Daaah unanikumbusha mbali sana
Naandika, nafuta. Naandika tena nafuta. Nina vingi Sana vya kuelezea kuhusu mpira
Tukio langu ambalo sitalisahau. Ilikua tanga muheza nilienda likizo kwa bro kipindi hiko nipo form six
Sasa mtaani pale kulikua na timu alafu kulikua na mashindano ya kombe limedhaminiwa na mbunge
Nikawa kwenye mazoezi naenda kupiga nao tiz, siku kwenye mechi naenda na mm kuangalia (pale pale muheza Mjini) uwanja upo karibu na hospital
Siku ambayo chama langu lipo uwanjani, Kama kawaida tukawasili uwanjani (hapo Mimi Kama mbeba maji ya wachezaji)


Mpira ulikua mkali Sana siku ile(tanga Wana vipaji Sana

)
Dakika ya 70 wachezaji wetu wawil waliumia namba nane na winger, sub moja ya winger ikapatikana
Ila huyu kiungo wachezaji walikua hawaiwez ile namba sijui ata sielewi
Mara kocha akaniita oya MKOREA vaa jezi kwasababu hauna tiz, kacheze namba 10. Namba kumi aje nane
chamsingi saidi kukaba tu.
Kumbuka Hadi hapo timu tulikua tunacheza nao ya kutokea amani/amana tupo moja moja
Nikaingia, kabumbu likaanza. kupiga One two one two Sana tu
Sasa damu ikachemka nasambaza upendo tu, zikitokea faulo au Kona huwa nakaa area ambazo mpira uki-bounce zile dead balls zinanikuta
Sasa Kuna Kona ilikua tunapiga dakika za lala salama, Mimi nikaka nje ya box. Ule mpira kipa aliutema huku yeye mwenyewe akaangua ukanikuta nipo on move
Ilisikika sauti moja tu 'misssssss' nilikandamiza shuti kimoja Cha mbuzi na kipa alikua ameanguka ule mpira ulipita kama upepo
Ubao unasoma 2-1
Mpira umeisha kocha ananiuliza ndio wewe au? Mbona haukusema mkorea



.
.
Kwenye mpira huwa nacheza namba nane, nikipatiwa namba sita mzuri kwenye kukaba na winger zinazotembea unaweza ukasema pirlo ana mdogo wake huku bongo
Pia napenda Sana kupiga, zile za Steve Gerald
Sehemu kubwa ya mpira nimecheza kishule shule zaidi, hizi zamchangani sijui ndondo nilikua zisikubali kabisa
Na ata nilivyokua mdogo, nyumbani wakisikia nimecheza mpira tena maeneo ya mbali ni msala, Yani nilizaliwa ili nisome kwaio nachangiwa na watu wawili mke na mume wake kwenye kupigwa

Kuna siku nilishuhudia pale kajiungeni Kama unaenda chanika mtu anavunjika mguu Kama kuni hivi kwa rafu ya makusudi kabisa. I was so sad, kama nimefanya Mimi hivi
Umiseta nilifika Hadi kibaha. Ila Bongo nyoso sana wazee kmmk. Tulioandikwa majina Tukaambiwa tutaitwa/kupigiwa simu. Hadi Sasa nasubilia huko kuitwa