Kwa hiyo katika hiyo miaka 21, yote Arsenal imekuwa ikimilikiwa na Kroenke?
Na kabla ya hapo Arsenal ilikuwa haijahama kutoka kwenye stadium moja hadi ingine kwa kutumia pesa zake yenyewe na si za mfadhili mmoja?
Kipindi hicho Arsenal imekuwa haina deni la kulipa la hiyo stadium na ukiacha ubingwa tu, haikuwa ikitegemea top 4 qualification ili ipate pesa ya kulipa deni na kujiendesha?
Ni kweli kuna makosa mengi sana Arsenal ilifanya katika jitihada zake za upambanaji, mfano kupiga dili za sponsorship za hela ndogo ukilinganisha na wenzake kama kina Man Utd, scouting ya wachezaji bora, viongozi wahuni, nk. Matokeo ya makosa hayo yalionekana kwa Arsenal kushuka mpaka kuanza kukosa kabisa champions league.
Ila je huoni kwamba baada ya Wenger kuondoka Arsenal imefanya juhudi za dhati za kurejea juu? Huoni kwamba sasa kwa misimu miwili mfululizo tumegombania kombe? Huoni kwamba kwa misimi 4 au mitano sasa tumetoka kwenye kumaliza kwenye nafasi ya hovyo mpaka bora huku tukiongeza points msimu hadi msimu?
Ukisema 'hakuna kitu ndani ya miaka 21', sielewi wewe unatazamaje mafanikio ama progress. Mwaka huu tumefika points nyingi zaidi tulizowahi kushika na bado hatujashinda ligi. Hiyo si progress? Mwaka huu Kipara kashinda ligi na points 91, nadhani kuna mwaka ameshinda na points 101. Points 10 chini zaidi. Je hiyo ni progress?
Najua mambo mengine ni ushabiki tu na tunapenda sana yawe hivyo, ila watu wanabidi wachunge sana attitude za mafanikio kwa maono yako wasiyapeleke kwenye maisha yao maana mtu unaweza kushindwa kujua wapi unasonga na wapi unarudi nyuma.
Enzi za shule niliwahi kuongoza darasa na average ya 76%. Nyumbani full shangwe ila mimi niliuchuna sikusherekea. Sababu ilikuwa ni muhula uliopita nilikuwa na average ya 86% ila nilikuwa wa nne (niliingia top 4 ila bingwa alikuwa mwingine). Enzi hizo pass mark yangu binafsi ni 80, bila kujali wanafunzi wengine wamefaulu vipi, nikipata chini ya hapo naona nimefeli. Nikipata hapo na zaidi naona nimeelewa material.
Arteta na Arsenal nawaangalia kwa jicho la hivyo pia. Naponda sana ila pia naona tofauti kutoka tulipoporomoka mazima na sasa naona tumepanda na tunapanda.
Mnatuita false hopers kwa sababu tunataka ubingwa? Sasa kwani ni nini tunapambania? Si ubingwa? Hamtaki tuseme kuwa tunautaka huo ubingwa? Mnafikiri tunatosheka na top 4 siku hizi?
Kuna watu ambao timu isipochukua ubingwa hawaoni kitu kingine cha maana tulichokifanya.
Wanashindwa kuangalia tulipotoka ni wapi ukilinganisha na hapa tulipo hivi sasa... mbaya zaidi hata mashabiki hata mashabiki wa Arsenal baadhi wako na hizi fikra kwamba baada ya kuukosa ubingwa basi hakuna kingine cha kujivunia.
Binafsi naona kama kusingekuwa na improvement yoyote kulinganisha na msimu uliopita basi tusingestahili hata kupigiwa makofi.
-Ukiangalia msimu huu points tulizokusanya(89) ni nyingi kulinganisha na tulizokusanya msimu uliopita(84).
-Mechi tulizoshinda(28) ni nyingi kulinganisha na tulizoshinda msimu uliopita(24)
-Magoli tuliofunga msimu huu(91) ni mengi kulinganisha na tuliofunga msimu uliopita(88), japo msimu jana tulikuwa na wafungaji wengi(19) kulinganisha na msimu huu(16).
-Magoli tulioruhusu msimu huu(29) ni machache sana kulinganisha na tulioruhusu msimu uliopita(43).... bila kusahau kwa mara ya kwanza tumemaliza msimu tukiwa na cleansheets 16, hii inaonesha ni jinsi gani defense yetu ilivyoimarika mara dufu.
-tukiacha na hizo records hapo juu, pia tukumbuke tumeshaondoa ule unyonge kwa wakubwa wenzetu, tumeshinda big matches zote hapo mwishoni..... sikumbuki mara ya mwisho ni lini tuliweza kushinda dhidi ya Chelsea, Tottenham, Manchester United na tena wakiwa wamefuatana fuatana ndani ya mwezi mmoja tena tukielekea kumaliza msimu kwenye nyakati ambazo ni za pressure.
-Vile vile pia tusisahau sisi ndio timu pekee tuliokuwa kiboko ya kipara msimu huu, kwenye mechi mbili zote ameambulia point moja tu something we had never done before, na pia sisi hawa hawa ndio tulimzuia Kipara asi achieve sextuple kwa pale uingereza baada ya kumtandika kwenye ngao ya jamii..... na iko wazi kuwa sasa hivi sisi ndio tunaomnyima usingizi kipara.
Kiukweli kuna massive improvements ambazo tumezifanya na zinatuweka mahala pazuri sana za kuchukua ubingwa msimu ujao... sasa kama kuna shabiki wa Arsenal ambaye anaona licha ya timu yetu kufanya hayo yote lakini bado ana nung'unika badala ya angalau ya kijivunia hapa tulipofika, basi nashauri mtu huyo atafute timu nyingine ya kushabikia ambayo anaamini itamuhakikishia mataji kila msimu.
We true gooners are so much proud of these little achievements we have made this seaso so far.