Execute
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 3,005
- 7,375
Nawashangaa ndugu zangu wa Arsenal kuwa na matumaini msimu huu. Mimi nilishamaliza baada ya komenti hii. Kitendo cha kumsajili Kai basi nilishaona hamna jipya pale.Arteta amenisikitisha sana kumsajili Kai Havertz. Hii inaonesha kwamba mpaka sasa hajafahamu mahali tatizo la Arsenal lilipo.
Paundi 65m kama angetulia na akaziongezea kwa kumuuza Balogun, Tavares na Nketiah angeweza kumleta pale Osimhen. Kai sijui amemleta kufanya nini.
Usajili wa Declan Rice na Timber ni mzuri na kwa sehemu utasaidia kuimarisha kiungo na ulinzi lakini still Arsenal inahitaji goalkeeper ambaye yupo serious.
Wachezaji wa kawaida kama Reiss Nelson, Fabio Vieira, Rob Holding, Cedric Soares, Nicolas Pepe na Sambi Lokonga wanatakiwa kuondolewa haraka.
Msimu ujao nategemea Arsenal itabakia kwenye top four lakini masuala ya ubingwa tuendelee kuyasahau.
Arsenal itabakia top 4 lakini kamwe haitabeba ubingwa wa epl chini ya Arteta. Huyu kocha ni wa mid-table teams, hana uwezo wa kushindania makombe makubwa.