🅱️USARA ZA GWIJI WA HIGHBURY
"Nidhamu Ulinzi"
✍🏾 Pre Game nilisema match hii ni tactical battle game kama hizi uwa zina amuliwa na Small Margins.
✍🏾 Ndio Maana utasikia watu wanasema Match inaboa sio Match kuboa bali tactical discipline Kwa kila mmoja kulingana na game Approuch yake.
✍🏾 Arsenal aliingia uwanjani kama nilivyotamani iwe kwe pre game analysis Arsenal alikuwa anahitaji matukio tu ( Transition game) hivyo kamuachia mpira Man City alafu yeye akawa na Nidhamu kiulinzi.
✍🏾 Unaweza kuona Namna gani Arsenal Aliweza kuziba Mianya Yote Kwa Man city kupata Central progression licha kina Bernando kuja ndani kujaribu kutafuta Numerical Superiority ila Kina Kai na Jesus walirudi deep kutoa Msaada.
✍🏾 Hii ikafanya Man City waanze kutumiq maeneo pembeni kutafuta 1vs 1 ndio Maana wakaaingia kina Grealish na Doku.
✍🏾 Arsenal pia Akaja na Jibu kuwafanya Winger wake kurudi chini kusaidiana na FB kukaba hii ikawapa shida tena Man city sababu Arsenal walifanya Discipline hali juu sana.
✍🏾 Nimewahi andika sana kuhusu OPP ( Out of possession Press) Arsenal ni hali juu mno.
✍🏾 kuna muda Wakakabia highline na city akifanikiwa bypass hapo hapo wanarudi haraka wanakabia Low block Utimamu unahitaji energy kubwa sana.
✍🏾 Tangu 2021 Man City hawajawahi shindwa kufunga goal lolote lile pale Ethard Mpaka leo Arsenal kawazuia.
✍🏾 Man City akiwa Home anapiga Ontarget 1 dakika 90, anatengeza XG below 1 unaweza kunielewa hii ilikuwa tactical battle.
✍🏾 Saliba Na Gabriel bila sahau White, Kiwior na team nzima japo Saka hakuwa mchezoni nadhani majeruhi pia na pia City walijiandaa kumzuia.
✍🏾 Kama huwezi kushinda mchezo basi jitahidi usipoteze pia Mapambano yanaendelea.
Amigos