Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,162
- 3,162
Ni dhahiri kuwa Arusha ni mkoa wa kitalii Tanzania, kwa vivutio vilivyopo Arusha bila shaka Africa nzima hakuna jiji lenye vivutio vingi kama Arusha. Arusha ina vivutio vifuatavyo kwa ukaribu; Tarangire, Lake Manyara, Arusha National Park, Ngorongoro na Serengeti, Oldonyo Lengai, Olvai Godge nk, lakini Arusha ina utajiri wa makabila yaliyotunza utamaduni ambao ni kivutio cha utalii wakiwemo Wamasai, Wabarbaig, Wahadzabe nk
Hadi mwaka 2010 Arusha haikuwa na hadhi kuwa mkoa unaopokea watalii kutoka kila kona ya dunia, ingawa hadi sasa bado hairidhishi lakini angalau vumbi limetoweka. Arusha mitaa ilikuwa vumbi, huduma ya maji ilikuwa ya shida. Sababu kubwa ya kuifanya Arusha iwe vibaya kimiundombinu ni kutokana na genge la wana CCM ambao wakati ule walikuwa wamekamata Halmashauri, kuanzia Mbunge hadi madiwani.
Mwaka 2011 baada ya upepo kugeuka na kuingia CHADEMA wakiongozwa na Mbunge Godbless Lema, Arusha ilishuhudia ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu na kufanya angalau mitaa mingi kuwa na kiwango cha lami. Lakini ilishuhudiwa usambazaji wa maji wa kasi zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika, uwepo wa CHADEMA ndani ya Halmashauri uliwafanya wezi waliokuwa wamejificha kwenye mwavuli wa CCM kupoteana, hivyo kusababisha mapato yatumike kwa usahihi.
Hivyo, itakuwa ni kosa kubwa kwa wana Arusha kuirudisha Arusha mikononi mwa CCM tena, ni vyema kuisoma historia kabla ya kufanya maamuzi.