Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tumeshatoa gundu
Tumefungulia koki

Mbona EPL naenda kuionea huruma sana
IMG-20260525-WA0010.jpg
 
Yaani timu imebeba ubingwa haijatoa mchezaji bora wala mfungaji bora, ubingwa wa kiboya kuwahi kutokea.

View attachment 3594196
Hii ni AI hii, sisi huwa ndiyo tunaadhibiwa na VAR kuliko timu yoyote, ila msimu huu tumetendewa haki kidogo zaidi ya misimu iliyopita. Pia ni kwamba tu ile moja ya West Ham kumkwida kipa wetu imetusaidia kupata ushindi badala ya sare na hatimae tukapata ubingwa, na hata hivyo uamuzi ule ulikuwa wa haki kabisa. Tena hapo wachezaji na Arteta walilalamika sana mpaka VAR wakaingilia. La sivyo ingekula kwetu tena.
 
Arsenal wame onyesha nia ya kumsaini Morgan Rodgers, ofa ya m80 ina hitajika
Bei mbaya kinoma na kina ManU nao watataka kutoa 100m.
Nataka tusubiri kombe la dunia tucheki viSouth Americans vipambanaji mifano kama ya Alexis Sanchez na Cavani enzi wakiwa wamoto tuvichukue kwa bei za kishikaji zaidi.
 
Toeni pesa kenge nyie, ubahili wenu ndio uliowafanya mkasota miongo miwili bila kubeba kombe la maana, mlivyoamua kuvunja kibubu mkamsajili Ubwabwa bila mchuzi na huyo Kokores imewalipa, hao wachezaji wenu wa eftatu tatu waliwachelewesha sana mbuzi katoliki nyie.
 
Mmevunja rekodi nyingine ya kuchukua ubingwa ila hamjatoa mchezaji bora wa ligi sababu ya magoli ya kona wadau. Big Up
Arsenyau wamehangaika zaidi ya miongo miwili na pira biriani lakini walikua wanaangukia pua, Tetea Kiwigi alivyoamua kutwist kwenye Haram Football walau imemlipa, ila pia ubingwa wao umetokana na fomu mbovu ya Man City, Liverpool, Chelkenge na Man Utd bila kusahau masaada mkubwa wa VAR.
 
Tafuta Pain killer tukununulie mkuu, tunajua una maumivu.
 
Toeni pesa kenge nyie, ubahili wenu ndio uliowafanya mkasota miongo miwili bila kubeba kombe la maana, mlivyoamua kuvunja kibubu mkamsajili Ubwabwa bila mchuzi na huyo Kokores imewalipa, hao wachezaji wenu wa eftatu tatu waliwachelewesha sana mbuzi katoliki nyie.
Umesahau madhara ya kina Captain Marvelous na Saint Anne na kocha wao bingwa ambaye sasa wanamwita Kichwa Mviringo jinsi wenge la kuwa na pesa lilivyowaponza wakaanza kununua wachezaji wa bei mbaya wakawajaza pale bandani mwao?

Yaani walikuwa kama mfanyakazi mlevi akishashika mshahara. Breki ya kwanza bar.

Kila mchezaji wakisikia mzuri au Arsenal na Manyumbu wanamtaka basi wanaruka naye.

Ekitike, wao. Kerkez, wao. Isak, wao. Frimong, wao. Yaani ilikuwa timu ingine ikumuangalia tu mchezaji flani majogoo wanaruka naye.

Mwishowe wameambulia UCL kwa bahati.

Haya mambo ni ya kutumia akili siyo kumwaga tu mihela.

Hata nyie si mnakumbuka mlivyomwaga mshiko kwa akina Pogba na Lukaku halafu mwisho wa siku mkiaishia kuchekwa mtaani?
 
Chelkenge nao walikuwa na hii tabia ya kudandia dandia deal za Arsenal wakaja kuangukia pua kwa Mudryk wakajifunza.Siku hizi huwasikii tena wakisogeza pia kwenye deal za Arsenal
 
Kumbe hili chama letu Lina wafuasi wengi kiasi hiki jamanišŸ¤”
Zile nyomi zilikuwa pale Uganda na Kenya sio za kitoto wakuu.

Sipati picha jinsi trophy parade itakavyokuwa pale London Jumapili haswa tukiwa tumenyanyua UCL
 
Bei mbaya kinoma na kina ManU nao watataka kutoa 100m.
Nataka tusubiri kombe la dunia tucheki viSouth Americans vipambanaji mifano kama ya Alexis Sanchez na Cavani enzi wakiwa wamoto tuvichukue kwa bei za kishikaji zaidi.
Uza-Martinelli, Jesus, Norgaard, Ben White
Nunua-Morgan Rodgers, Alvarez, tonali na beki namba 2 mzuri...
Kuna timu zitakuwa haziji uwanjani....msimu huu tumehangaika kwa kuwa ule upande wa kushoto kulikuwa na mamburula...Rodgers aje ku compete na trossard na pia ni namba 10 mzuri....tonali mapafu ya duma....Alvarez mfungaji....tutakuwa tumekamilika kuanzia beki mpk forward mbele
 
Ningependa kumbakiza Martinelli niwauze Havertz au hata Gyokeres na Trossard ikibidi ndiyo aje Rojers. Nampenda Trossard ila naona Martinelli abaki kwa sababu ya umri wake na kiwango hayupo nyuma sana ya Trossard hivyo anaweza kumfukia kiwango chake na hata kumpita akikomaa, msimu ujao au ndani ya miaka michache.

Striker, sijazoea kuangalia La Liga so sijui Alvarez ana hatari kiasi gani ila nakumbuka kuna mechi tulicheza na Levrkusen halafu yule striker wao , Kofane, dogo ana miaka 19 ila kina Saliba walipata taabu sana kumzuia. Ningependa aje yeye au wa kufanana nae wa gharama nafuu ziaidi maana striker yeyote anayeweza kuwamudu kina Saliba, bora awe upande wetu. Halafu tutafute AM mwenye uwezo w kuwaweka Ode na Eze bench (kama Rogers).
 
Back
Top Bottom