HENRY14
JF-Expert Member
- May 13, 2021
- 3,593
- 6,932
Hili goli ambalo mpira uliufuata mkono wa Kai haina hata haja ya kusumbuana. Mechi imeshaisha hata kama ikaonekana ni kweli zaidi ya kugewa barua ya kuombwa msamaha hakuna jipya.
Kilichotokea kimeendeleza ambacho tunakiona mara nyingi. Weka Partey RB observe unavyoshindwa kusecure points 3. Kipindi fulani hivi wakati liva ipo on fire inamiliki mpira mpaka 80% nikawa nasema kwamba tunateseka dhidi ya liva kwakua Arteta ana tabia kama ya Wenger.
Ilikua haijalishi anakutana na mpinzani gani Wenger alikua anataka acheze sexy football huku anascore. Arteta aliwahi kufanya defense iliyowahi semwa haifundishiki kua ya pili kutoruhusu magoli mengi. He did it with back 3.
Kama hatuna RB na inatusumbua hiyo ishu kwanini isichezwe back 3. Nimeona anasema kikosi ni kidogo na wanacheza kila baada ya siku 2. Ok sawa, nani ambaye hachezi kila baada ya siku 2?.
Ratiba hua inatoka ya mwaka mzima. Hakujua hili swala?
Kweli. Tuachane na yaliyopita. Ila kwa jana nasema ni yale yale ya sisi kukosa kidogo na wao kupata. Je Partey angewahi kidogo au Timber angekuwa RB ile cross ya goli la kwanza ingezuiwa? Haya cross ilipigwa ila...je Merino angefikisha mguu nusu sekunde kabla si Tielemans asingepata header?
Ok, Tielemans amepata header ila kidogo tu Raya aokoe....au je Raya angetokea kuclaim ile cross...? Mambo yote yamekaa sawa Villa wakapata lile goli ila wangeweza kukosa kimoja kati ya hivyo vingetokea. Marubani wanaita hii 'Swiss Cheese Model'.
Goli la pili pia, Havertz angeugusa kidogo zaidi ule mpira, Watkins hafungi. Au Raya angeiclaim ile cross...?
Lakini kwa kweli kwa game ya jana simlaumu sana Partey kwa position yake maana naweza kusema ni lile goli moja la kwanza alichelewa kuzuia cross ila mengine yamgefanyika kuzuia goli.
