Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Havertz, saka msimamo wangu ni ule ule. .... kapunguzwa martinelli..
Hawa ni matapeli.

Huyu kai anachofanya ni utumbo
Hiki kitu nimewahi kuzungumza kwenye jukwaa hili lenu mnawachezaji wengi wa kawaida ambao ukiwatoa Rice, Raya labda na Saliba ambapo wakienda Chelsea au Man City wanakula benchi ila Sasa Castr anavyowapaisha Hana tofauti na mashabiki wa manyumbu utofauti uko wapi ni kwasababu ya mfumo wa Arteta unafanya wanaonekana wapo kwasababu ya ile team work.
 
Kwenye hii mechi Aston villa hawana shot on target ingawa Arsenal tumecheza hovyo sana.

Hii sasa ndiyo hiyo fear factor
Msimu huu Aston villa wabovu kumbuka wamepigwa 4 bila na Brighton wameuza wachezaji wao bora
 
Mfumo wa Arteta.

So leo unakubali kwamba Arteta ni kocha mzuri kiwango cha dunia?

Timu inayotaka matokeo ikipigwa low block lazima istruggle. Nyinyi pia hiyo Jumapili mkicheza low block mtatusumbua ila kufungwa ni palepale
 
Msimu huu Aston villa wabovu kumbuka wamepigwa 4 bila na Brighton wameuza wachezaji wao bora
Tangu Emery aende Villa wamekua wanacheza jihad wakikutana na sisi.

Kwani hizo nne walizopigwa na Brighton walipaki basi? Unadhani nyinyi mtajiachia mkikutana na Arsenal?
 
Through ball aliyopiga Bruno kwa Kai jana ni weakness iliyokuepo game ya jana pamoja na kutopiga long balls.
 
Niliwaambia humu jukwaani lenu wakati mnataka kumsajili Gyrokerez nikasema huu ni Usajili wa mihemko usiozingatia matakwa ya mfumo wenu wa uchezaji, Victor Gyrokerez ni bonge la mchezaji na analijua goal lakini hafit mfumo wa Arteta, Mfumo wa Arteta hatuhitaji target Man kama Gyrokerez unahitaji mshambuliaji anayenyumbulika akai kwenye eneo moja mara nyingi ili kutoa space kwa wachezaji wengine wapembeni kuingia ndani ndio maana anampenda sana Kai Swali nilikuwa najiuliza ilikuwaje Arteta akamsajili wakati unajua hafit mfumo wako wa uchezaji?
 
Umeacha statistics uchwara umeamua tuongee mpira?

Siyo mbali, ni Jumapili.
Takwimu ni sehemu ya mpira nawaonea huruma sana kwa kweli mnaenda kukutana na ile front three alafu wanakasi wale halafu hawana utani na goal
 
Tangu Emery aende Villa wamekua wanacheza jihad wakikutana na sisi.

Kwani hizo nne walizopigwa na Brighton walipaki basi? Unadhani nyinyi mtajiachia mkikutana na Arsenal?
Hata sisi Fulham walicheza jihad na wakala 3 takatifu na Fulham ina watu haswa huwezi kufananisha na Aston villa kucheza jihad ni jambo moja kuwa na watu wenye quality ya kucheza hivyo ni jambo lingine
 
Hata mwaka jana mlisema hivyo hivyo.
Msimu uliopita tulikuwa na changamoto nyingi ndio maana hatukuwa na hayo matarajio Sanchez alitukosesha amani kwa kugawa point kwa wapinzani, wachezaji wetu Bora Cole Palmer na Colwil walivyoumia ndio msimu wetu uliishia hapo safari hii kila idara imetimia hata Palmer akiumia tuna Rogers balaa ni lile lile, Tuna Kipa mwenye ubora tunachokifanya Sasa kutafuta balance nzuri kwenye safu ya beki maana tuna mabeki wazuri individually.
 
Bado mnaruhusu magoli mengi, ngoja tuone hadi mechi ya tano ndipo tuzungumzie vizuri. Kwa sasa dalili zote zinaonesha kuwa timu yenu inafungika kirahisi sana.
 
Mfumo wa Arteta.

So leo unakubali kwamba Arteta ni kocha mzuri kiwango cha dunia?

Timu inayotaka matokeo ikipigwa low block lazima istruggle. Nyinyi pia hiyo Jumapili mkicheza low block mtatusumbua ila kufungwa ni palepale
Mimi Sina ushabiki wa kijinga kwenye ukweli nasema sijawahi kusema Arteta mbaya labda mashabiki wa manyumbu Arteta ni bonge la kocha hii team yenu angekuwa kocha wenu ni Enzo Maresca mngekuwa mnatafuta nafasi ya kugombea ligi ndogo ya mabingwa( Europa league) hata angekuwa ni Guardiola msingechukua ligi.
 
Bado mnaruhusu magoli mengi, ngoja tuone hadi mechi ya tano ndipo tuzungumzie vizuri. Kwa sasa dalili zote zinaonesha kuwa timu yenu inafungika kirahisi sana.
Ndio maana Alonso akasema kuanzia December tutakuwa hatushikiki kwa maana hiyo anatafuta namna nzuri itakayofanya defensively tuwe Bora ila kule mbele tupo moto na huko ndipo panatupa matokeo
 
Ndio maana Alonso akasema kuanzia December tutakuwa hatushikiki kwa maana hiyo anatafuta namna nzuri itakayofanya defensively tuwe Bora ila kule mbele tupo moto na huko ndipo panatupa matokeo
Ni kweli, lakini huku mwanzoni msipojikaza ndo manatuachia ubingwa mapema sana.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…