. Ambangile

Mechi nzuri sana imechezwa leo , timu zote mbili zimetendea haki wapenda soka wote

Arsenal bado na muundo wao ule ule wa 3-Box midfield -3 ( yani 3-2-2-3 ) White Saliba na Tomiyasu wanabaki nyuma , Partey anatoka kwenye namba 2 mpaka kwenye kiungo kuwa na Rice wakati Kai na Odegaard namba 8 wawili na utatu wa Martinelli Nketiah na Saka ...kwanini ?
1: Kwasababu Palace walikuwa wanazuia na 4-4-2 maana yake Edouard na Eze anajikuta wana press mabeki watatu wa Arsenal 3 Vs 2 na kwenye kiungo wapo wawili Lerma na Doucoure dhidi ya wanne wa Arsenal
2: Lakini walichofanikiwa Palace ni kwamba Lerma na Doucoure waligoma kuwa press Rice na Partey badala ya Edouard na Eze walishuka chini kuwazuia Partey na Rice na kuwaacha BACK 3 wa Arsenal huku Lerma na Doucoure ni kuzuia space nyuma yao dhidi ya Kai na Odegaard.
3: Suluhisho ni Arsenal ku switch mpira haraka sana kutoka upande wa Saka mpaka Martinelli na Viceversa ili kuwafanya wapate 1v1 dhidi ya fullbacks wa Palace .

Kilichowaangusha Palace ni kushambulia kwa idadi ndogo ya wachezaji kwenye penati box la Arsenal kabla ya Arsenal kuwa wachezaji 10 ( kadi nyekundu ya Tomiyasu ) , walikuwa wakishambulia kwa 4-2-3-1 krosi zote za Ayew zilikuwa hazina wamaliziaji ni Edouard pekee ndio yupo ndani ya Box badala ya Eze , Schlupp na kiungo mmoja baina ya ( Lerma na Doucoure ) kuongezeka kushambulia

Baada ya kadi nyekundu kwa Arsenal , vijana wa Arteta waliamua kulinda walichonacho na walizuia vizuri sana kulingana na kile ambacho Palace walichokuwa wanauwauliza .
NOTE
1: Doucoure najua kwanini Liverpool wanamtaka , kiungo mzuri wa ulinzi
2: Saliba ni kitasa aisee, kasi nguvu uwezo wa kusoma mchezo mtulivu akiwa na mali mguuni . Mara moja alifanya kosa na akasawazisha mwenyewe
3: Nketiah hajafunga goli lakini kazi zingine zote kafanya vizuri sana hasa kushuka kwenye namba 10 , touch and turn
4: Declan Rice ... a very good game kacheza
5: Eberechi Eze , hana muda mrefu ndani ya Palace huyu
FT: Palace 0-1 Arsenal