Arusha: Hekari 101 na Magunia 482 za Bangi zateketezwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya imeteketeza jumla ya hekari 101 za mashamba ya bangi sawa na kiasi ya kilo 550 za bangi mbichi pamoja na magunia 482 ya aina hiyo ya dawa za kulevya katika eneo la Kisimiri juu kata ya Uwalu, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Ukamataji huo umefanyika kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya operesheni nchi nzima ili kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa Nchini.

Akizungumza operesheni hiyo, iliyofanyika mkoani humo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama itaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo haya ili kuhakikisha bangi inatokomea kabisa mkoani humo na hatimaye wakulima na wananchi kwa ujumla wanaoishi katika eneo ya kisimiri juu na chini wanaachana na kilimo cha bangi na kujikita katika mazao mengine ya biashara badala ya bangi.

Kamishna Lyimo amesema kuwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) katika kuhakikisha agizo la Mheshimiwa Rais ilinatekelezwa, ameelekeza kufanyika kwa utafiti kujua ni mazao gani mbadala yanaweza kulimwa katika maeneo haya ambayo yamekithili kwa kilimo cha dawa za kulevya, ili wananchi wa maeneo husika waweze kupewa mbinu mbadala za kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara badala ya kuendelea na kilimo cha bangi. ‘‘Tumewasiliana na Wizara ya Kilimo na Afisa kilimo wa kata ya Uwalu hapa kisimiri ambaye ameeleza tayari utafiti huo umefanyika.

Aidha, Kamishna Lyimo amesema, elimu juu ya athari za biashara na matumizi ya dawa za kulevya itatolewa kupitia shule za msingi na sekondari. Hii inafanyika kufuatia agizo la Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) kuitaka Mamlaka kushirikiana na wadau kutoa elimu katika maeno hayo. Ambapo tayari maafisa elimu Kata wameanza kutoa elimu kwa wanafunzi, ili baadaye wasijihusishe na kilimo cha bangi na mirungi badala yake wajikite kwenye mazao mengine.

Katika kuhakikisha maagizo ya Waziri Mkuu yanatekelezwa, Afisa kilimo Kata ya Uwelu, Samwel Parangyo, amesema kuwa, utafiti uliofanywa na Wizara ya Kilimo kupitia kituo cha utafiti wa kilimo cha TARI Tenguru, imebaini kuwa yapo mazao yanayostawi katika maeneo hayo kama vile pareto, karoti na viazi mviringo na kuwa mbadala wa zao haramu la bangi ambalo halifai katika jamii yatu. Ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kwa kutoa ruzuku ya mazao hayo.

Operesheni hii imefanyika ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) kutoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2022 ambapo katika taarifa hiyo alitaaja mikoa inayojihusisha na kilimo cha Bangi kwa kiasi kikubwa, Mkoa wa Arusha Ukiwa kinara ukifuatiwa na Mikoa na Iringa, Morogoro na Manyara.
IMG-20230601-WA0018.jpg
IMG-20230601-WA0015.jpg
IMG-20230601-WA0017.jpg
IMG-20230601-WA0014.jpg
IMG-20230601-WA0012.jpg
IMG-20230601-WA0009.jpg
IMG-20230601-WA0011.jpg
 
Ni Aibu sana.

Tunatiana umasikini
. Tunapoteza Mbegu Asilia.

Tunapoteza Nguvu za Rasilimali watu.

Kulima bangi sio lele mama hata kidogo.

Madawa ya kulevya yanayouwa utamaduni mila na desturi zetu zimetapakaa na hatuoni chochote kinachofanywa.

Hapana, Hapana kutiana umasikini.

Walima bangi watetewe.
 
Wachomaji wenyewe ni wavutaji yan unachoma bila kuvaa kuvaa chochote cha kuzuia usivute Moshi? Waache kutuona sisi wajinga
 
Ningekuwepo hapo ningezuga tu upande wa moshi unapoelekea.

Anga la Arusha limepata neema. Huo moshi mtakatifu utaenda kurutubisha na watu kupata mvua za kutosha na kilimo kunawiri na mavuno ya kutosha.
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya imeteketeza jumla ya hekari 101 za mashamba ya bangi sawa na kiasi ya kilo 550 za bangi mbichi pamoja na magunia 482 ya aina hiyo ya dawa za kulevya katika eneo la Kisimiri juu kata ya Uwalu, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Ukamataji huo umefanyika kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya operesheni nchi nzima ili kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa Nchini.

