Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Psg wamenunua refa. Bayern haruki hapa kama atatarajia fairness
 
Kubababake wazee Bayern wamesusa kucheza wamemfuata refa wamemzunguka kaona aibu sasa hivi.
 
Mashabiki wa Bayern wameanza kutupa vitu uwanjani. Neuer anawaomba waache
 
Hivi unajua mwaka jana PSG katutoa kwa sababu ya ubora wa donaruma na sio walituzid mpira
mechi zote mbili ndio alikuwa MAN OF THE MATCH
Teh teh kuna muda inabidi utulie tu ukubaliane na mawazo ya haters.

Hao Bayern na Psg unaweza ukafikiri ni timu za Sayari ya 20 huko, kumbe tushacheza nazo tukazifunga/zikatufunga kama timu nyingine tu tulizokutana nazo.

Naangalia game ya Psg/Bayern now, hakuna cha ajabu wanachocheza Arsenal tusiwafunge. Tukutane Budapest.
 
Haya majinga yamegundua Defence nzuri itawapeleka fainali, hayachezi tena kama yamekatwa vichwa.

Waungane watengeneze kikosi kimoja tukutane fainali l
 
Bayern inacheza kama imekata tamaa sitashangaa wakisema refa amewaua. Yaani wanacheza hawana haraka utadhani wao ndiyo wanaongoza.
 
Huyu refa asipopigwa leo na jinsi Bayern hawapendi kufungwa nitashangaa
 
Kipindi cha Kwanza Atletico walipigwa msako wa nyani ikabidi weweke ukuta wa Yeriko

Baada ya kufungwa goli walilazimika kutanua uwanja kwa lengo la kutafuta goli ila tukawakalia ngumu.
Walipata clear chances mbili pekee mechi nzima bt hawakuzitumia ipasavyo.

Dakika 15 za mwisho Atletico walikamia Sana mechi nusura watufunge.
Ahsante mkuu, trailer limetosha kupata picha kamili
 
Tunaenda kukutana na PSG.

Sasa jana tulilalamikiwa Arsenal tumeshangilia kupita nusu utadhani tumechukua kombe. Niliangalia hii mechi nione kama atakayepita hatoshangilia.

Anyways, kwanza Luis kaiongopea dunia, alidai yeye haji kulinda ule ushindi anakuja kushambulia. Kilichotokea Bayern nahisi wakaamini na wakadhani wenzao watakuja swinging kama ile first leg.

PSG kaja kapaki basi. Alikua anafanya swarming mbele ya goli, advantage ya swarming ni kwamba hata kama hamjui kukaba ila mkiwa wengi tu mbele ya goli basi tayari mmeshakua kikwazo.

Bayern hawajaamini macho yao.

Nataka nione waliodai mpira wa burudani ni goli tisa kwa mechi watahukumu vipi hii game. Kitakwimu first leg ya Atletico na Arsenal ilikua juu kiushambuliaji kuliko first leg ya Bayern na PSG.

Lakini tulivyopoint takwimu tukajibiwa kinachomatter ni magoli. Ngoja tuone hii ya leo itasemwaje.

Mimi ninaamini Donnaruma aliwaokoa PSG dhidi yetu msimu uliopita, niliangalia hii mechi pia nione kipa wa PSG, Safonov, ana ukali gani. Jamaa siyo mbaya, lakini Bayern hawakumpa tests nyingi za kuhitimisha hii observation.

Mengine nitayakumbuka nikiamka.

We move
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom