Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kwenye mauzo ya wachezaji, nakubaliana ba waliosema mauzo yetu huwa hayalingani na thamani ya wachezaji husika. Hii ni kwa sababu wahusika wa hizo deals na uongozi wetu kwa ujumla ni wabovu katika kazi hiyo. Tuliwapoteza kina Henry, Fabregas, Van Persie...kwa pesa ndogo tu huku kina Tottenham wakiwauza kina Bale, Modric na hata Kane kwa pesa mingi. Ozil, Auba tulivunja mikataba kabisa ili wasepe, kwa sababu zilizoeleweka wakati huo ila bado ilikuwa hasara kifedha. Hasara hiyo pia tunaweza kusema imeleta faida kwa timu, ikaleta faida uwanjani na hatimaye ikaleta faida mfukoni maana tulirejea champions league.
Kwa upande mwingine, tuliweza kuwauza kina Iwobi na Ox kwa pesa tuliyoona ni zaidi ya thamani yao. Tuseme tu hatuna uongozi mzuri kwenye mauzo. Ni suala lakushughulikiwa.
 
Hata wakiwepo there is no way watapokea ofa ya kumuuza Saka au Martinelli leo
 
Jamaa unawapiga nyundo za miguu.
Sema sasa hivi wana SAKA watauza € 80m.
 
Kama mtu asipoelewa hiki basi ni kichaa na mtindio wa ubongo, izi takwimu mara nyingi haziakisi lolote, izi izi takwimu unaweza kumkataa Rasmus Hodjland mbele ya Eddie Nketia 😁.
 
Kwa mu
kwa mujibu wa aliyeleta hoja kai ana goli 3 Bruno G ana Goli 1 kwaiyo kwa maana iyo anaenda na Kai why nimuache Nje kai.. Uyo shabiki wa 4castle ndo anaamin takwimu pekee wala sio mimi
 
Sitajibu kitu chochote cha shabiki wa nyukesto kuhusu ubora wa timu yake/ wachezaji wake mpaka akirudi top four.

Mijadala mingine naweza kuendelea naye.

Mkinikuta, nikumbusheni hii post najipiga ban
 
Hata wakiwepo there is no way watapokea ofa ya kumuuza Saka au Martinelli leo
Inawezekana tumeboresha utendaji wetu. Unaona siku hizi wachezaji vijana wazuri wanaongezewa mikataba mapema. Hii inafanya iwe ngumu kwa wapinzani kuwasogelea wachezaji wetu.

Kuhusu hao wachezaji wa newcastle, tusimind sana maana hata sisi tuliwataka au tulihusishwa na Isak, Bruno... kwa hiyo tuwapongeze kwa kupata wachezaji. Labda Labyrinth anajaribu kutuambia kuwa tungekuwa na Bruno, Isak, Wilson na Gordon saivi tungekuwa tumebeba kombe 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…