Akizungumza operesheni hiyo, ilianza tarehe 31 Mei, 2023 mkoani humo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Usalama itaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika maeneo haya ili kuhakikisha bangi inatokomea kabisa mkoani humo na hatimaye wakulima na wananchi kwa ujumla wanaoishi katika eneo ya kisimiri juu na chini wanaachana na kilimo cha bangi na kujikita katika mazao mengine ya biashara badala ya bangi.

Kamishna Lyimo amesema kuwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) katika kuhakikisha agizo la Mheshimiwa Rais ilinatekelezwa, ameelekeza kufanyika kwa utafiti kujua ni mazao gani mbadala yanaweza kulimwa katika maeneo haya ambayo yamekithili kwa kilimo cha dawa za kulevya, ili wananchi wa maeneo husika waweze kupewa mbinu mbadala za kulima mazao mbalimbali ya chakula na biashara badala ya kuendelea na kilimo cha bangi. ‘‘Tumewasiliana na Wizara ya Kilimo na Afisa kilimo wa kata ya Uwalu hapa kisimiri ambaye ameeleza tayari utafiti huo umefanyika.

Aidha, katika kuhakikisha wananchi wanoishi katika maeneo yaliyokithiri kwa kilimo cha dawa za kulevya hususani bangi na mirungi, wanapata elimu juu ya athari za biashara na matumizi ya dawa hizo, elimu juu ya tatizo hilo itatolewa kupitia shule za msingi na sekondari.

Hii inafanyika kufuatia agizo la Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) kuitaka Mamlaka kushirikiana na wadau kutoa elimu katika maeno hayo. Ambapo tayari maafisa elimu Kata wameanza kutoa elimu kwa wanafunzi, ili baadaye wasijihusishe na kilimo cha bangi na mirungi badala yake wajikite kwenye mazao mengine.

Operesheni hii imefanyika ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) kutoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2022 ambapo katika taarifa hiyo alitaaja mikoa inayojihusisha na kilimo cha Bangi kwa kiasi kikubwa, Mkoa wa Arusha Ukiwa kinara ukifuatiwa na Mikoa na Iringa, Morogoro na Manyara.
 
Wanamsingizia Rais.
Raisi hakuwatuma kwenda kuangamiza Bangi.
Raisi hakuwaagiza kwenda kuwafanya Watanzania masikini.

Mbona hationi makilo ya Cocaine? Mbona hatuoni Heroin? Mbona hatuoni madawa mengine yakipigwa moto?

Huo ni Ulimbukeni, hayo magunia na hayo mashamba yakipigiwa hesabu, siajabu yakatosha kulipia matungi ya gesi tosha kwa wananchi.

Tumedumazwa na Sheria za Kikoloni na za Ukimbari. Tunatiana umasikini!
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya imeteketeza jumla ya hekari 101 za mashamba ya bangi sawa na kiasi ya kilo 550 za bangi mbichi pamoja na magunia 482 ya aina...
Hivi wilaya ya Arumeru kuna kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya Kweli ?

Kama wapo wanalinda nini?

Cha kufurahisha zaidi, Kisimiri juu kata ya Uwalu vijiji vyote vinaongozwa na viongozi wa ccm na Serikali ya ccm!!!!
 
watu wanahangaika na mambo yasiyo ya maana , kuna mbunge aliwahi kusema bungeni bangi iruhusiwe wakamshambuliaaaaaaaa, alimaanisha waruhusu watu walime kwa mpango na itumike kuuza nje kwa wanaotengeneza dawa mbali mbali. Watu wanajua kazi yake ni kuvuta tu , mwenzenu Mike Tyson sasa ana hekari kama 40 hivi za huo mmea na ni tajiri wa kutupwa kwa ajili hiyo tu, nyie endeleeni na ngonjera zenu za ooh eti dawa ya kulevya , wakati huko mnakoomba misaada wao ndio wanatumia kwenye mambo yao ya matibabu na dawa.
 
Back
Top Bottom