Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Huyu amesajiliwa ili kumpuzisha Saka tukikutana na timu mlenda mlenda kama nyumbuz.
Then tukikutana na timu kama Real Madrid ndo tunapanga 1st eleven
 
Tunaongeza takataka kwa kweli...
Huyu MADUEKE nimewahi kumuona mara 2 tu, na zote hizo nikaamini mie nikifanya mazoezi ni bora kuliko yeye, sasa imagine mchezaji kama huyu ndio anakuja arsenal..
Ila mganga wa Chelsea ni kiboko, kuna tetesi zinaagaa kwa kasi kua Nyumbu tunamtaka Nicolas Jackson, utashangaa tunaingia kichwakichwa tunagongwa £65m na tunatoa.
Nyumbu na Arsenyashi kwa Chelkenge ni kama tu mbwa mbele ya chatu.
Huaga tunajipeleka wenyewe huku mkia tumeubana matter konny.
 
JAoa Pedro alivyomwambia kocha wa PSG Hana tofauti na Arteta akaona ni tusi ikabidi arushe ngumi ndio sisi Chelsea tutamani kuwa Kama nyie kweli ???
 
Yule Hoijlund wenu sio takataka kweli?
 
Inawezekana ushabiki wa mpira umeanza juzijuzi hujui wala huelewi haya yameanzia wapi ndio maana unasema haya. Kwenye hii michuano ya FIFA CWC ilikua ni Chelsea dhidi ya vilabu vyote vya EPL na wapinzani wakubwa ni Liverpool, Man Utd, Arsenal, Man City.

Sasa kwanini Arsenal? Kwanza kabisa ni mpinzani wa jadi katika jiji la London, kila mmoja anataka kuonesha yeye ndio ana timu bora zaidi London. Hivyo hayo yanaenda sambamba na kubeba makombe, hivyo kinachoendelea hapa ni muendelezo wa hayo yote. Pili, anasemwa zaidi Arsenal kwasababu misimu ya hivi karibuni hajabeba kombe lolote wakati Chelsea ndani ya msimu huu kabeba makombe mawili tayari.

Hasemwi Man Utd kwa sababu yule tayari keshajifia kibudu, hasemwi Liverpool kwa sababu tayari ni bingwa EPL, Hasemwi Man City kwa sababu huna wa kubishana naye mtandaoni, hasemwi Spurs kwa sababu ni bingwa wa EUROPA. Kwahiyo usishangae haya yanayoendelea siku ukifika level ya Chelsea nawewe utafanya hivi. Walikuwepo kina Dully Jr sijui yuko wapi huyu dogo, wengine nishawasahau na wengine bado nawaona humu, tulikua tunabishana na kutambiana sana. Wewe yawezekana ni mgeni karibu.
 
Wanawake wamemchukua Olivia Smith wa Liverpool kwa world record fee ya 1 million pounds.
Hapo Kelly naye tayari, na kipa mpya...
Wapewe tu makombe yao mapema.

Bado wanaume sasa kufanya maajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…