Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Wajinga wengi sana mkuu.
 
Wachambuzi wengi wa bongo hawajui kuchambua soka la Ulaya huwa wanachambua kwa mapenzi na mihemko.Mimi nilijua matokeo kabisa yatakuaje na ndio maana haujaniona humu kuwaponda. Nyinyi tayari mna team mlichofanya ni kuongezea baadhi ya wachezaji kwenye nafasi ukiangalia msimu uliopita Man city walikuwa kwenye Decline stage msimu uliopita ni vile ubovu wa team nyingine ambao walikuwa kwenye Hali mbaya zaidi kama Liverpool, Man u na Chelsea ndio imefanya washike nafasi ya Pili na uzembe wenu mlioonesha kwenye baadhi ya mechi.Ukiacha kuwa kwenye Decline stage msimu uliopita ukichanganya na ujio mpya wa kocha Enzo Maresca na kutofanya maboresho how comes team hii unaipa nafasi eti imemfunge Arsenal???
 
Tukutane GW3 jomba tumalize huu utata
 
hao wachezaji uliowataja watasumbuliwa na fitness. Mungu asaidie wasirud tena kwenye majerui

Unasema una wachezaji wenye ubora kuliko team yoyote epl, mkuu mimi naomba nitajie wachezaji 5 wanaoingia first eleven ya arsenal. Kuna 10,000 ya maji
 
mpira wa sasa ni coach vs coach na sio tena wachezaji dhidi ya wachezaji ,pep ndie aliekuwa mpinzani mkuu wa arteta.. kuondoka kwake kutamrahisishia arteta kwenye utawala wa soka la uingereza.

kuna baadhi ya makocha waliobakia.. wanaweza kumpa changamoto arteta ambao ni kocha wa brighton ,kocha wa liverpool ,kocha wa man utd na kocha wa villa.
 
Spurs simsemei sana kocha wao mzuri unayemtaja hapa alikua Brighton, akafananishwa na Arteta, kilichofuata tunakijua.

Kwa kawaida timu ikiwa na beki mbovu mchezo wao hua ni kujitahidi kufunga sana, refer kwa Barcelona, itashinda 5 - 3, au 4 - 3.

Nyinyi shida haikua defense, shida ni mpaka kwa forward. Enzo alikua AM sijui ni mechi zipi Pedro akawa AM badala ya Enzo. Juzi nimeona mashabiki wa Chelsea wanauliza "Ni muda umefika tukubali ukweli Palmer ni one season wonder?"

It's nice kwamba miongoni mwenu mnajiuliza mumchukulieje huyo jamaa.

Arsenal, tushakutana na Chelsea ambayo mashabiki mliita strong na Arsenal tukakubali kwamba kweli hii ni strong. Ilikua ni first game na lukaku yumo, mna kocha experienced, Tuchel. Nyinyi hamtakua na kikosi kama kile kwa hivi karibuni.

Labda mgombee top six, ila kwamba ndiyo mchukue kombe siyo leo
 
Arteta anasema timu ipo kwenye phase ambayo sasa ataacha wachezaji waamue uwanjani kwa 70% na yeye ukocha utashuka mpaka 30%.

Means individual brilliance sasa ndiyo itaanza kufanya kazi zaidi tofauti na mwanzo ambapo timu iliendeshwa 100% kwa mbinu za kocha tu.
 
Kuna rumors ziliwahi kuja kwamba Arsenal tunamtaka Tammy Abraham nikasema badala ya kumnunua Tammy ni bora tumvumilie Nketiah.

Mimi ni miongoni mwa niliosema kumnunua Madueke ilikua ni miyeyusho, na haikuhusiana na kiwango chake, ilihusiana na fact kwamba anatokea Chelsea.

Msimu huu kuna page ilisema tumeshasajili mchezaji atayekuja kuperform, Tzolis, tushasaini beki bado usajili mmoja kutoka chelsea wa kuwagawa mashabiki, ni kama vile imekua ni tambiko kwamba lazima asajiliwe mtu kutoka chelsea.

Sasa leo unamuachia Nwaneri sehemu ambayo angeweza develop umemuweka Madueke.
 
hao wachezaji uliowataja watasumbuliwa na fitness. Mungu asaidie wasirud tena kwenye majerui

Unasema una wachezaji wenye ubora kuliko team yoyote epl, mkuu mimi naomba nitajie wachezaji 5 wanaoingia first eleven ya arsenal. Kuna 10,000 ya maji
Reece James, Moi Caicedo, Joao Pedro, Cole Palmer na Colwil
 
Cole Palmer alishaset standard ya juu tayari msimu wake mbovu ni wa msimu uliopita ambao kakosa mechi nyingi plus injury za mara kwa mara ndio kafunga goals 11 na Assist 3 kuwa mkweli hii takwimu kwa mchezaji mwingine kwake ndio best. Msimu wake wa Kwanza 2023/2024 kafunga goals 25 assist 15, msimu wake wa pili 2024/2025 kafunga goals 18 assist 14. Nakuja kwenye suala la Joao Pedro wewe umemuona kwenye hizi mechi za kumaliza msimu ndio kaanza kama no 9 ila nyingi hasa msimu wa Kwanza kaanza kama no 10 hasa tukicheza na team ndogo huwa Enzo anacheza no 8 sio 10.
 
Nafikiri kama ikitokea tutamwachia Nwaneri aende ni kwa sababu huenda tunaona tuna Max Dowman ambaye anaweza kucheza nafasi yake na kwa sababu Dowman naye bado ni mdogo, anaweza kuvumilia kukaa benchi kuliko Nwaneri.

Pia Nwaneri anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji wachache ambao wanaweza kuingiza pesa kubwa kuliko wachezaji kama Vieira au Nelson, ambao wanalipwa mishahara mikubwa na wanakuwaga majeruhi sana, hivyo timu zinaogopa kuwachukua.
 
Ndio maana huwa nashangaa jesus kuwekwa bench halibaina ya uchezaji wake ndio unaendana na arsenal..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…