CCM Arusha yawapokea Madiwani wa CHADEMA

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Hatimaye Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Arusha mjini kimewapokea wanachama wapya ,waliokuwa madiwani wa chadema akiweno katibu wa wilaya waliokihama chama chao na kujiunga na CCM.

Mwenyekiti wa ccm wilaya hiyo Joseph Masawe amewapokea wanachama hao wapya kwenye ofisi za chama hicho.

Na kusema kuwa hawajachelewa wamerudi wakati muafaka wa uchaguzi mkuu ambao wanahitaji ongezeko la wanachama.

" Leo tunayofuraha kuwapokea waliokuwa madiwani wa chadema,Melance Kinabo wa kata ya Them,Zacharia Mollel wa Olerieni ,James Lyatuu wa Kata ya Ungalimitedi pamoja na katibu wao wa wilaya Innocent Kisanyage,kikubwa naomba fuateni taratibu za chama na tunawakaribisha sana kujenga chama zaidi,"alisema Masawe.

Katibu wa Chama cha CCM Wilaya ya Arusha Denis Zakaria alisema chama chao bado hakijafunga milango ya kupokea wapinzani kwani bado wanahitaji wanachama wengi zaidi.

Alisema ujio wa viongozi wa Chadema unaashiria wengi wao kukubali kazi zinazofanywa na Rais John Magufuli za maendeleo.

Kwa upande wa madiwani hao wakiongozwa na aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Innocent Kisanyage alisema ametoka Chadema sababu ya kupinga kila kitu na wakati yeye anaona kazi zinazofanyika.

Diwani wa Kata ya Zakaria Mollel (Olorieni) alisema amejiunga CCM ili ashirikiane naye Rais John Magufuli kufanya kazi za maendeleo katika kata yake.

"Lakini wale wanaofikiri nimekuja CCM nimehongwa waongo maana mimi mfanyabiashara hakuna wa kunihonga na Chadema nilitumia fedha zangu nyongi kujenga chama,"alisema.

Diwani Kata ya Themi Melace Kinabo alisema ametoka Chadema kwa sababu ya kupata vikwazo vya kimaendeleo.

"Chadema kuna siasa za kutotenda na mimi nimekuja huku namwomba Mtakatifu Joseph chama changu kanisani aniombee ili nikaungane na Rais kuleta maendeleo ya kasi ya chama changu,"alisema.

Diwani wa Kata ya Unga Limited James Lyatuu alishukuru kupokelewa CCM na ataungana nao kuiepeleka nchi kwenye uchumi wa kati.

IMG-20200203-WA0018.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni utani nyie madiwani, msitake kudanganya watu, hii sababu ya kukimbilia CCM kuunga juhudi mui-modify, kwanini hizo juhudi msiende kuziongeza kwenye vyama vingine vya upinzani?, semeni tu mmeenda CCM mambo yenu yawe safi.

Mkumbuke mlipewa udiwani na wapiga kura, sasa ni vizuri kama mna hakika mmehama na hao wananchi, vinginevyo kama mnaamini nguvu ya dola zaidi ya nguvu ya wapiga kura, poleni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom