Inawezekana ushabiki wa mpira umeanza juzijuzi hujui wala huelewi haya yameanzia wapi ndio maana unasema haya. Kwenye hii michuano ya FIFA CWC ilikua ni Chelsea dhidi ya vilabu vyote vya EPL na wapinzani wakubwa ni Liverpool, Man Utd, Arsenal, Man City.
Sasa kwanini Arsenal? Kwanza kabisa ni mpinzani wa jadi katika jiji la London, kila mmoja anataka kuonesha yeye ndio ana timu bora zaidi London. Hivyo hayo yanaenda sambamba na kubeba makombe, hivyo kinachoendelea hapa ni muendelezo wa hayo yote. Pili, anasemwa zaidi Arsenal kwasababu misimu ya hivi karibuni hajabeba kombe lolote wakati Chelsea ndani ya msimu huu kabeba makombe mawili tayari.
Hasemwi Man Utd kwa sababu yule tayari keshajifia kibudu, hasemwi Liverpool kwa sababu tayari ni bingwa EPL, Hasemwi Man City kwa sababu huna wa kubishana naye mtandaoni, hasemwi Spurs kwa sababu ni bingwa wa EUROPA. Kwahiyo usishangae haya yanayoendelea siku ukifika level ya Chelsea nawewe utafanya hivi. Walikuwepo kina Dully Jr sijui yuko wapi huyu dogo, wengine nishawasahau na wengine bado nawaona humu, tulikua tunabishana na kutambiana sana. Wewe yawezekana ni mgeni karibu.