Hii formation haitofanya jipya. Naelewa Arteta anajaribu kuwa unpredictable lakini kwa mfumo huu atatu-cost points nyingi msimu huu.. aache kabisa, turudi kwenye mfumo wetu.
Pia aache kujaribisha wachezaji, iwe kama alivyosema- alieko tayari ndie acheze!
Kwa Havertz ashafeli, akubali akae benchi nae ajifunze.
Tuna kipa mzuri kwenye benchi, Raya, na yeye anajua lakini bado kamng'ang'ania Ramsdale.
Mbona simple tu:
Kipa aanze Raya, Zinchenko awepo na back 4 inayomjumuisha Gabriel Magalhaes
Kati Partey, Ødegaard na Rice. Pembeni Saka na Martinelli. Japo Martinelli anatakiwa a-improve game yake. Vile vile yuko predictable sana.
Mbele Jesus au Nketiah.
Kai mkeka ili ajifunze.
Turudi kwenye mfumo wetu wa 4-3-3.