Charlz ze son conscious
JF-Expert Member
- Aug 22, 2019
- 563
- 856
1: Compact 4-4-2 hakuna space kabisa katikati ya mistari yao yote mitatu na kuwalazimisha Arsenal kwenda pembeni kutumia wingers
2: Uzuri kwa Porto fullbacks wao wazuri kwenye 1v1 na pia hata Arsenal wakifanikiwa kupiga krosi Pepe , Otavio na Golikipa wao Costa wanacheza mipira yote wao tu .... goli linatokea wapi ???
3: Viungo wawili wa kati Nico na Varella walikuwa muda wote wame switch ON kuzuia namba 8 wawili wa Arsenal Kai na Odegaard ( Track runners ) na hata wakipata mali wanapasia vizuri sana , ni msingi mzuri wa kufanya counter attacks
NOTE
1: Kwenye timu hutakiwi kuwa na abiria kama unataka matokeo mazuri tena kwenye mechi za daraja la juu Ulaya , Porto wamefanya hivyo
2: Odegaard akiwa na mali mguuni , kafundi sana kale kajamaa
3: Saka , Martinelli ,Trossard na Kai kazi yao ilikuwa ngumu sana leo
4: Diogo Costa : Mipira ya hewani alikuwa anaicheza vizuri sana na akiwa na mali mguuni kushoto au kulia bila wasiwasi anapiga mipira vizuri
5: Galeno kwanza alivyogongesha nguzo halafu baadae alivyomtungua Raya ... umaliziaji mzuri sana .!
6: Arsenal wamemaliza mechi bila shot on target hata moja
FT: FC Porto 1-0 Arsenal
#ambangille