Ni Ujinga kumind hali ya kua wewe ni mtanzania, Hata Ulimwenguni wakiisifia Arusha basi ujue wameisifia Tz.
Halikadhalika pia ni ujinga kuponda kwa hoja za kijingajinga, pia ni ujinga kusifia ati kwa sababu umezaliwa pale au kwa sababu wewe/baba/babu yako anakijishamba cha robo eka pale Kisongo_Na_mwanya. Wote wanaoangukia kundi hilo ni wajinga/wapumbavu,
Ila ni vyema kuisifia mandhari ya jiji la Arusha kama mfano wa kuigwa kwa majiji mengine ndani ya nchi mf. mwanza, Mbeya n.k.
Pia ni bora Zaidi na Ufahari mkubwa kwa Mtanzania yyt yule bila kujali anatokea wapi kujinadi na kuisifia Arusha kwa wakazi wa nchi nyingine za East Africa mfano Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi n.k
Nadhani hapo ndio kwenye Hoja ya msingi na ndio maana wanaonadi kua Tz tunautajiri mkubwa wa Gas hawatokei Mtwara tuu peke yake bali hutoka sehem mbali mbali ya nchi.
The issue ni kua wasifiaji wanahusisha maendeleo ya Arusha na Majority Ethnic groups living there interms of Tribes/Religion ndio maana wapingaji nao wanaponda kwa hoja za kijingajinga kama hizo zitolewazo na wasifiaji mf Arusha si lolote si chochote, Hamna dili ninyi wakaskazini wabaguzi tuu.
Kwa hoja za namna hii ya kusifia Uzuri wa Arusha ati ndipo bora Zaidi kuliko kwengine na uzuri huo umetokana na wakaazi wa Arusha basi hata watu wa Dar kesho watajisifia ya kua Nyumbani kwao ndipo panaongoza kwa kutoa pato kubwa kwa Taifa letu/ watu wa Dodoma nao watasema kwao ndio mji mkuu wa nchi/watu wa Moshi watasema wao ndio wasafi kuliko watanzania wote na mwisho maswala mazima ya Ukabila, Udini na Ukanda ndipo yatashika kasi nchini kwetu.
Huu ni ukaburu na ni Ubaguzi wa watu wenye fikra fupi wanaotaka kutumia Natural Endowements kujinadi kua ni matakwa ya uweledi wao ktk namna moja au nyingine ndio maana miji yao imekua bora kuliko mingine.
Thx