Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Waite mkuu
Huwa wanatutambia Sanaa....ile Pre season ya Marekani iliwadanganya🤠🤠🤠...ww tangu 2017 hujawahi kushinda pale Emirates unapataje jeuri ya kuja kutupigia kelele hmu🤠🤠🤠...bila kumsahau Labyrinth 84...aje naye tudiscuss....maana kama namuona alivyoshangilia goli la Garnacho baada ya jana kumpiga mabango na kile kikundi chake cha Marathon Nyukesto🤠🤠🤠
 
Tufurahie ushindi wana Gunners.

Ni point 3 kubwa.

Lakini pia tukumbushane au tuekane sawa, msimu huu tupunguze matarajio makubwa.

Kwa namna tunavyocheza haivutii kama ilivyo msimu uliopita na naomba nimlaumu Arteta moja kwa moja, yeye ndio tatizo.

Twende kwenye international break, lakini tujue timu yetu bado. Ina safari ndefu. Tusijipe false hopes!
 
Arteta ni mpuuzi sana anavyolazimisha HARVETZ acheze,hii mechi ilikuwa na magoli mengi tangu half ya kwanza
Havertz amechukua nafasi ya Xhaka na ataweza kuwa sawa.

Anatakiwa awe na maelewano mazuri ya Zinchenko upande wao wa kushoto.

Atakuwa sawa tu na atafunga magoli kama ilivyokuwa kwa Xhaka.

Mpira wa wenzetu ni mipango na mifumo na ili kuipatia kucheza yatakiwa uwe na ustahamilivu.

Meneja ana imani na Harvetz na atakuwa acheza kila mechi ili kufit in katika mfumo wa uchezaji wa Arsenal.

Ila huko mbele Jesus atarudi kuanza mechi na Nketia atarudi bench.

Pia hali ya hewa kulikuwa na joto kali hivyo kuathiri uchezaji kwa kuufanya uwe slow sana.
 
Tumeshinda lakini tumecheza mpira low quality sana
Hii game angeanza Jesus ingeisha half time ,najua ilikuwa ngumu kumpiga bench nketiah sababu ya form yake

Saka hakuwa mchezon kabisa leo

Kai bado anatafuta confidence kucheza double 8 anazidi kuzoea

Declan Rice what a player

Zinny atapiga pass za mbele Hana show mbovu

Vieira Ni muda Sasa aingie first eleven,alisakamwa Sana tukasimama nae kidete ,siku zote naamini katika talent
 

Now you are talking my friend
 
Bro,kwa HARVETZ ndipo uwezo wake ulipoishia,ile move ya goli la Jesus kwa mfano nina uhakika angekuwa Harvetz asingeweza kufanya vile,Harvetz inatakiwa acheze mechi za CARABAO huko ili apate fitness kwa kuwa sasa anacheza kwa pressure na sio kulazimisha aingie moja kwa moja kwenye Timu,ni mzigo kukaba kwenyewe anakaba kwa macho,kuna goli alikosa hata mtoto wangu wa darasa la pili angefunga
 
Mwanzo mzuri,pole kwa Man.U,huo ndio mchezo,endeleeni kujipanga ili next time angalau tuwapunguzie kidogo magoli...
 
Havertz wengi wadhani ni striker au "deep lying midfielder" jambo ambalo si sahihi.

Arteta ataka Havertz awe analink mchezo kati ya Zincheko na Ben White na awe anakuja mwisho kumalizia shambulizi kwa kufunga goli.

Ndo maana mechi zingine zilopita amecheza kama "false 9" au attacking midfielder nafasi ambayo leo amecheza Odegaard kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kufunga goli la kusawazisha.

Hivyo Havertz ni "deep lying midfielder", Odegaard ni attacking midfielder na Declan Rice ni central Midfielder nafasi ambayo ilikuwa ni ya Thomas Partey.

Havertz atakiwa sasa akazanie kujifunza kutopoteza mipira sana na pia kutokuwa slow kwenye kulink mchezo.

Hivyo mechi ijayo na Everton utashangaa Arsenal ikiwa ni timu ingine kabisa kwa kutumia mfumo mwingine ili kumzuia Sean Dyche asicheze "10 men behind the ball" kisha kuvizia kufanya counter attack kama alivyokuwa akifanya Rashford leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…