Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nuno hawezi kukubali Nottingham wasogee kwenda mbele halafu yeye abaki pale chini.

Ninaona akienda kujaribu kuleta upinzani dhidi ya United. Allypipi atakachotabiri kitatoa picha zaidi
Mkohoti
Umemaliza kujichekesha au hujapata matokeo ya United na Westham
 
tukishinda hii game itakuwa unyama sana.
Hii mechi ina maana kubwa sana, kama tutashinda itakuwa ni mwendelezo wa marekebisho katika zile timu ambazo zilitunyima ubingwa msimu wa 23

Zikiwemo Fulham ambayo tumeshinda, west ham ambayo tumeshinda na engine ni hii Aston villa, kwahiyo kama tutashinda itakuwa tumepata points 9 katika mechi za awali ilhali msimu ile tuliambulia point 0
 
At this point ni ushindi tu ndiyo way forward. Kila timu hua inatusubiri kwenye long balls na kupaki basi, ni vile tu Villa amekua successful kuzidi wenzake ndiyo sababu tunahofia anaweza haribu shughuli
Shida ni kwamba kwa sasa timu yetu imepoteza balance hasa kwenye kupata magoli, tulikuwa tunafunga magoli aima zote yani kwenye set piece na open play

Ila tangu Gabriel apate majeruhi hatujafunga tena goli la set piece na hii ni wazi kuwa Kuna nguzo imepungua kwa sasa katika timu yeti

Na Saliba nae kuumia kumeongeza kitu kwa timu pinzani na kupunguza kitu kwetu, timu pinzani hawatuoni tena kama timu ngumu kufungika kwa sababu Moja ya fear factor haipo

Msimu huu ndio ule msemo wa Sir Alex Ferguson "Attack wins you games, defence wins you titles" ulikuwa unaenda kutimia, kwa sababu ata ukipata goli moja la set piece na ukalilinda umepata point 3

So tulikuwa na Advantage ambayo City msimu huu hana kwa sababu ana ruhusu sana Magoli though nayeye anafunga sana magoli na faida ingine kubwa aliyonayo City hana bahati mbaya ya Majeruhi kama sisi
 
Hii game tukipata ata suluhu TU inatosha, maana Unai waga ni kama vile bado ana bifu na Arsenal, huwa anachukulia very personal

Wakati sisi tunaomba suluhu na City nae apate suluhu kwenye game yake na Sunderland lasivyo maji yatazidi Unga
Aisee
 
Upo sahihi, kuna interview moja ya Saliba alisema anajaribu na yeye kuhusika zaidi kwenye kufunga kwakua mara zote amekua akifanya set up ya Magalhaes kuscore.

Muda wa kona Saliba hua anakaa mbele ya kipa anakua kama anamkinga ili akicheza vibaya iwe penalty. So ni sahihi kwamba uwepo wa Saliba ungeweza saidia hata wengine kuscore kona siyo Magalhaes pekee.
 
Nyie vilaza nasikia milio imeanza kuwatoka, sasa hatutaki visingizio vya mechi ya mapema.
 
Hii mechi kila mtu anaisemea jambo.

Mimi naona kwa leo tuna fursa ya kufia arena kwakua CL tunakuatana na timu ya kawaida.

Inaaminiwa Saliba atakuepo leo. Na ingawa Gyokeres amerudi ila Merino works hard so inawezekana kabisa akaanza Merino. Odegaard karudi, Eze anaweza kupelekwa LW.

Ngoja kikosi kije
 
Kabisa, ngoja tuone lineup Arteta amekaa vp leo.
 
leo ni kama timu itacheza na viungo wa ndani wa5 na mshambuliaji wa pembeni saka.

nafkiri ni sahihi kwa hicho kikosi mana villa wao timu yao pia ina viungo wa ndani wengi ,mshambuliaji wa kati ni watkins.

umakini unahitajika kwenye mipira ya kona.. villa ni hatari zaidi kwa leo.

draw kwa arsenal ni fair result.. ushindi ni bonus.
 
Saka awe makini zaidi, hii ya kupoteza mipira na tuko kwenye move itazaa bao mda si mrefu
 
ΓΈ akirudi kipindi cha pili nitashangaa mno.. yuko soft mno na mpira leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…