Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Sir Alex Ferguson aliwahi kusema good attack wins you matches but good defence wins you titles, baada ya injury ya Saliba na Tomiyasu defense yetu ilishake sana last season mpaka tukakosa taji la ligi kizembe. This time our young side has matured, let the marathon continues.
20231130_094741.jpg
 
Natamani sana Nyumbu watolewe na tena wasienda hata Europa. Ila group lao lilivyo, daah, wana chance ya kushika nafasi ya 2 kama wakimpiga Bayern na Copenhagen na Galatasaray wakitoka sare. Siyo poa kabisa. Nilitaka mpaka hapa iwe imeshathibitika kuwa wameshafungishwa virago.
Hiyo permutations ngumu sana, mechi ikishakuwa nje ya mikono yako ujue imekula mazima tu.
 
Daaah kila nikiangalia Man Utd yangu na lile pira letu pira makande, Halafu hawa Arsenyau wazee wa Teta ball jinsi wanavyopiga pira Biriani pira Makange roho Inauma kinyama.
Ila uzuri wa Arsenyau ikifika mwisho wa msimu wakati wenzao wananyanyua makwapa wenyewe hua wakuna madako hapo ndio hua nafarijika sana
Kai Harvez jana kafunga mbona tutamkoma Masingeli leo humu.
Hongereni sana wanangu wa ukweli The gunners kwa kuongoza kundi ingawa kundi lenu mmepangiwa timu mchekea.
 
Amini mkuu hilo ni suala simple sana kwenye group lao. Group liko wazi mno. Bayern naona amefaidi kwa kutangulia kwa kushinda games ila kufungika anafungika. Nyumbu wakaze tu wampige bayern. Hao wengine wataumana sana jino kwa jino maana wote wanataka kufuzu na hatimae wataishia kutoka sare 😃
 
Daaah kila nikiangalia Man Utd yangu na lile pira letu pira makande, Halafu hawa Arsenyau wazee wa Teta ball jinsi wanavyopiga pira Biriani pira Makange roho Inauma kinyama.
Ila uzuri wa Arsenyau ikifika mwisho wa msimu wakati wenzao wananyanyua makwapa wenyewe hua wakuna madako hapo ndio hua nafarijika sana
Kai Harvez jana kafunga mbona tutamkoma Masingeli leo humu.
Hongereni sana wanangu wa ukweli The gunners kwa kuongoza kundi ingawa kundi lenu mmepangiwa timu mchekea.
Bro, kwenye kundi lako mpinzani wako ni Bayern tu, na Hamisi aka chambuzi nguli alishawaambia huyo bayern mwenyewe wa sasa maharagwe ya mbeya tu. Sasa nyie wenyewe mmelifanya kundi lionekane gumu halafu unakuja kuongea kuhusu hili letu. Mngetaka hilo kundi mngeliongoza, ila hamkutaka.
 
Natamani sana Nyumbu watolewe na tena wasienda hata Europa. Ila group lao lilivyo, daah, wana chance ya kushika nafasi ya 2 kama wakimpiga Bayern na Copenhagen na Galatasaray wakitoka sare. Siyo poa kabisa. Nilitaka mpaka hapa iwe imeshathibitika kuwa wameshafungishwa virago.
Mwanangu HENRY14 punguza roho mbaya basi, ukizeeka hatupendi kukuona una macho mekundu.
Ila Arsenyau mambo yakiwanyookea jukwaa lenu hua amani inatawala aiseee.
Hongereni sana wanangu wenyewe kabisa The gunners, ila huko mbele mnakoelekea nawakumbusha tu mtaenda kukutana na kina Bayern Munich.
 
Bro, kwenye kundi lako mpinzani wako ni Bayern tu, na Hamisi aka chambuzi nguli alishaambia huyo bayern mwenyewe wa sasa maharagwe ya mbeya tu. Sasa nyie wenyewe mmelifanya kundi lionekane gumu halafu unakuja kuongea kuhusu hili letu. Mngetaka hilo kundi mngeliongoza, ila hamkutaka.
Bayern Jana kaweka full mkoko against Copenhagen na hajashinda na alikuwa nyumbani

Mechi ya kwanza Copenhagen pia alikuwa vzr dhidi ya Bayern

Hilo kundi Lao Lilikuwa mchekea sana
 
Mwanangu HENRY14 punguza roho mbaya basi, ukizeeka hatupendi kukuona una macho mekundu.
Ila Arsenyau mambo yakiwanyookea jukwaa lenu hua amani inatawala aiseee.
Hongereni sana wanangu wenyewe kabisa The gunners, ila huko mbele mnakoelekea nawakumbusha tu mtaenda kukutana na kina Bayern Munich.
Hayo ya mbele tutashughulika nayo tukifika huko. Huenda hata tukatolewa 16 bora tu hapo. Ila nyie bado tuna hasira nanyi juu ya ile 3-1 ya pira janja janja na ile picha ya masebene mliokuwa mkiipost huku kutuchafulia uzi wetu.
 
Amini mkuu hilo ni suala simple sana kwenye group lao. Group liko wazi mno. Bayern naona amefaidi kwa kutangulia kwa kushinda games ila kufungika anafungika. Nyumbu wakaze tu wampige bayern. Hao wengine wataumana sana jino kwa jino maana wote wanataka kufuzu na hatimae wataishia kutoka sare
Mangungu Fc kumfunga Bayern hizo ni ndoto labda hongo itembee, na suala la hao wengine kudraw sahau.
Mimi binafsi natamani hata hio yuropa tusiende kabisa, tukomae na ligi tu tupambanie hio top 4.
 
Bayern anapigika vizuri tu. Changamoto ni hao wahuni wengine. Atakayempiga mwenzake anafuzu bila kujali matokeo yenu Nyumbuz na hao walevi wa Bavaria
 
Bro, kwenye kundi lako mpinzani wako ni Bayern tu, na Hamisi aka chambuzi nguli alishawaambia huyo bayern mwenyewe wa sasa maharagwe ya mbeya tu. Sasa nyie wenyewe mmelifanya kundi lionekane gumu halafu unakuja kuongea kuhusu hili letu. Mngetaka hilo kundi mngeliongoza, ila hamkutaka.
sio suala la kutaka broo, ukweli ni timu letu mpaka dakika hii halieleweki, sio kocha wala wachezaji.
Hakuna kitu inaniuma kama kushindwa kushikilia bomba, yaani timu letu hata likiwa linaongoza kwa goli 3 - 0 bado mashabiki tunashikilia roho mkononi mpaka mpira uishe.
 
Mangungu Fc kumfunga Bayern hizo ni ndoto labda hongo itembee, na suala la hao wengine kudraw sahau.
Mimi binafsi natamani hata hio yuropa tusiende kabisa, tukomae na ligi tu tupambanie hio top 4.
Bayern atafanya makusudi awazabue

Nyumbu Sasa hivi kombe lenu ni top 4, akili zimeanza kuwarudi Sasa. Safi sana
 
Hayo ya mbele tutashughulika nayo tukifika huko. Huenda hata tukatolewa 16 bora tu hapo. Ila nyie bado tuna hasira nanyi juu ya ile 3-1 ya pira janja janja na ile picha ya masebene mliokuwa mkiipost huku kutuchafulia uzi wetu.
Mkuu kwani hio 3 - 1 si tayari tushamalizana?
Au bado hamjaridhika na zile goli 3 - 1 mlizotufunga msimu huu pale Emirates?
Mimi nawashauri mechi ya marudiano pale Old Trafford komaeni mtufunge walau goli 8 ili mfute ile fedheha ya kuitwa Arse8.
 
sio suala la kutaka broo, ukweli ni timu letu mpaka dakika hii halieleweki, sio kocha wala wachezaji.
Hakuna kitu inaniuma kama kushindwa kushikilia bomba, yaani timu letu hata likiwa linaongoza kwa goli 3 - 0 bado mashabiki tunashikilia roho mkononi mpaka mpira uishe.
Si ndiyo maana yenyewe ya hamkutaka hiyo sasa 🤣. Kama jana kwa nini hamkucheza tu game lenu bovu la janjajanja la kupaki basi na kuvizia counter? Mkaanza kujiona eti na nyie mnaweza kama wengine mkaanza kupishana na wale wanaOttoman. Mkawapa confidence, mwishowe mkapoteza points 2.
 
Natamani sana Nyumbu watolewe na tena wasienda hata Europa. Ila group lao lilivyo, daah, wana chance ya kushika nafasi ya 2 kama wakimpiga Bayern na Copenhagen na Galatasaray wakitoka sare. Siyo poa kabisa. Nilitaka mpaka hapa iwe imeshathibitika kuwa wameshafungishwa virago.
Bayern jana naamini kafanya makusudi, lengo lake ilikua ni kufungwa kabisa ili aue possible rival huko mbele ni vile copenhagen hawakukomaa zaidi
 
Mkuu kwani hio 3 - 1 si tayari tushamalizana?
Au bado hamjaridhika na zile goli 3 - 1 mlizotufunga msimu huu pale Emirates?
Mimi nawashauri mechi ya marudiano pale Old Trafford komaeni mtufunge walau goli 8 ili mfute ile fedheha ya kuitwa Arse8.
Bado hatujaridhika aisee. Tena hiyo ya marudiano tunatamani tuwapige kama hawa Lens. Kwa maneno ya mkorea , 'heshima irudi'. Ila pale unyumbuni naona mna mali aisee. Kale ka Garnacho tupeni basi kaje kusugua benchi. Akitoka Martinelli kaingie. Huyo Fernándes pia tupeni tumuweke bench ili akitoka Kai, Bruno aingie.
 
Back
Top Bottom