanaweza kumfukuza
Lakini Lema kapigwa ndani makamanda yakawa yanachungulia tu kwa mbali kwa uoga yasijue la kufanya.
Nawauliza makamanda wa mikoa hiyo msimamo mmepelaka wapi?

Mbwembwe nyingi kumbe mko kama mrenda tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Messages
1,773
Points
2,000

kindikwili

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2016
1,773 2,000
Kuna clip nimekutana nayo inayoonesha madiwani 3 wafuatao wa jiji la Arusha CDM wakitangazia umma kuwa wanajiuzulu udiwani na kuachana na uanachama wa CHADEMA kisha kujiunga na CCM. Walifanya hivyo jana kwa mujibu wa clip hiyo.
Zacharia A. Molel diwani wa Oloirieni
James M Lyatuu diwani wa Unga limited
Melance E Kinabo kata ya Themi
Kisanyage Innocent Katibu wa CHADEMA jiji la Arusha

Kinabo anasema "nimejiuluzu kwasbabu sioni future ya chadema kwenye upande wa kuleta maendeleo kwenye jiji la Arusha na Tanzania kwa ujumla. Lakini pia nimpongeze mkurugenzi wa jiji la Arusha Mr . Madeni kwa kazi kubwa anayoifanya bila ubaguzi wa vyama ndani ya jiji la Arusha"

Zacharia Molel " Kwa hiari yangu mwenyewe nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya udiwani na kujiunga na ccm , sababu ni moja tu kuongeza wigo na fursa ndani ya kata yangu na pia ni kuona jinsi mheshimiwa rais anavyofanya kazi ya maendeleo ndani ya nchi yetu , lakini pia mkurugenzi wetu ambaye amekuwa akishirikiana pamoja na sisi ndani ya jiji la Arusha na kuweza kufanya kazi zinazoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu kwahiyo nikaona sitakuwa na uzalendo kuendelea ndani ya chadema kwasababu sioni nini kinafanyika huko hayo yanayofanyika huko ni malumbano na majungu mengi hivyo nikaona nichukue fursa hii kujiunga na wanaoleta maendeleo"

James Lyatuu "bila kushawishiwa au kufosiwa na mtu yeyote nimeamua kujiuzulu udiwani na nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo cdm ili niweze kuunga juhudi za maendelo yanayofanywa na rais kuleta maendeleo makubwa ambayo tunayaona kujenga madaraja makubwa, kununua ndege amefanya maendeleo makubwa hata kwenye kata yangu amefanya. Tunapitisha bomba la maji taka , bado tunakuja tunatengeneza barabara ya lami pamoja na hayo leo nimehakikisha inaingia kwenye budget ya 2020/2021 ujenzi wa shule ya secondary eneo la mwembeni na mkurugenzi Dk Madeni amenihakikishia kwamba pale tutajenga sekondary ya kiwango cha juu sana cha gorofa. nimetoka kwenye kikao cha mwisho cha baraza la madiwani kitakachotekelezwa 2020/2021 wale ambao walikuwa wananiunga mkono cdm na wale ambao walikuwa waniona adui wao (ccm) sasa wanichukulie kama ndugu zao, ccm nguvu moja lakini pamoja na hayo nimetazama future kwenye chama changu, sioni future kwenye chama changu"

Kisanyagi anasema "nilikuwa katibu wa cdm Arusha mjini najiuzulu kwa ridhaa yangu uongozi ndani ya chama na uanachama ndani ya cdm , naunga mkono jitihada za rais wa JMT kwa haya yanayofanyika kupeleka nchi kwenye uchumi wa kati wa viwanda na miradi mikubwa ya maendeleo itakayokuwa na faida kwa siku za usoni . Nimeamuakujitoa chadema kwasababu hakiyafanyi yale wanayoamini na kimepoteza muelekeo"

MAONI YANGU
1. Nampongeza sana Mkurugenzi wa jiji la Arusha (usiniulize kwanini)
2. Chadema poleni sana najua mnapitia maumivu makali kupoteza kizembe jimbo na kata mlizozipata kwa jasho na damu
3. Kama kweli madiwani hawa wamejiuzulu kwa hiari yao basi bado tuna kazi kubwa sana ya kufanya kuleta uelewa juu ya kazi na majukumu ya upinzani
4. Madiwani wanapswa kupewa semina juu ya kazi zao ,kazi ya upinzani kwa ujumla na kazi ya serikali pamoja na chama tawala.

Kindi
3.
 

Forum statistics

Threads 1,391,862
Members 528,498
Posts 34,092,309
Top