Kwanza kabisa Gunners hongereni kwa kumfunga City maana alizoea kuwanyanyasa muda mrefu sana. Nashindwa kujua furaha yenu imejengwa na kumfunga City au kukaa juu ya City kwenye msimamo wa ligi?
Katika hoja zote 2 hapo juu ni kwamba mnaizidi City point 2 pekee wakati ndio kwanza mechi ya 8 ya msimu. Kama experience ni mwalimu mzuri,msingefiria ubingwa katika kipindi hiki kwa ubabe wenu wa point 2 dhidi ya City.
Ijumaa niliongea humu kuhusu udhaifu wa sasa wa City kwa sasa ya ukos3fu wa wachezaji wake muhimu watu wakasema City sio mchezaji bali ni mfumo uliotengenezwa na plan na mbinu za Pep,ni kweli lakini mwisho wa siku ili hilo dude lifanye kazi linahitaji watu sahihi wa kuliendesha,hapo ndipo unakutana na brain za De Bruyne,silva pamoja na Rodri. Jana Silva kacheza lakini hakuwa kwenye kiwango chake sababu nadhani za majeruhi au kutu ya kutokuwepo uwanjani kitambo kidogo au alikosa muunganiko aliouzoea toka kwa machine De Bruyne na Rodri.
Nafasi ya Rodri alicheza Kovacic angalia utumbo aliokuwa anaufanya uwanja ila Pep alikosa mbadala tu,nusura aigjatimishe timu kwa Red card. Rico William ndio alicheza nafasi ya De bruyne,hakuna mfanano wa hata 60% kiubora kwenye eneo hilo ndio maana Haaland alionekana kama Benteke tu. Hakuna huduma ya maana ilikuja kwake kutokana na uchezaji wake. Hata hizo 4 shots off target niliona zimechezwa na wchezaji wengine tu.
Kwahiyo Gunners wakati mnafurahia kumfunga City jana,kumbukeni wachezaji wake 2 hawakuwepo na mmoja ndio kwanza katoka majeruhi muda si mrefu.