HENRY14
JF-Expert Member
- May 13, 2021
- 3,674
- 7,130
Chelsea huwa hauzi magarasa yake mbali na London, anajua sehemu ya kuwapeleka pindi wakishindwa kufit kwenye mfumo wake.
No one saw this coming! Unakataa kumuongezea Octopus £50,000 unamleta Madueke akupe EPL!
Kama chelsea sio wachawi basi Arsenal huwa wanapenda kitenga sana.
Octopus kuna wabaya wetu walikuwa wanatutegea tumpe mkataba mpya halafu akisaini na msimu mpya ukianza tu wanaanza kumpeleka mahakamani na kumtoa kwenye mfumo. Sisi hapo tunabaki na Zubimendi tu, hatujamnunua Norgaard.
Ila Berta ni Mmafia akaushtukia mchezo akatoa ofa mezani.
Tukiacha haya mambo serious, mimi kweli sikuona kama Partey ni mtu wa kumuongezea mshahara wala mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja, miwili ikibidi saaanaa. Huu ndiyo msimu ambao ameweza kukwepa meza ya matibabu. Amekuwa kama wachezaji wengi ambao wanacheza vizuri msimu wa mwisho au kuwa fit msimu wao wa mwisho wakiwa wanataka mkataba mpya.