Shukrani
mkorea kwa Mwaliko,
hamis77 we Jamaa nakuwaga interested na Comments Zako, Nimeona Michango Mingi ya waja Huku kuhusu Game ya ArsNott, Honestly hakuna kipya nje ya last Season Game ambayo Arsenal wanapoteza 1-0, ile Game Partey alianza nafasi aloanza Game ya jana na kati walikuwa Xhaka, Jorginho, Ode, CB's Kiwior, Gabriel na White. So kiuhalisia kama amekuja na Mfumo Ule ule alopoteza nao Game, na sababu kubwa ya Arsenal kupoteza ilikuwa kichwani zaidi kuliko habari za Mifumo tofauti wakati ule kwa Arsenal Notts walikuwa na World Class GK in Navas!
Mimi naungana na baadhi ya wachangiaji kwenye Uhitaji zaidi wa Arsenal{CB na CF} Fergie alishapitia mambo mingi mpaka kufikia hatua ya kusema
"Attack wins you Games, Defense wins You Titles" Pep na sifa zote karibu Madirisha yote huwa anaboresha Def na sasa kaleta lile Jini Josko {Hapa wengi mtasema kuhusu Timber but Arsenal ukitoa Saliba wanaomkaimu Ubora unapungua sana, Injury yake Imewacost Ubingwa, Jesus anaumia lakini Gari Ars lishawaka na still timu inapata Matokeo, Zile Big Figures Nyuma hazina cha maana akikosekana Saliba} Timber Mchezaji na nusu but anapenda sana Duels kwa EPL kuwa salama season yote Ni kudra tu,
ARS players wengi walikiri kabisa ile kukosa Title ni mentality zaidi, Hapa Experince inafanya kazi zaidi, kama ARS ingekuwa na Mwalimu kariba ya kina PEP, KLOPP et al, wangekuwa na Title mda huu. Leicester walijikuta nafasi ambayo hawakuitegemea wakianza season, ilibidi uzoefu wa kina Ranieri ufanye kazi zaidi ya Uwezo wa Players,
Kuna kitu ki1 nakionaga sana kwa walimu wenye asili ya Kispanish, "EGO" Pep alikuja akataka tuaminisha angeiweza EPL Bila Natural CF, Na aliweka sababu nyingi kwamba Aguero haezi Press, Mwisho Kun ndo alimpa mataji karibu yote, amekuja pata Treble baada ya kusajili CF. Ila awali alituteletea kina Nolito, akaanza amini kina Negredo and Co. Luis Enrique alishndwaga Roma na Celta hivyo hivyo, Case yake Barca ni tofauti {Hakuna mwalimu wa daraja la kati mpaka juu angeshindwa chukua kila kitu na Neymar, Messi na Suarez tena wakiwa kwenye Peak yao} Enrique kachukua Spain anawaacha Alcantara na kina Ramos, hata kama asingewapanga wale washazoea mataji wanajua jinsi ya kuhandle Pressure, hana cha maana kafanya nayo,
Narudi kwa Mikel, Huyu jamaa ana Potential ya kuwa the Best Manager kwa kipindi kifupi kinachofata, ila asipotoa "EGO" wako naye wenzake na yeye ni mhanga anayo, ARS Inahitaji CB wa kiwango na CF wa uhakika then inakuwa ni Force haswa, mana City unaweza wabana ila Haaland anaweza kufunga hata 3 ndani ya dk 20, ukitaka makombe unatakiwa kuwa na watu hawa, Jesus mchezaji na Nusu ila unakuwa na Plan B ya kina Nketiah ni uongo,
Nahitimisha kwa Suggestion za mimi ARS ilimtaka sana Dusan Vlahovic, Bei yake ishajulikana sasa Pauni 45~60 unajibebea, then unakuwa na Beki mwingine wa kati mwenye Uwezo wa kueleweka Pembeni ya Saliba, hapa nadhani wa Bei za kawaida na ubora juu kuna Nico Schlotterbeck, Facundo Medina au Bastoni.
Mikel Game ya mwisho ya Msimu ulopita ilikuwa Emotional sana kwake na Mashabiki hata kuongea ikawa tabu Emirates, Fans walikuwa wana-Applauds karibu dk na zaidi, Sababu aliwafanya waamini tena, alizidi malengo ila msimu huu wanaamini wanaweza ni mapema sana but ARS inahitaji CF wa maana kuwa Force kamili, Msimu huu wanaamini tuna kitu ila karata ni za kuchanga vyema mana mashindano anakuwa yote ni ya Maana huwezi sema unapotezea moja kubaki na lingine kama ilivyokuwa kwa Europa, kwa sasa Emirates kamziki cha Ligi ya Mabingwa katasikika.
Inatosha waja naomba Kai iwe mada ya wakati Mwingine!