Mwamba anavyoandika kwa uchungu, kana kwamba ana nia nzuri na Arsenal. Sisi sote tunaijua Arsenal yetu ilipotoka, na ilipo sasa hivi. Kelele zote hizi ni kwa sababu wanaogopa kinachokuja kuwatuka misimu ijayo.Yes, kinachokuja kuwakuta.
Klopp, anapewa Liverpool October ya 2015, iliyomaliza nafasi ya 6 msimu wa nyuma na kwenda Europa League. Klopp anawapeleka Liver fainali, na kushika nafasi ya 8 EPL. NO TITLES
Misimu wa pili wa Klopp, 2016/2017, anashika nafasi ya 4 EPL, timu inaenda UEFA CHAMPIONS LEAGEA KWA MARA YA PILI NDANI YA MIAKA SABA. Yani from mwaka 2009 mpaka 2017, Liverpool imeshiriki UCL mara Moja tuu, msimu wa 2013/2014. Klopp anawapeleka kwa mara ya pili 2017/18. NO TITLES
Msimu wa tatu wa Klopp, 2017/2018, NO TITLES
Anaanza kupata mafanikio msimu wa nne, 2018/19
Huyu Klopp tunayemzungumzia hapa, ni experienced coach wakati anakuja Liverpool, tofauti na Arteta ambaye ndio timu yake ya kwanza kuimanage.
Mwaka 2019, December, Arsenal wanamchagua Arteta kuwa kocha.
Msimu wa kwanza, Dec 2019 to May 2020, FA CUP.
2020/21 COMMUNITY SHIELD
2021/22 NO TITLES, Huku timu inaendelea kujengwa
22/23, 2nd Place EPL (kwa timu ilipotoka, hii ni ishara mwelekeo wa timu ni mzuri)
23/24, COMMUNITY SHIEF, Timu inarudi UCL, 2nd Place EPL
Kwa akili iliyosalimika, ukiangalia hiyo safari ya Arteta, unaona kabisa Arteta kuna kitu kinakuja. Hiki kitu kinachokuja, akina FLANO na MKOHOTI wanahofia yasije yakawa kama ya Klopp, EPL na UCL. Hapa ndo msingi wa kelele zao unapoanzia