TEMBO YULEEEE .!! TAWI LAKE ANALITAKA
Mechi ilikuwa tight sana ni kama vile hakuna mtu aliyetaka kupoteza kwa muda mrefu mpaka nafikiri dakika 25 za mwisho ndio uliona Arsenal wanazitaka zaidi pointi 3 kuliko City na wamestahili kwa hilo
Kipindi cha kwanza kila mmoja alikuwa na mapungufu hasa wakivuka mstari wa kati
ARSENAL :
Kama ukiwa pressed katikati ya uwanja basi njia nzuri ni pembeni ya uwanja na hapo ndio kipindi cha kwanza walimiss sana huduma ya Saka na Martinelli kwenye 1v1 na fullbacks wa City , ndio maana walikuwa wanatupa sana mipira hasa wakikaribia katikati ya uwanja
MAN CITY
Walikuwa wanaishinda pressing ya Arsenal lakini tatizo lao kubwa ilikuwa mbele wamebana uwanja ( Foden Alvarez na Lewis ) walikuwa karibu karibu sana katikati ya mstari wa ulinzi na kiungo wa Arsenal na matokeo yake pembeni ya uwanja waliwaachia Walker na Gvardiol ambao sio wazuri sana kama attacking fullbacks
Kipindi cha pili baada ya kuingia Martinelli lakini hasa hasa Partey ndio naamini mechi ilianza kuwa ya Arsenal zaidi , kwanini ?
1: Partey mzuri zaidi ya Jorginho dhidi ya Counter attacks maana yake anawapa uhuru fullbacks na viungo wa Arsenal kusogea juu zaidi
2: Partey ana uthubutu wa kupiga pasi za mbele zaidi kuliko Jorginho anayependa pasi salama
3: Hapo ndio Arsenal walipoanza kushambulia kwa idadi kubwa zaidi ya wachezaji maana yake City wanakuwa mbali na lango la Arsenal hata wakipata mpira
NOTE
1: Kovacic kaponaje na kadi nyekundu ?
2: Raya ana bahati sana ameenda mapumziko bila kuruhusu goli alikuwa na mchecheto sana
3: Rice Rice Rice
ndio maana City nao walimataka
4: Gvardiol
anajua boli
5: Haaland kwani alikuwepo uwanjani ?
Saliba roho mbaya sana
6: MARTINELLI MATCH WINNER
FT: Arsenal 1-0 City
AMBANGILE