Hapa Zinny mtamlaumu bure, mara nyingi mchezaji ‘left footer’ mguu wake wa kulia ni weaker kulinganisha na mguu wa kushoto wa mchezaji ambaye ni ‘right footer’.
Kwa LB anayetumia mguu wa kushoto akikutana na inverted winger kama Salah, Saka, Bailey, Foden nk kwenye mazingira ya 1v1 atateseka tu.
Hawa watu ni ama umuwekee watu wawili au apate LB anayetumia mguu wa kulia kama Tomiyasu ama Timber. Last game vs Liver alipoingia Tomiyasu ule upande, Salah hakuonekana tena.
Tukiacha yote, unamuongelea Salah ambaye anatajwa kuwa one of the greatest player in PL history. Kama unamchukulia Salah poa, tafuta records zake against ‘big six’ uone anacho wafanya, hapo usizungumzie hawa team ndogo ndio balaa kabisa.
LBs wengi kama si wote wa EPL na hata Uefa kwa Salah ‘wanaloa’, huyu jamaa ni msumbufu sana kumdhibiti kiukweli bila kuwa na mkakati maalum.