Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Walcott sijui ana matatizo gani siku hizi..Huu ndo muda mzuri wa oxlade kupata namba.
Huyu dogo hamna kitu kabisa.
Park naye vp? Naona fom yake kwenye tim ya taifa ipo juu sana. Mbona babu hampi nafasi?
 
Nimesahau kukupa hongera zako Wacha1 Shawcross and the gang wanatia timu Emirates jpili, jiandae.

Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee chubiri ubatizo kutoka kwa QPR khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Sawa sawa mkuu wangu wala hamna tatizo, tusubirie tu tutaona.....lazima tutembeze kichapo pale nyumbani maana lazima ukumbuke tuna record hapa kwenye uwanja wetu.....

Records are there to be broken khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee



BTW Wakuu mwacheni Theo hana tatizo lolote kila ndege huruka kwa mbawa zake kuna siku game hukataa he is ok. Wasi wasi wangu upo kwa Arshavin na Santos zaidi Theo anajituma sana na hawezi kutusaliti kama wachezaji wengine wanaotoka nje ya UK.
 
Habarini wana Gunners wenzangu,tupo pamoja wakuu.Tujipongeze kwa ushindi wa leo,na imani kabisa huo ni mwanzo tu,Hii ni baada ya wachezaji kuanza kuelewana vizuri.Japokuwa defence yetu bado haijakamilika lakini baada ya wiki mbili TV5 anarudi hapo ndo moto wake utashika kasi ya ajabu.

Mkuu karibu sana naona umeingia na baraka tele, mwakani kutakuwa na sherehe kubwa sana Emirates , Wacha vijana warejee.
 
Mkuu karibu sana naona umeingia na baraka tele, mwakani kutakuwa na sherehe kubwa sana Emirates , Wacha vijana warejee.
Mkuu nashukuru sana,naona vijana wameanza kuelewana,tukumbuke kuwa hawakuwa pamoja kwenye Pre-season,walianza game bila kuwa wamoja lakini kwa sasa naona wameanza kuelewana,tatizo liko kwa Arshavin ni kama vile hupiga vitoti vya Vodka kabla ya kuingia uwanjani.
 
Sawasawa "Kweli", na blues wamewaonea wale wabelgiji bure, naona walikuwa wamekula mno "Cheese"!

Mpaka Torres kafunga?!

Ila babu wetu naona sio mkali sana kwenye dressing room, kuna wapuuzi kama Arshavin na Rossicky, wangekua "Manure", sidhani kama wamekungua wanacheza hivyo au kucheka cheka kimzahamzaha kama vile!



Nitakukumbusha tarehe 29.10.11.
 
yaani game ya Leo naisubiri kwa hamu.. Nasoma tetesi online wanasema v.persie anaweza kupumzishwa , sijui kweli ..?
 
yaani game ya Leo naisubiri kwa hamu.. Nasoma tetesi online wanasema v.persie anaweza kupumzishwa , sijui kweli ..?

bora atokee kwenye benchi, kwani hawa wacheza rugby *stoke city* hawachelewi kumvunja.
 
Yeah Van Perse yupo nje, yaani naangalia leo mtakavyotandikwa....why awekwe nje kwa ajili ya league cup au kwa ajili ya nini???leo mtafungwa naona
 
Ndio hapo unapomkumbuka mtu aina ya Emmanuel Eboue........Alikuwa ni mbadala mzuri sana wa Sagna pale kulia nyuma.....Huyu Jenkinson kalegea sana na hana nguvu kabisa.......

Labda ifike mahali AW aanze kuwajaribu Squillaci na Djourou kwenye nafasi ya beki wa kulia sasa.....
Nafurahi kuona AW anaanza kusikiliza kilio/maono yetu.....Dogo Jenkinson pamoja na kwamba ni majeruhi huwa kalegea sana......

Arsenal Vs Stoke

Asenal Team in full: Szczesny, Djourou, Koscielny, Mertesacker, Andre Santos, Song, Arteta, Ramsey, Walcott, Gervinho, Chamakh.

Substitutes: Fabianski, Frimpong, Rosicky, Benayoun, Arshavin, Park, Van Persie.

Kila la heri 'Ze Gunaz' wenzangu
 
Yeah Van Perse yupo nje, yaani naangalia leo mtakavyotandikwa....why awekwe nje kwa ajili ya league cup au kwa ajili ya nini???leo mtafungwa naona
Pilipili iko shamba ...........................?
 
Back
Top Bottom