Kama ni project, Arteta kafanya sehemu yake na kaweka msingi mzuri unaoonekana. Lakini bahati mbaya sio kocha mwenye utashi wa kubeba makombe maana anaishiwa mbinu mbadala kipindi flani. Fikiria ndani ya misimu 3 au 4 Kocha anaishia kuwa nafasi 2 halafu bado una matumaini naye ya kukutengenezea timu ya makombe uko mbeleni?
Nakumbuka msimu wa 2011/2012 SAF alivyokosa kombe kwa tofauti ya magoli ya kufunga, usajili wake uliakisi mapungufu aliyoyaona msimu uliopita, akamleta RvP na msimu uliofuata akachukua kombe kwa mchango mkubwa wa Van Persie. Msimu wa kwanza wa Pep 2026/17alifanya sajili karibia 8 hivi lakini akaishia nafasi ya 3, msimu uliofuata akaleta wachezaji wazuri hadi kufikia kubeba ndoo. Sasa rudi kwa Arteta, anauza Partey anamleta Zubimendi na Norgaard, Madueke na mabeki wahuni wa kiitaliano ili kucheza haram football. Kimsingi arsenal hakukosa ubingwa msimu uliopita sababu ya defence, bali offense. Tuliongea humu kwamba Partey alikuwa anawapa bima akina Rice wanaonekana world class lakini mkamletea Zubimendi mwishowe jamaa haonekani kwenye attack mara kwa mara kama ilivyokuwa msimu jana.
Narudia tena, hata kama ikitokea bahati mbaya Arsenal akachukua ubingwa msimu huu anatakiwa kuondoka Arsenal kama mnataka kuendelea kugombea mataji ila kama ndoto ya uongozi ni kuchukua kombe moja na kuendelea kufanya biashara ya jezi, basi ni kocha sahihi wa kutoa burudani ya inverted fullback na overloading ila mwishoni mtakuwa Netflix