Tunakosa sana nafasi za wazi kiasi kwamba unaanza kuhisi tuna nafasi ndogo ya kusonga tukikutana na Elite teams kwenye hatua ya mtoano... Kwasababu haziwezi kukupa nafasi nyingi hivyo. Nafasi chache utakazopata inabidi uzitumie.
Kuna vitu Jesus anakupa Kai Havertz hawezi kukupa kamwe.. Kuna vitu Kai Havertz anakupa Jesus hawezi kukupa kwa sasa na amepoteza uwezo huo hasa anapokuwa 1vs1 na kipa. Hatuwezi kwenda mbele na aina hii ya wachezaji ambao wanabeba roho ya timu pale mbele. Arsenal wanamuhitaji namba tisa Kariba ya Alexander Isak.
Yani sisi kwenye transition ni sifuri sifuri kabisa na ndio sababu tupo kwenye nafasi tuliyopo, mtu anakwambia leao hana maana tena sababu kasajiliwa Harvertz, kwa nafasi hizo za trossard, ode na Martinelli?
Goli la kwanza lilionyesha mipango la pili ni matokeo ya high pressing, la 3 limeonyesha poor form ya mguu wa kulia wa Saka na kua wakati sahihi na muda sahihi kwa Kai.
Tulikua na big chances 6. Tatu zilizokoswa ni zimeonyesha udhaifu wa forwards zetu kwenye 1 v 1. Hapa Odegaard na Jesus walibaki na kipa na hakuna aliyekua na composure wala skills kwenye execution.
Against timu kama Fulham ambazo zipo nyingi EPL hupati hizo 1 v 1 unabaki kutegemea crosses ambazo wamaliziaji hua hawapo sehemu sahihi.
Martinelli is shaky. Kuna watu online wanasema hua anaangalia sana chini hadi hajui anapoenda. Mimi namuona mchezaji ambaye confidence imekata kwakua kila ambacho zamani alifanya kilikua sahihi sasa hivi hakiwork tena.
Lewis-Skelly ana pasi nzuri yule dogo, jana ni mwendelezo wa pasi zake ambazo magoli yalianzia hapo. Kuna watu pia wanasema Arsenal imchukue Arda kwa mkopo kutoka Madrid na nikawahi kusema sasa kwanini game time asigewe Nwaneri badala ya kuleta mtoto mwingine ambaye timu yake imeshindwa kumpa game time?
Tulikua na Chido. Great goal scorer akaenda united kwakua scale yetu ya mshahara haikusapoti alichotaka alipwe. Juzi nikaona sehemu inasema alienda united kwakua ina sera nzuri ya academy kuingizwa first team.
Ni uongo ila ni ngumu kuoverlook kama wachezaji kama Nwaneri huwapi game time.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.